Wananchi wafurika Kijiji cha Kasala Kata ya Makurugusi Wilaya ya Chato kumuona Nyoka wa ajabu

Dr. Wansegamila

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Messages
1,699
Points
2,000
Dr. Wansegamila

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2012
1,699 2,000
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Geita wamepiga kambi katika pori llililopo Kitongoji cha Iseni Kijiji cha Kasala Kata ya Makurugusi Wilaya ya Chato Mkoani humo baada ya kudaiwa kuwepo kwa nyoka aina ya chatu mwenye maajabu huku wengine wakionekana kuchota Baraka kutoka kwa nyoka huyo kwa kufanya matambiko.


======

UPDATES;

Chatu Aliyeonekana Chato Achukuliwa

September 11, 2019

NYOKA mkubwa aina ya chatu ambaye hivi karibuni alizua gumzo baada ya kuonekana Kitongoji cha Iseni, Kijiji cha Kijiji cha Kasala Kata ya Makurugusi wilayani Chato Mkoani Geita amechukuliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (Tawa) na kumpeleka pori la akiba la Kigosi Mulowosi, lililopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
1568374243165-png.1206341

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato, Richard Bagolele amesema nyoka huyo anapelekwa pori la akiba la Kigosi kwa ajili ya kuhifadhiwa.

Nyoka huyo aliyeanza kuonekana siku saba zilizopita aligeuka kivutio kwa wananchi waliodai kuwa ni baraka, wengi kushinda porini wakimtazama huku wakiwa na mbuzi, maji na unga na vyakula wakiamini endapo nyoka atakula watapata baraka ya mvua, kuongezeka kwa mavuno na kuondoa mikosi kijijini hapo hivyo kuwaletea mafanikio.
1568374272447-png.1206342

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel amewataka wanakijiji wa kijiji cha Makurugusi waliokuwa wamepiga kambi porini wakisubiri maajabu ya nyoka huyo, wafanye kazi kwa bidii na kuachana na imani potofu za kupata baraka kwa matambiko na kuabudu nyoka na vitu vingine.

Na Edwin Lindege
 
The Monk

The Monk

Platinum Member
Joined
Oct 12, 2012
Messages
13,147
Points
2,000
The Monk

The Monk

Platinum Member
Joined Oct 12, 2012
13,147 2,000
Nimeona mzee mmoja hapo kajipiga shuka jekundu, alivyotoa simu ndio kujua kumbe ni baharia Mshana Jr

Mganga na smartphone wapi na wapi? Nikajiridhisha pasi shaka kwamba ni mwanakilinge mwenzetu wa JF
 
A

Amonni

Member
Joined
Jul 29, 2015
Messages
11
Points
45
A

Amonni

Member
Joined Jul 29, 2015
11 45
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Geita wamepiga kambi katika poli llililopo Kitongoji cha Iseni Kijiji cha Kasala Kata ya Makurugusi Wilaya ya Chato Mkoani humo baada ya kudaiwa kuwepo kwa nyoka aina ya chatu mwenye maajabu huku wengine wakionekana kuchota Baraka kutoka kwa nyoka huyo kwa kufanya matambiko.


Duh yaani tuna kazi kubwa kufikia ustarabu!
 
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Messages
18,360
Points
2,000
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2015
18,360 2,000
Watu wa kanda hiyo wana imani za kijinga sana, mpaka wasomi hawana tofauti na wasiosoma
Katiba imetoa uhuru wa kuabudu chochotee.Waziri lugora hao wanaosali hapo hiyo dini umeisajili ?maana wewe siku hizi umegeuka msajili wa dini na miungu wakati serikali haina dini.Yule nabii uliyemkamata kisa kanisa lake anaposalia halijasajiliwa mwachie.Kazi ya wizara Ni kusajili NGO Sio dini.Ziko NGo zenye Mashule ,mahospitali nk hizo ndizo usajili Sio dini.Ona Sasa hao wanaabudu nyoka wao nenda kawakamate kwa kuabudu bila kusajiliwa wizara ya Mambo ya ndani.Haya hao waabuduo wa chato kawakamate Kama ulivyokamata nabii wetu kuwa anasalisha bila kanisa lake kusajiliwa.Nilikuambia kukamata nabii SI kitu Cha mchezo .Kawakamate na hao.Huyo mzee padri wao mkamate Kama ulivyomkamata nabii wetu
 
FaizaFoxy

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2011
Messages
65,988
Points
2,000
FaizaFoxy

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2011
65,988 2,000
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Geita wamepiga kambi katika pori llililopo Kitongoji cha Iseni Kijiji cha Kasala Kata ya Makurugusi Wilaya ya Chato Mkoani humo baada ya kudaiwa kuwepo kwa nyoka aina ya chatu mwenye maajabu huku wengine wakionekana kuchota Baraka kutoka kwa nyoka huyo kwa kufanya matambiko.
View attachment 1203478
Wajinga ndiyo waliwao.
 
Mkokaa

Mkokaa

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2019
Messages
637
Points
1,000
Mkokaa

Mkokaa

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2019
637 1,000
Katika hali isiyokuwa ya kawaida wananchi kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Geita wamepiga kambi katika pori llililopo Kitongoji cha Iseni Kijiji cha Kasala Kata ya Makurugusi Wilaya ya Chato Mkoani humo baada ya kudaiwa kuwepo kwa nyoka aina ya chatu mwenye maajabu huku wengine wakionekana kuchota Baraka kutoka kwa nyoka huyo kwa kufanya matambiko.
View attachment 1203478

Aisee kuna watu wana lafudhi mbaya
 

Forum statistics

Threads 1,336,651
Members 512,670
Posts 32,546,692
Top