Wananchi wachangie kwa hiyari

Petro E. Mselewa

Verified Member
Dec 27, 2012
9,473
2,000
Jambo la maendeleo ni jambo ambalo kila mtanzania analilenga. Kuanzia viongozi hadi wananchi wa kawaida analenga na kutamani kupata maendeleo. Yaweza kuwa maendeleo ya kiuchumi,kijamii,kiutamaduni na kisiasa. Katika kuyaleta maendeleo hayo, Serikali na wananchi kila mmoja ana wajibu wa kutimiza. Wajibu mkuu wa wananchi ni kulipa kodi. Yaweza kuwa kodi ya ongezeko ya thamani (VAT) au nyingineyo. Kikubwa ni kila mwananchi kulipa kodi impasayo kulipa.

Wajibu wa Serikali katika kuelekea maendeleo hayo ni kukusanya kodi, kupanga mipango ya kimaendeleo na kuitekeleza. Kutekeleza kunaweza kuambatana na ujenzi wa majengo ya miundombuinu mbalimbali. Yawezekana kabisa,Serikali kapungukiwa kipato au kuwa na miradi mingi ya kuitekeleza kwa wakati mmoja na hivyo kuhitaji uchangiaji wa wananchi.

Katika hili na katika mazingira hayo, wananchi wanapaswa kushawishwa. Waelezwe kwa mifano na vitendo jinsi watakavyonufaika na miradi inayohitaji uchangiaji wao. Kwa mfano,ujenzi wa Shule au Maabara utaimarisha ubora wa elimu ya watoto wa nchi hii kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla. Ujenzi wa madaraja na barabara utarahisisha usafirishaji wa watu na mizigo toka sehemu moja hadi nyingine. Kuimarika kwa elimu na kurahisishwa kwa usafirishaji ndiyo maendeleo yenyewe. Hakutakuwa na mpinzani wa hayo kirahisirahisi katika jamii yetu ya kitanzania.

Pia washawishi wenyewe wakiserikali wawe wanaaminika. Kimsingi,watanzania wanapoteza kwa kasi imani juu ya viongozi wao hasa kaika masuala ya kifedha. Mwananchi aweza kuwa tayari kuchangia lakini akaghairi baada ya kumuona anayezikusanya. Asipoaminika mkusanyaji uchangaji utasuassua au kukwama kabisa. Ufisadi katika nchi hii unaacha kovu baya.

Wananchi wa Tanzania hawapaswi kushurutishwa katika kuchangia maendeleo. Hawapaswi kushurutishwa kisheria (ingawa hakuna sheria kama hiyo hivi sasa) au hata kwa kutumia kauli za viongozi.Washurutishwe tu kulipa kodi. Kwa michango ya kimendeleo washawishiwe na kuombwa kwa hoja.Kushurutisha ni kurejea enzi ya manamba ambayo haivutii. Wananchi wachangie kwa hiari.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom