- Source #1
- View Source #1
Salaaam wanajukwaa
Nimekutana na video inaonekana kama imepostiwa na Jambo Tv, kichwa cha habari kinasema wananchi wamkosoa Lissu, video hiyo inapoendelea kucheza naona kuna comments zinapop up, Je video hiyo uhalisia wake ni upi wakuu?
Nimekutana na video inaonekana kama imepostiwa na Jambo Tv, kichwa cha habari kinasema wananchi wamkosoa Lissu, video hiyo inapoendelea kucheza naona kuna comments zinapop up, Je video hiyo uhalisia wake ni upi wakuu?
- Tunachokijua
Tundu Lissu ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA tangu mwaka 2019 alipochaguliwa kutumikia nafasi hiyo, pia alikuwa mbunge wa jimbo la Singida mashariki kuanzia mwaka 2010 mpaka mwaka 2020 ambapo wagombea wengi wa upinzani hawakufanikiwa kushinda nafasi mbalimbali wakati wa uchaguzi huo.
Lissu ni mwanasiasa anayesifika kwa haiba yake ya kuwa muwazi na msema kweli huku akiwa mkosoaji wa ukiukwaji wa haki za binadamu, demokrasia na masuala mbalimbali yenye maslahi kwa umma.
Mara kadha wapotoshaji wamekuwa wakitumia kauli za Lissu kupotosha uhalisia wa yale yanayosemwa na Lissu juu ya masuala mbalimbali hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27, 2024. Unaweza kurejea hapa, hapa na hapa.
Mnamo tarehe 21 Novemba 2024 Lissu alifanya mkutano wa hadhara na wananchi wilayani Tarime mkoa wa Mara ili kuwanadi wagombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
View: https://youtu.be/o26xw6MDhlA?si=JnZEDxuTuqUqKGm7
Kutokana na mkutano huo kumeibuka video inayodaiwa kuchapishwa na Jambo TV ikisambaa mtandaoni ikiwa na kichwa cha habari kinachosomeka “wananchi wamkosoa Lissu” huku video hiyo ikiambatanishwa na jumbe mbalimbali zinazodaiwa kuwa ndiyo wananchi waliomkosoa Lissu.
Je ni upi uhalisia wa video hiyo?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kupitia utafutaji wa kimtandao umebaini kuwa video hiyo imepotoshwa uhalisia wake kutoka kwenye video halisi iliyochapishwa na Jambo TV ikiripoti kutoka mkutano uliofanywa na Lissu Tarime Mkoani Mara. Video hiyo imepotoshwa kwa kuwekewa kichwa cha habari kinachosomeka “wananchi wamkosoa Lissu” tofauti na video halisi yenye kichwa kinachosomeka “Lissu akosoa uokoaji wahanga Kariakoo”
Kadhalika video hiyo imeongezewa jumbe zinazodaiwa kuwa ni za wananchi wanaomkosoa Lissu tofauti na Video halisi ambayo haina jumbe hizo za maoni zinazotokea kwenye video hiyo.
Hata hivyo video iliyopotoshwa ambayo haikuchapishwa katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya Jambo TV imebainika kuwa na mapungufu kadhaa ukilinganisha na machapisho halisi ambayo hutolewa na televisheni hiyo ya mtandaoni, sehemu ya mapungufu hayo ni pamoja na kutofautiana kwa mwandiko (fonts) uliotumiwa kuandika kichwa cha habari pamoja na mpangilio wake.