Wananchi walio wengi weshagundua kuwa wabunge wengi wa CCM ni wanafiki wakubwa

It is true.....

twaweza:ccm inaungwa mkono zaidi na vilaza
sikushangai
Yale majibu ya twaweza yametoa picha kamili ya CCM.......

Kuwa wanaungwa mkono zaidi na wazee wanaozidi miaka 50, wananchi walioko vijijini na wananchi ambao hawajaenda shule!

Kumbe ndiyo maana na wao wakaridhia kuwa qualification pekee ya kuwa Mbunge hapa TZ ni only kujua kusoma na kuandika!

Nadhani hiyo utaikuta TZ pekee ambako dereva wa Mheshimiwa anatakiwa kuwa na HIGHER qualification ya minimum requirement kuwa form four leaver, wakati bosi wake Mbunge hata kama kaishia darasa la 4 siyo issue, ilimradi tu ajue kusoma na kuandika!
 
Wabunge wa CCM ni chama kwanza uzalendo baadae ndiyo sababu wanafundwa kabla ya vikao vya bunge kuanza
Inapaswa iwe vice versa,Taifa kwanza na Chama baadaye, kama wanataka kuwa wazalendo wa kweli
 
Zaidi ya 75% ya watanzania wote wamefunguka .
It is true.

Kama kweli hao wabunge wa CCM watataka kutuaminisha kuwa ni wazalendo wa kweli, tunahitaji kwanza waturejeshee Bunge Live, kwa kuwa hayo ndiyo matakwa ya wananchi zaidi ya asilimia 95.

Tunajua wasiotaka Bunge live ni watu wachache sana ambao ni viongozi wa ngazi ya juu kabisa ndani ya serikali ya awamu ya 5.
 
Bunge ni miongoni ya mihimili mikuu 3 ya nchi ambapo mingine ni Mahakama na Serikali.

Kazi kubwa ya mihimili hiyo katika nchi yoyote inayoendesha utawala bora ni kile kitu kinachoitwa power separation katika maana ya check and balance.

Kwa utaratibu wa kawaida ni kuwa kila mhimili una majukumu yake ya msingi ya kiutendaji na haipaswi mhimili mmoja kuingilia utendaji kazi wa mhimili mwingine au mhimili mmojawapo kati ya hiyo kujiona upo juu ya mihimili mingine.

Katika post yangu nitajitahidi kuelezea majukumu makuu ya mhimili wa Bunge ambayo ni kutunga sheria zenye manufaa mapana kwa nchi, kuwasimamia wananchi wanaowawakilisha katika kuwasemea matatizo yao yanayowakabili na pia jukumu lake jingine kubwa ni kuisimamia serikali na kuhakikisha kuwa kwa yale mambo mabaya yanayofanywa na serikali kuyakemea kwa nguvu zao zote.

Sasa hebu tuangalie utendaji kazi wa Bunge letu ambalo wabunge wake walio wengi ni wabunge wa Chama tawala cha CCM.

Bunge letu limegawanyika katika makundi mawili ambayo ni wabunge wa CCM na wabunge wa vyama vya upinzani.

Kwa upande wa wabunge wa upinzani wamekuwa wakitekeleza majukumu yao kama ambavyo wanavyohitajika kufanya, ambapo ni kuisimamia serikali na kuyapigania matatizo yanayowakabili wananchi wanaowawakilisha.

Hali ni tofauti kwa upande wa wabunge wa CCM, ambao wao huwa wanaamini kuwa jukumu lao kubwa ni 'kuikingia' kifua serikali iliyoko madarakani kwa maovu inayoyafanya!

Tumeshuhudia mara nyingi wabunge wa upinzani wakitoa hoja za msingi kabisa za kuikosoa serikali kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi, lakini wakaishia kuzomewa na wakati mwingine kukashifiwa na kuitwa wazushi na hadi wakati mwingine wabunge hao wa CCM wakatumia vibaya wingi wao humo bungeni kwa kufanya maamuzi ya kuwatimua kuhudhuria vikao vingi vya Bunge hata kinyume cha kanuni za Bunge lao kwa lengo moja tu la kuwakomoa wabunge wa upinzani!

Baada ya kuibuka sakata hili la wizi wa makinikia kwenye migodi yetu ya dhahabu lililosimamiwa kikamilifu na Rais John Pombe Magufuli ambaye anatoka chama tawala cha CCM, ndipo wananchi tumethibitisha pasipo mashaka yoyote kuhusu unafiki wa hali ya juu wa wabunge wa CCM!

Hoja hiyo ya wizi wa rasilimali zetu kutokana na sheria mbovu za uwekezaji ambazo zimekuwa zikawependelea zaidi wawekezaji wa kigeni na kutonufaisha wananchi wa nchi hii ambako rasilimali hizo zipo na pia sheria hizo mbovu za madini zimekuwa zikipitishwa kishabiki na wabunge hao hao wa CCM kwa kura nyingi za NDIYOOO..........

Kwa upande wa wabunge wa upinzani wamekuwa wakipigia kelele kwa nguvu zao zote kwa miaka takribani 20 iliyopita na wamekuwa wakionyesha uzalendo wa hali ya juu lakini kwa bahati mbaya sana wamekuwa wakipuuzwa na wabunge wa CCM, na kuwakejeli wabunge hao wa upinzani na kuwaita wazushi na hadi wakati mwingine baadhi ya wabunge hao wa upinzani wamekuwa wakifukuzwa Bungeni kwa 'kosa' la kusimamia haki za wananchi.

