Wananchi wakataa agizo la mbunge Kafulila kuhusu maabara

mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,913
916
TBC habari,
wakazi wa jimbo la kigoma kusini ambalo linaongozwa na kafulila wamekataa kufuata agizo la mbunge wao kwamba wasishiriki katika ujenzi wa maabara badala yake wamejitokeza kwa wingi katika ujenzi wa maabara hizo.

Akizungumza kwa niaba ya watu wake mwenyekiti wa halmashauri wa eneo hilo ambaye pia ni kutoka chama cha kafulila alibainisha kuwa hawako tayari kufuata amri ya mbunge ikiwemo kugomea kushiriki ujenzi wa maabara pamoja na kutochangia shilingi 2000 kila kaya ukiwa ni mchango wa wananchi kwenye maabara,

mwenyekiti alisema kuwa mbunge anaposema tusichangie shilingi elfu mbili anambadala gani,je analeta hizo pesa au anafanya jitihada gani ili maabara zijengwe tumegundua kuwa hakuna anachofanya sisi tumeamua kusonga mbele bora tutofautiane katika hili ili maabara zijengwe alisema mwenyekiti.

jitihada hizo pia zilichagizwa na mhandisi wa wilaya hiyo baada ya kuamua kushiriki na wananchi katika ujenzi huo pamoja na watumishi wengine wa wilaya hiyo.
 
Mkuu siku hizi wananchi wanatazama mbele zaid hata ukiwashawishi kwa baya hawatakubali. Kumbuka msemo usemao "akili za kuambiwa,changanya na zako"
 
Kweli wakuu kafulila anatafuta pakutokea huwezi kuhimiza watu wasishiriki maendeleo kama kweli unayo nia ya dhati ya kuendeleza jamii yako,kafulila anafanya siasa za kitoto kabisa.
 
Hakika mkuu jamii imeelimika sana kwa upeo huu tunakwenda vizuri sana katika kuleta maendeleo.
 
Kweli kabisa Mkuu, hata huku Arusha hata vijana wamehamasika sana, ile hela ya kununua mirungi sasa wanachangia maabara!
 
TBC habari,
wakazi wa jimbo la kigoma kusini ambalo linaongozwa na kafulila wamekataa kufuata agizo la mbunge wao kwamba wasishiriki katika ujenzi wa maabara badala yake wamejitokeza kwa wingi katika ujenzi wa maabara hizo.

Akizungumza kwa niaba ya watu wake mwenyekiti wa halmashauri wa eneo hilo ambaye pia ni kutoka chama cha kafulila alibainisha kuwa hawako tayari kufuata amri ya mbunge ikiwemo kugomea kushiriki ujenzi wa maabara pamoja na kutochangia shilingi 2000 kila kaya ukiwa ni mchango wa wananchi kwenye maabara,

mwenyekiti alisema kuwa mbunge anaposema tusichangie shilingi elfu mbili anambadala gani,je analeta hizo pesa au anafanya jitihada gani ili maabara zijengwe tumegundua kuwa hakuna anachofanya sisi tumeamua kusonga mbele bora tutofautiane katika hili ili maabara zijengwe alisema mwenyekiti.

jitihada hizo pia zilichagizwa na mhandisi wa wilaya hiyo baada ya kuamua kushiriki na wananchi katika ujenzi huo pamoja na watumishi wengine wa wilaya hiyo.

Ala...TBC! Ze commedy tv...
 
Hakika mkuu jamii imeelimika sana kwa upeo huu tunakwenda vizuri sana katika kuleta maendeleo.

elimu gani unayowaifia nayo? mnatumia udhaifu wao kwa kuwakamua zaidi? ccm inapiga hela halafu inasifiasifia iliowaibia! mimi siwezi kuibiwa eti nachangia.
 
Kweli kabisa Mkuu, hata huku Arusha hata vijana wamehamasika sana, ile hela ya kununua mirungi sasa wanachangia maabara!

Wacha kuongopea umma wa Jf, Arusha kila Mwana ccm akipita na Matembele aka Nguo za Kijani wananchi wanalia Waturudishie Hela Zetu
 
Mbona mimi nikipita huwa sisikii muhuni yeyote akiongea? Natamani siku moja nipite mtu afungue mdomo ili nimfundishe adabu!
 
Kweli wakuu kafulila anatafuta pakutokea huwezi kuhimiza watu wasishiriki maendeleo kama kweli unayo nia ya dhati ya kuendeleza jamii yako,kafulila anafanya siasa za kitoto kabisa.

Kwa wanaojitambua wanaelewa kafulila anamaanisha nini,wenzangu tuendelee kuropoka tuu
 
Mbona mimi nikipita huwa sisikii muhuni yeyote akiongea? Natamani siku moja nipite mtu afungue mdomo ili nimfundishe adabu!

unapita Arusha ipi acha kuongopea UMMA WAKATI uko Dar LUMUMBA unakandamiza key board upate buku saba
 
Mbona mimi nikipita huwa sisikii muhuni yeyote akiongea? Natamani siku moja nipite mtu afungue mdomo ili nimfundishe adabu!

Karibu kesho asubuhi kipenzi cha Juliana Sonza usiishie kuandika toka LUMUMBA DAR
 
Back
Top Bottom