Areus
JF-Expert Member
- Jul 27, 2016
- 324
- 403
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Wananchi waelewe kuwa kujengewa miundombinu,kupewa huduma za jamii sio hisani ya serikali ila Ni wajibu wa serikali yoyote ile duniani. Hilo tuliweke sawa.
Pesa zote zinazopelekwa kwenye shughuli za miradi ya Maendeleo ni kodi za wananchi wenyewe wala hazitoki mfukoni mwa mzalendo yeyote. Kwahyo serikali yoyote haina haki ya kuwabagua watu kwa misingi ya vyama vyao kwamba sehemu fulani kuna wananchi wa upinzani na hawezi kupelekewa maendeleo.zana hii ni mbovu na sio nzuri kutumia kwenye kampeni. Ni harufu mbaya ya kuligawa Taifa.
Kwahyo ni vema wanasiasa wakaeleza watawafanyia nini wanachi ila sio kuwatisha.
MAENDELEO HAYANA VYAMA