Wananchi wamemchoka JK?

nsami

Senior Member
Jun 11, 2010
175
8
Leo tukiwa tunaenda job asubuhi kwa gari lakzini ( Staff bus) tukawa tunasikiliza dondoo za magazeti mara kikasomwa kichwa cha habari katika gazeti la Raia Mwema chenye muundo wa swali kuwa "JK Kuongezewa muda?" watu karibu wote basi zima wakaguna na kusema "mmmh tena? inatosha!" Mara ukaibuka mjadala humo ndani huku watu wengi wakisema hawataki kusikia hiyo habari.

Swali ni kwamba ni kweli wananchi wamemchoka mheshimiwa kiasi hicho? Na je hali ikoje katika eneo ulilopo?
 
Kiongozi!

Mbona unauliza jibu? Mbona hata mwenyewe analijua hilo na ndio maana kila kukicha kiguu na njia!
 
Kama kungekuwa na uwezekano wa kuona mioyo ya watz waliosikia hiyo dondoo kwa wakati huo "ungeshangaa".
 
Mkuu haya mawazo mengine huwa yanatoka wapi jk anamaliza uongozi wake 2015 haya mengine ni porojo tu za wanahabari kutaka kujaza gazeti.
 
Waliomchoka ni wale ambao hawajafaidi urais wake. Ebu mwulize Mbatia kama na yeye kamchoka?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Sie pande za huku bado tunahitaji uongozi wake. Ni kiongozi bora aliyetoa uhuru mkubwa wa raia wake kusema watakacho. Kiongozi yupi aliyewahi kutoa uhuru wa namna hii.?
 
Waliomchoka ni wale ambao hawajafaidi urais wake. Ebu mwulize Mbatia kama na yeye kamchoka?

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
Au michuzi
Huhu pasco wa JF akisubiria kuponda raha zamu yake kwa hamu.
 
...Mchezo unaanzia kwenye rasimu ya wachache iliyopo ubaoni!kama walio wengi walitaka serikali 1 na 2 iweje waje na rasimu ya serikali 3!

Kupoteza muda,ikataliwe warudi tena,waje na serikali 2...(Lengo wanalijua wao) kuwashikisha adabu upande wa pili!maana wanajua kwa bajeti yao ya 660Bil na mapato ya 120Bil kwa mwaka!hawawezi kusimama wenyewe na kuchangia Muungano!

Hizi ni dana dana na chenga twawala!ngoma itarudi ubaoni!hadi 2015 itakuwa bado tunarumbana tu!....ndio maana CDM wameikubali wakijua mchezo unaochezwa!kuwa CCM wataikataa ili kupoteza muda!
 
Mkuu hili la mheshimiwa kuchokwa mbona lipo, naamini hata ndani ya chama chake wapo wanaosema mbona miaka haiendi huyu bwana akamaliza muda wake, ila kama waliosema wengine wapo wanaosema dah akitoka huyu mirija imekatika na hawa ni wale wasiovna cv lkn wamekalia ofisi kiushkaji.
 
Sie pande za huku bado tunahitaji uongozi wake. Ni kiongozi bora aliyetoa uhuru mkubwa wa raia wake kusema watakacho. Kiongozi yupi aliyewahi kutoa uhuru wa namna hii.?

Uhuru huu wa kupigana mabomu ya machoz tumboni? wa kung'oana kucha? kumwagiana tindikali na kubambikana rushwa?
km tunasema tutakacho ni technology imetupa uhuru sio Kikwete. Ghaddafi kang'olewa kwa msaada mkubwa wa mitandao ya kijamii angeweza angezuia.
pia wananch wengi sasa tunajua haki zetu na namna ya kuzidai ukizingua we make a hell lot of noise.
labla tu tumsifie kikwete kwa uoga, jamaa anaogopa sana kelele.
 
Mimi alinishangaza alipompandisha cheo Kamuhanda. Hata wakati ambapo familia ya Mwamgosi hawajasahau maumivu ya kumpoteza mpendwa wao.
 
Ndugu yangu lisemwalo lipo, kama halipo laja, walianza mara baada ya uchaguzi 2005, mbunge akasema kipindi cha raisi kiwe miaka 7, Lupumba nae kesha sema, kama alikurupuka au alimaanisha, sijui

Mkuu haya mawazo mengine huwa yanatoka wapi jk anamaliza uongozi wake 2015 haya mengine ni porojo tu za wanahabari kutaka kujaza gazeti.
 
Back
Top Bottom