Wananchi wa Zanzibar wataka Muungano lisiwe ni suwala la Kulazimishwa irudi Tanganyika kwanza.

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Messages
858
Points
0

abdulahsaf

JF-Expert Member
Joined Aug 31, 2010
858 0
[h=1]Muungano watawala maoni (“Tanganyika haionekani, iko wapi? Itoeni kwanza Tanganyika ndipo tuzungumze masuala ya Katiba na masuala ya Muungano,” alisema Suleiman[/h]


Written by abdulwaheed // 27/11/2012 // Habari // 2 Comments


Wananchi na wakazi wa Zanzibar wameligeuza maoni ya mabadiliko ya Katiba kuwa jukwaa la kujadili mambo ya Muungano na kero zake.
Maoni mengi yanayotolewa yanahusu muundo wa Muungano kuliko masuala mengine yaliyomo katika Katiba, kama haki na wajibu wa raia, haki na wajibu wa serikali, ulinzi na usalama, madaraka ya umma, madaraka ya Rais, madaraka ya Bunge na Mahakama.
Kinachozungumzwa na walio wengi ni muundo wa Muungano, kwamba wanataka Serikali ya Tanganyika ijipambanue na iwe na mamlaka yake kamili, kisha Zanzibar nayo iwe na mamlaka kamili na baadaye ndiyo nchi mbili ziketi kuamua kuunda muungano kwa baadhi ya mambo.
Suleiman Juma Suleiman, mkazi wa Kianga alihoji ilipo Tanganyika na kwanini Watanganyika wenyewe hawaidai nchi yao.
“Tanganyika haionekani, iko wapi? Itoeni kwanza Tanganyika ndipo tuzungumze masuala ya Katiba na masuala ya Muungano,” alisema Suleiman.
Ramadhan Faki mkazi wa Kianga, alisema hivi sasa Wazanzibari wengi wanataka serikali yao iliyo huru na yenye uamuzi wa mambo yote ya ndani na ya nje, hasa kwa sababu wanaona kama viongozi wao hawawezi kutetea maslahi ya Zanzibar ndani ya Muungano.
Hassan Mohamed Abdallah mkazi wa Kianga alisema yeye anataka Serikali ya Tanganyika irudi, ndipo wazungumzie masuala ya kuimarisha muungano.
Kwa wale waliozungumzia haki za binadamu wengi wao wanaelezea unyanyasaji unaofanywa na polisi.
“Tumechoka vipigo, jambo si jambo bakora zinatembea, sasa kwani hawa askari kutoka Bara wameletwa Zanzibar kulinda wananchi au kutukomesha?” alihoji Haji Ali Haji.
Haji alisema yeye anaamini wananchi wanayo haki ya kutoa mawazo yao kuhusu serikali yao au jambo lolote linalohusu maslahi yao.
“Sisi (wananchi) tunao uhuru wa kutoa mawazo, sasa kwanini tunaposema kile tunachokitaka, tunapigwa na kunyanyaswa?” alihoji Haji.
 

Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2010
Messages
3,316
Points
2,000

Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2010
3,316 2,000
Kikwete alikosea sana kusema maswala ya muungano yasijadiliwe, wanachi wameamsha hasira zao wakitaka good governance ktk swala muungano.wengi wao wakisema wanaitwa wakorofi, nadhani jaji warioba tayari ameshapima joto la kutaka tanganyika ionekane kama nchi kamili ili kuweza kujadili whether muungano au no.JK dunia ya leo si ya kutumia mabavu baba ni demokrasia na utawala bora.Mengi tutasikia as we go along the process
 

Forum statistics

Threads 1,389,283
Members 527,879
Posts 34,022,069
Top