Wananchi walio wengi weshagundua kuwa wabunge wengi wa CCM ni wanafiki wakubwa

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,477
30,130
Bunge ni miongoni ya mihimili mikuu 3 ya nchi ambapo mingine ni Mahakama na Serikali.

Kazi kubwa ya mihimili hiyo katika nchi yoyote inayoendesha utawala bora ni kile kitu kinachoitwa power separation katika maana ya check and balance.

Kwa utaratibu wa kawaida ni kuwa kila mhimili una majukumu yake ya msingi ya kiutendaji na haipaswi mhimili mmoja kuingilia utendaji kazi wa mhimili mwingine au mhimili mmojawapo kati ya hiyo kujiona upo juu ya mihimili mingine.

Katika post yangu nitajitahidi kuelezea majukumu makuu ya mhimili wa Bunge ambayo ni kutunga sheria zenye manufaa mapana kwa nchi, kuwasimamia wananchi wanaowawakilisha katika kuwasemea matatizo yao yanayowakabili na pia jukumu lake jingine kubwa ni kuisimamia serikali na kuhakikisha kuwa kwa yale mambo mabaya yanayofanywa na serikali kuyakemea kwa nguvu zao zote.

Sasa hebu tuangalie utendaji kazi wa Bunge letu ambalo wabunge wake walio wengi ni wabunge wa Chama tawala cha CCM.

Bunge letu limegawanyika katika makundi mawili ambayo ni wabunge wa CCM na wabunge wa vyama vya upinzani.

Kwa upande wa wabunge wa upinzani wamekuwa wakitekeleza majukumu yao kama ambavyo wanavyohitajika kufanya, ambapo ni kuisimamia serikali na kuyapigania matatizo yanayowakabili wananchi wanaowawakilisha.

Hali ni tofauti kwa upande wa wabunge wa CCM, ambao wao huwa wanaamini kuwa jukumu lao kubwa ni 'kuikingia' kifua serikali iliyoko madarakani kwa maovu inayoyafanya!

Tumeshuhudia mara nyingi wabunge wa upinzani wakitoa hoja za msingi kabisa za kuikosoa serikali kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi, lakini wakaishia kuzomewa na wakati mwingine kukashifiwa na kuitwa wazushi na hadi wakati mwingine wabunge hao wa CCM wakatumia vibaya wingi wao humo bungeni kwa kufanya maamuzi ya kuwatimua kuhudhuria vikao vingi vya Bunge hata kinyume cha kanuni za Bunge lao kwa lengo moja tu la kuwakomoa wabunge wa upinzani!

Baada ya kuibuka sakata hili la wizi wa makinikia kwenye migodi yetu ya dhahabu lililosimamiwa kikamilifu na Rais John Pombe Magufuli ambaye anatoka chama tawala cha CCM, ndipo wananchi tumethibitisha pasipo mashaka yoyote kuhusu unafiki wa hali ya juu wa wabunge wa CCM!

Hoja hiyo ya wizi wa rasilimali zetu kutokana na sheria mbovu za uwekezaji ambazo zimekuwa zikawependelea zaidi wawekezaji wa kigeni na kutonufaisha wananchi wa nchi hii ambako rasilimali hizo zipo na pia sheria hizo mbovu za madini zimekuwa zikipitishwa kishabiki na wabunge hao hao wa CCM kwa kura nyingi za NDIYOOO..........

Kwa upande wa wabunge wa upinzani wamekuwa wakipigia kelele kwa nguvu zao zote kwa miaka takribani 20 iliyopita na wamekuwa wakionyesha uzalendo wa hali ya juu lakini kwa bahati mbaya sana wamekuwa wakipuuzwa na wabunge wa CCM, na kuwakejeli wabunge hao wa upinzani na kuwaita wazushi na hadi wakati mwingine baadhi ya wabunge hao wa upinzani wamekuwa wakifukuzwa Bungeni kwa 'kosa' la kusimamia haki za wananchi.

Ipo mifano hai ya wabunge wa upinzani ambapo 'walionewa' na kufungiwa kuhudhuria vikao vya Bunge kutokana na wabunge hao kuonyesha uzalendo wa hali ya juu na kuisimamia maslahi mapana ya Taifa letu.

Mifano michache ni kama vile Mbunge Zito Kabwe alipotimuliwa bungeni mwaka 2007 kwa kuibua ufisadi mkubwa wa mkataba wa uchimbaji wa dhahabu wa mgodi wa Buzwagi uliosainiwa jijini London na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo Nazir Karamagi, ambapo 'uozo' huo umethibitishwa na tume ya pili ya Rais iliyosomwa hivi karibuni.

