Wananchi wafurahishwa na serikali ya wanyonge inavyoshughulikia sakata la sukari walaumu mabeberu

nzagambadume

JF-Expert Member
Apr 9, 2018
2,430
5,769
Ni maoni ya wananchi wanyonge sehemu mbalimbali nchini wanaofurahishwa na jinsi wakuu wa wilaya na mikoa wanavyoonekana kwenye TV wakifoka kwa hasira huku wameambatana na askari polisi wenye silaha kuwakamata vibaraka wa mabeberu wanaouza sukari kwa shillingi 4000 hadi 7000(Chanika) kwa kilo ili kuichonganisha serikali na wananchi

Ikumbukwe kwamba wakati Rais Magufuli anaingia madarakani bei ya sukari ilikuwa 5000 wa kilo na nauli ya ndege toka dsm-mwanza ilikuwa sh 800,000 najua kuna watakaobisha lakini haya maneno yalitoka kinywani mwa Rais wetu mpendwa kabisa kipenzi cha wanyonge John Pombe Joseph Magufuli

Wanyonge wako pamoja sana na viongozi wetu waadilifu kama Makonda, Gambo na eagle 3 wa kule hai kwa jinsi wanavyoshuhulikia hili suala la sukari, wamesema hata kama ikifika 10,000 watanunua tu ili kuwakomesha mabeberu na vibaraka wao
 
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 sikuona namna nyingine ya kukoment mkuu nimeona nicheke tu ila kuna watu hawataelewa
Capture.JPG
 
:D:D:D:D:D:D:D:Dmkuu utaniharibu mbavu, nife kwa changamoto ya upumuaji, aisee! Juyisi yenyewe zimekuja box 3...

Everyday is Saturday......................:cool:
 
Back
Top Bottom