Ipo mifano hai ya wabunge wa upinzani ambapo 'walionewa' na kufungiwa kuhudhuria vikao vya Bunge kutokana na wabunge hao kuonyesha uzalendo wa hali ya juu na kuisimamia maslahi mapana ya Taifa letu.

Mifano michache ni kama vile Mbunge Zito Kabwe alipotimuliwa bungeni mwaka 2007 kwa kuibua ufisadi mkubwa wa mkataba wa uchimbaji wa dhahabu wa mgodi wa Buzwagi uliosainiwa jijini London na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo Nazir Karamagi, ambapo 'uozo' huo umethibitishwa na tume ya pili ya Rais iliyosomwa hivi karibuni.

Cha kushangaza kupita kiasi ni kwa wabunge hao hao wa CCM ambao miaka 10 iliyopita walimpuuza Zito Kabwe hadi kumwangushia 'rungu' la kumfungia kuhudhuria vikao vingi vya Bunge kwa kuibua sakata hilo la Buzwagi ndiyo hao hao hivi leo wanamshangilia Rais Magufuli na kumuita shujaa na mzalendo kwa kulinda rasilimali zetu!

Kutokana na unafiki huo wa hali ya juu wanaoendelea kuuonyesha wabunge wa CCM ambao ndiyo umesababisha hata kukwama nchi yetu kupata Katiba mpya, dawa yao ni moja tu kuwapiga chini wabunge wote wa CCM kwenye majimbo yao yote kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020 ili kutoa fundisho kwa wabunge wa CCM kuwa unafiki wao kwa wananchi wao zawadi yao ni moja tu ya kuwapiga chini kwa kishindo kikubwa!
nchii hii mkuu ukiifikiria unapatwa na hasira sana unatamani yale mabunge dom ukuyachomoe yote unayatandika viboko vya nguvu yapunguze neno hili la '''ndiyoooooooo’’’’
 
Tatizo mkuu Mystery watanzania ni wasahaulifu sana kuna madudu mengi yamepitishwa hapo bungeni.Fikiria fao la kujitoa kwenye mifuko ya jamii mpaka ufike miaka 55 wakati life span ya mtz ni 45-55 na kazi zenyewe ni temporary contracts,ikapitishwa tu kiaina aina.ukufuatilia kiukweli ni sheria nyingi zimepitishwa kiushabiki na kiitikadi pasi na weledi na inaonesha wabunge wengi ni michosho tu.THIS COUNTRY BWANA IS VERY POOR!
Naunga mkono hoja!
 
Tatizo mkuu Mystery watanzania ni wasahaulifu sana kuna madudu mengi yamepitishwa hapo bungeni.Fikiria fao la kujitoa kwenye mifuko ya jamii mpaka ufike miaka 55 wakati life span ya mtz ni 45-55 na kazi zenyewe ni temporary contracts,ikapitishwa tu kiaina aina.ukufuatilia kiukweli ni sheria nyingi zimepitishwa kiushabiki na kiitikadi pasi na weledi na inaonesha wabunge wengi ni michosho tu.THIS COUNTRY BWANA IS VERY POOR!
Naunga mkono hoja!
It is true.

Miongoni ya miswada ya hovyo kabisa iliyopitishwa na hawa jamaa zetu wa Ndiyooooo...ni hiyo sheria ya kuondoa FAO la kujitoa.

How comes wabunge wawapangie wananchi wakati wa kwenda kuchukua pesa yao waliyojiwekea kwenye mifuko ya Hifadhi ya Jamii?

Mbona wao wabunge kila wanapomaliza muda wa kulitumikia bunge kila baada ya miaka 5 wanachukua mafao yao bila kujali kama mbunge amefikisha miaka 55 au bado?

Yaani watanzania wengi bado hawajarealize tu kuwa adui mkubwa no. 1 hapa nchini anayesababisha nchi yetu ipige mark time na isiwe na maendeleo miaka yote ni CCM.

Sawa ni moja tu iliyobaki ni ifikapo 2020 kuwapiga chini wabunge wote wa CCM huko majimboni kwao na hapo ndipo watanzania tutakapoanza kuyaona maendeleo ya kweli ya nchi yetu.
 
Ifike muda enough iwe enough cause tumekuwa wajinga kwa muda mreefu mpaka mungu katusaidia kumfanya yule mzee amrudie mungu na kumpa nguvu ya kuspeculate hiyo mikataba japo atapigwa vita
 
Ifike muda enough iwe enough cause tumekuwa wajinga kwa muda mreefu mpaka mungu katusaidia kumfanya yule mzee amrudie mungu na kumpa nguvu ya kuspeculate hiyo mikataba japo atapigwa vita na manyumbu wengi tu.
It is true, ingawa wanaccm wengi 'wanaigiza' kuwa wanamuunga mkono kwa asilimia 100 Mwenyekiti wao wa CCM Rais Magufuli, lakini in reality mioyoni mwao wanampinga vikali mno.

Hivi unadhani watu kama akina Chenge, Karamagi, Ngeleja na wengineo waliotajwa na Tume ya Profesa Ossoro watakuwa wanafurahia haya matukio ya 'kuvuliwa' kwao nguo hadharani?
 
Twaweza washa sema vilaza wote wanapatikana ccm
Ndiyo maana na wao wabunge nao wakaifanya nafasi ya Uheshimiwa Ubunge ni ya ukila....za kwa kuweka minimum requirement ya mtu kuwa Mheshimiwa mbunge hapa nchini qualification yake ni only kujua kusoma na kuandika!
 
Back
Top Bottom