Dr. Wansegamila
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 2,856
- 7,846
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Geita wamepiga kambi katika pori llililopo Kitongoji cha Iseni Kijiji cha Kasala Kata ya Makurugusi Wilaya ya Chato Mkoani humo baada ya kudaiwa kuwepo kwa nyoka aina ya chatu mwenye maajabu huku wengine wakionekana kuchota Baraka kutoka kwa nyoka huyo kwa kufanya matambiko.
======
UPDATES;
Chatu Aliyeonekana Chato Achukuliwa
September 11, 2019
NYOKA mkubwa aina ya chatu ambaye hivi karibuni alizua gumzo baada ya kuonekana Kitongoji cha Iseni, Kijiji cha Kijiji cha Kasala Kata ya Makurugusi wilayani Chato Mkoani Geita amechukuliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (Tawa) na kumpeleka pori la akiba la Kigosi Mulowosi, lililopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Richard Bagolele amesema nyoka huyo anapelekwa pori la akiba la Kigosi kwa ajili ya kuhifadhiwa.
Nyoka huyo aliyeanza kuonekana siku saba zilizopita aligeuka kivutio kwa wananchi waliodai kuwa ni baraka, wengi kushinda porini wakimtazama huku wakiwa na mbuzi, maji na unga na vyakula wakiamini endapo nyoka atakula watapata baraka ya mvua, kuongezeka kwa mavuno na kuondoa mikosi kijijini hapo hivyo kuwaletea mafanikio.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel amewataka wanakijiji wa kijiji cha Makurugusi waliokuwa wamepiga kambi porini wakisubiri maajabu ya nyoka huyo, wafanye kazi kwa bidii na kuachana na imani potofu za kupata baraka kwa matambiko na kuabudu nyoka na vitu vingine.
Na Edwin Lindege