Cha kushangaza kupita kiasi ni kwa wabunge hao hao wa CCM ambao miaka 10 iliyopita walimpuuza Zito Kabwe hadi kumwangushia 'rungu' la kumfungia kuhudhuria vikao vingi vya Bunge kwa kuibua sakata hilo la Buzwagi ndiyo hao hao hivi leo wanamshangilia Rais Magufuli na kumuita shujaa na mzalendo kwa kulinda rasilimali zetu!

Kutokana na unafiki huo wa hali ya juu wanaoendelea kuuonyesha wabunge wa CCM ambao ndiyo umesababisha hata kukwama nchi yetu kupata Katiba mpya, dawa yao ni moja tu kuwapiga chini wabunge wote wa CCM kwenye majimbo yao yote kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020 ili kutoa fundisho kwa wabunge wa CCM kuwa unafiki wao kwa wananchi wao zawadi yao ni moja tu ya kuwapiga chini kwa kishindo kikubwa!
 
Watanzania wengi ni ngumu kwao kukumbuka kurasa za nyuma za historia ya nchi hii na ndipo CCM uchukulia point
 
Aaah sawa kama unaamini ni kweli subiri uchaguzi utaona mwenyewe. Ww c unatetea chama fln
Na wewe si unatetea chama chako cha kijani?

Hebu kuwa mkweli toka ndani ya nafsi yako bila kuegemea itikadi za kisiasa, baada ya kuibuka hili sakata la makinikia, hivi ni wabunge wepi ni wazalendo wa kweli ni wa CCM au ni wa upinzani?

Hivi kama kweli wabunge wa CCM wangekuwa na uzalendo kama unavyotaka kutuaminisha, wangeweza kweli kutuingiza 'mkenge' na kupitisha hiyo miswada ya sheria ambayo imelisababishia Taifa kuibiwa matrilioni ya pesa ambayo kama utaamua kuwagawia watanzania, kila mtu angeweza kwenda Show room na kuondoka na Noah yake!?
 
Tena unashangaa mtu anasimama ametoa jicho akiwaponda wapinzani ati ni wanafiki wezi nk... Sasa unajiuliza wabunge kazi yao pale bungeni cjui hawaifaham km wao ndo watunga miswaada huo uozo ungepatikana wap na si wote ila asilimia kubwa ni wazee wa ndioo
 
Nchi yetu hasara tupu,sio kwa rais,sio kwa wabunge,sio kwa wakuu wa mikoa yaani mpaka mtu unajuta kuzaliwa Tanzania.

Ngoja tuone inapoelekea lakini ua kwamba unafiki upo kila mahali katika nchi yetu
Umesema kweli.....

Hebu fikiria madudu yanayofanywa na maRC mathalani wa Dar na Arusha na bado Mkulu anasema yeye hawezi kuwatumbua hao eti kwa kuwa yeye hapangiwi la kufanya na mtanzania yeyote kwa kuwa ni yeye mwenyewe ndiye aliyeenda kuchukua fomu ya kugombea Urais kule Dom na hakushauriwa na mtu yeyote......

Hebu tusubiri mwaka 2020 tuone kama kura yake moja na ya mama Jesca ndizo zitakazomrejesha pale Magogoni!
 
wabunge wa ccm ni wabunge wa chama na wabunge wa serikali iliyopo madarakani. kazi yao kubwa ni kuisifu serikali na kuipongeza. ukichagua mbunge wa ccm umechagua mzigo.
 
wabunge wa ccm ni wabunge wa chama na wabunge wa serikali iliyopo madarakani. kazi yao kubwa ni kuisifu serikali na kuipongeza. ukichagua mbunge wa ccm umechagua mzigo.
Ndiyo maana katika suala la makinikia, miaka ya nyuma kwenye awamu ya 3 na 4 waliwaona wabunge wa upinzani wachochezi.

Lakini awamu hii ya 5 baada ya Mwenyekiti wao wa CCM Taifa kutamka yale yale ambayo yalikuwa yakitamkwa na wabunge wa upinzani kwa kipindi cha miaka 20 mfululizo na wabunge wenzao wa CCM kuwaita wazushi na wachochezi, eti hivi sasa wamebadilisha gia angani na wanamuita Magufuli mzalendo na shujaa!
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom