Wananchi waikwepa kamati ya shule, wachangia matokeo mabovu kwa wanafunzi

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Inaelezwa kuwa kiwango cha ushiriki wa wananchi katika shughuli za jamii hasa za kiutawala nchini Tanzania kiko chini na bado kinashuka, jambo ambalo linaathiri utolewaji wa maamuzi yanayohusu maendeleo ya taifa.

Sekta ya elimu kwa muda mrefu imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali za ubora wa elimu inayotolewa na mazingira yasiyoridhisha wanayosomea wanafunzi. Changamoto hizo kwa kiasi kikubwa zinasababishwa na ushiriki duni wa wananchi katika maendeleo ya shule.

Ripoti ya Shirika la HakiElimu (2017) inaeleza kuwa kiwango cha ushiriki wa wananchi katika sekta mbalimbali za utawala nchini Tanzania, hasa kwa wanawake, kiko chini sana na bado kinashuka.

“ Kwa mfano, ushiriki wa wananchi katika vikao vya kamati za shule ulipungua kutoka asilimia 36 mwaka 2006 hadi kufikia asilimia 15 mwaka 2013, hii ni sawa asilimia 13 ya kushuka kwa ushiriki wa wananchi kwenye huduma hii muhimu ya umma”, inaeleza ripoti hiyo.

Kamati za shule ni sehemu muhimu ambapo wananchi wanajadili changamoto za shule zilizopo katika eneo husika uhakikisha kunakuwa na matumizi mazuri ya rasilimali fedha zinazoelekezwa katika kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia katika shule.

Zaidi, soma hapa => Wananchi waikwepa kamati za shule, maamuzi na mipango ya elimu yatekelezwa na wachache | FikraPevu
 
Back
Top Bottom