BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,831
- 287,782
10/5/2007
*Mgodi wa Buzwagi waitwa Kabwe Gold Mine
Na Shija Felician, Kahama
Mwananchi
WAKAZI wanaoishi kuzunguka eneo la Mgodi wa Buzwagi, wamelibadili jina la Mgodi huo na kuuita Kabwe Gold Mine.
Hali hiyo ilibainika baada ya waandishi wa Habari kutembelea eneo hilo na kukuta mabango yakionyesha maandishi jina hilo.
Kuitwa kwa jina hilo, kunatokana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zito Kabwe kupinga kusainiwa kwa mkataba wa mgodi huo nchini Uingereza na kusababisha kupewa adhabu ya kutohudhuria vikao vya bunge.
Baadhi ya wakazi waliohojiwa kuhusu jina hilo, walidai wameamua kuuita hivyo, kwa sababu mbunge huyo anajali maslahi ya wakazi wa Buzwagi.
Tumeamua kuuita Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi kuwa Mgodi wa Kabwe tukiwa na maana ya kwamba huo ndio uliosababisha Mbunge huyo akafukuzwa bungeni, " walisema kwa nyakati tofauti.
Kumekuwa na malumbano ya kisiasa takribani miezi mitatu kuhusu utata wa ufungaji wa mkataba huo wa Buzwagi uliofanywa baina ya Kampuni ya Barrick na Serikali ya Tanzania hali iliyosababisha baadhi ya wanasiasa kuchukua nafasi hiyo kujipatia umaarufu wa kisiasa.
Baadhi ya Wabunge wa Kanda ya Ziwa wamekuwa wakizomewa mara kwa mara na wananchi wao pindi wanapozungumzia mgogoro huo kwenye mikutano ya hadhara.
Wanachi hao wanauzunguka Mgodi huo wamekuwa wakimsifia Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwani kwa sasa wanamuona kama mkombozi wao.