Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,898
2008-03-24 10:47:05
Na Mary Edward, PST Dodoma
Wananchi wa Kijiji cha Iringa Mvumi Wilayani Chamwino, mkoani hapa, wamegoma kuchangia miradi ya maendeleo hadi uongozi wa kijiji hicho utakapowaeleza zilipo Sh. milioni 21 walizochangia kwa ajili ya ukarabati wa ghala la chakula.
Ghala hilo sasa limegeuzwa kuwa madarasa ya wanafunzi wa sekondari ya kata hiyo.
Wakizungumza na PST ilipotembelea kijiji hicho, wananchi hao walisema, fedha hizo zilichangwa na wananchi kwa ajili ya kulifanyia ukarabati jengo hilo, lakini hadi sasa limepakwa rangi tu ambapo gharama zake hazifiki Sh. 500,000.
``Tulikubalina na uongozi wa kijiji kuchanga Sh. milioni 21 ili kufanya ukarabati wa jengo hilo, kwa ajili ya kupata vyumba vya madarasa, lakini cha kushangaza hakuna ukarabati uliofanyika,.. badala yake limepakwa rangi tu`` alisema Bw. Sinai Chimagu.
Uamuzi wa wanakijiji kususia kazi zote za maendeleo katika kijiji hicho, unatokana na uongozi kushindwa kuwasomea mapato na matumizi ya kijiji hicho.
Pia walilalamikia kitendo cha viongozi wa vijiji kuwabambikizia kesi wananchi wanaoonekana kuhoji fedha hizo, kwa lengo la kuwanyamazisha na kuwatisha wananchi wengine, wasiendelee kuhoji suala hilo.
Mwananchi mmoja, Bw. Dikson Nyamwanji aliambia PST kuwa, aliwekwa mahabusu kwa siku tano kutokana na kutaka kujua hatua za ukarabati wa jengo hilo, ambalo kwa sasa imegeuzwa kuwa shule ya Sekondari ya Kata inayojulikana kwa jina la Makwama.
Naye Mkuu wa Sekondari hiyo, Bw. Samwel Chimoche alisema, hata mkandarasi aliyepewa tenda ya ukarabati wa jengo hilo, inaonyesha ameshirikiana na uongozi wa kijiji, kwani ukarabati huo haulingani na thamani ya fedha.
``Sh. milioni 21 zilizochangwa na wananchi ni nyingi kulingana na ukarabari wenyewe,.. jengo hili ni jengo la zamani ambalo lilikuwa ghala hapo awali, na lilitakiwa kuwekwa madirisha, kupakwa rangi na mambo mengine, lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika,`` alisema.
Mkuu huyo wa shule, alimtaja mkandarasi huyo kwa jina moja tu la Bw. Chamgeni, na kusema kuwa, hadi sasa hajulikani alipo, lakini uongozi wa kijiji na kata bado unaendelea kulinyamazia suala hilo.
Wakati huo huo, Afisa Mtendaji wa kijiji hicho, Bw. Sospiter Ngarongwa ambaye pia analalamikiwa katika ubadhirifu wa fedha hizo, alisema kuwa yeye ana jukumu moja tu la kukusanya fedha na kuziwakilisha kwa wakubwa wake, ambao hakuwataja.
Alipoendelea kuhojiwa, Afisa Mtendaji huyo alishindwa kuonyesha ushirikiano na kuwatupia lawama Mwenyekiti wa Kijiji na Kamati ya Maendeleo ya Kijiji.
Naye Katibu wa CCM tawi la Iringa Mvumi, Bw. Amos Kwanga alisema, ukweli unaonyesha wazi kuwa, viongozi hao wa kata wanahusika na ubadhirifu wa fedha zinazochangwa na wananchi.
Aliwatuhumu viongozi hao kuishi kama miungu watu, huku hawataki kusikiliza malalamiko ya wananchi, na wale wanaonekana kuwafuatilia, huwabambikizia kesi ambazo huishia kwenye ofisi za mtendaji wa kata.
Wananchi hao wamemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw. William Lukuvi kwenda kijijini hapo kuzungumza nao au kuunda kamati ya kuchunguza suala hilo.
``Hatutakubali fedha zetu zipotee huku watoto wetu wakisomea katika jengo ambalo halina madirisha wakati fedha tumechanga, hatutakubali hata kidogo, kama hatua za makusudi hazitachukuliwa, sisi tutajua la kufanya,`` walisema.
SOURCE: Nipashe