Wananchi waandamana kushinikiza serikali kutekeleza ahadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi waandamana kushinikiza serikali kutekeleza ahadi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtumiabusara, Jun 29, 2011.

 1. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Wakazi wa vijiji vinavyozunguka mgodi wa dhahabu wa Bulyankulu (BGMCL) Wilaya ya Kahama mkoani hapa, wameandamana katika Kijiji cha Segese na kufanya uharibifu mkubwa wa barabara kuu iendayo mgodini kwa lengo la kushinikiza serikali kutekeleza ahadi iliyotolewa na vingozi wake wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana

  Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Diwani Athumani, alisema wananchi hao waliandamana mwishoni mwa wiki bila kibali na kuchimba mtaro mkubwa katika barabara ya Kakola. Alisema licha ya kuchimba na kuharibu barabara hiyo kwa nia ya kuzuia magari kwenda au kutoka katika mgodi huo, wakazi hao waliweka vizuizi vya mawe na magogo barabarani.

  Watu walishuhudia tukio hilo walidai kuwa polisi walifyatua risasi za mpira na za moto hewani na mabomu ya machozi ili kuwatawanya wanakijiji hao na kusitisha maandamano hayo.

  Inadaiwa kuwa sababu kubwa ya maandamano hayo ni kuwasilisha madai na malalamiko yao serikalini dhidi ya utekelezaji wa ahadi za viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali yake mwishoni mwa mwaka jana wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu.
  Miongoni mwa ahadi hiyo ni kuwajengea barabara ya lami, kuondoa kero ya maji na uharibifu wa mazingira unaodaiwa kufanywa na mgodi huo.
  Kamanda huyo alisema polisi wamewatia mbaroni watu 40 kwa tuhuma hizo.

  Athumani alisema kati ya hao, 31 waliachiwa baada ya kuhojiwa na wengine wanaendelea kushikiliwa na kwamba watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,494
  Trophy Points: 280
  mdogo mdogo tutafika
   
 3. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ukiona moshi unafuka ujue kunaungua,yataka moyo kuzuia nguvu ya umma.
   
 4. kibakwe

  kibakwe Senior Member

  #4
  Jun 29, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuna siku Serikali ambayo si sikivu itakuja kuelewa kilio cha wananchi ambao ndiyo wenye NCHI yao
   
Loading...