Wananchi wa Sierra Leone kuchagua Rais, Wabunge, Madiwani na Mameya leo

Saharavoice

Saharavoice

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2007
Messages
2,783
Points
1,500
Saharavoice

Saharavoice

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2007
2,783 1,500
Leo ni siku ya uchaguzi nchini Sierra Leone ambapo wananchi wanatarajiwa kupiga kura za urais, ubunge, udiwani pamoja na mameya wa miji. inakadiriwa kuwa vyama zaidi ya kumi vinashiriki katika uchaguzi huo, ingawa ni vyama viwili yaani All peoples' congress (APC) chama tawala, na Sierra leone peoples' party (SLPP) chama kikuu cha upinzani vinatarajiwa kuchuana vikali katika uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa katiba ya Sierra Leone, mshindi wa kiti cha urais ni lazima apate kura zaidi ya asilimia hamsini, mwelekeo unaonyesha wazi kwamba huenda uchaguzi huu ukaingia duru la pili kwani inatabiriwa kwamba hakuna mgombea wa kiti cha uraisi atakayepata zaidi ya asilimia hamsini ya kura zitakazopigwa.

Vyombo vya usafiri yaani mabasi ya abiria, taxi pamoja na pikipiki vimepigwa marufuku kuanzia saa moja asubuhi hadi saa moja jioni ikiwa ni tahadhali ya kudhibiti vurugu zinazoweza kutokea wakati wa upigaji kura, pia wananchi wameamuriwa kurejea na kutulia majumbani mara baada ya kupiga kura.

Itakumbukwa kuwa, ni miaka kumi sasa tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vimalizike nchini Sierra Leone na uchaguzi huu ni wa tatu tangu kumalizika kwa vita hivyo.

Tuwatakie wananchi wa Sierra Leone uchaguzi mwema, huru na wa haki.
 
Freetown

Freetown

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2008
Messages
887
Points
195
Freetown

Freetown

JF-Expert Member
Joined Apr 6, 2008
887 195
Leo ni siku ya uchaguzi nchini Sierra Leone ambapo wananchi wanatarajiwa kupiga kura za urais, ubunge, udiwani pamoja na mameya wa miji. inakadiriwa kuwa vyama zaidi ya kumi vinashiriki katika uchaguzi huo, ingawa ni vyama viwili yaani All peoples' congress (APC) chama tawala, na Sierra leone peoples' party (SLPP) chama kikuu cha upinzani vinatarajiwa kuchuana vikali katika uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa katiba ya Sierra Leone, mshindi wa kiti cha urais ni lazima apate kura zaidi ya asilimia hamsini, mwelekeo unaonyesha wazi kwamba huenda uchaguzi huu ukaingia duru la pili kwani inatabiriwa kwamba hakuna mgombea wa kiti cha uraisi atakayepata zaidi ya asilimia hamsini ya kura zitakazopigwa.

Vyombo vya usafiri yaani mabasi ya abiria, taxi pamoja na pikipiki vimepigwa marufuku kuanzia saa moja asubuhi hadi saa moja jioni ikiwa ni tahadhali ya kudhibiti vurugu zinazoweza kutokea wakati wa upigaji kura, pia wananchi wameamuriwa kurejea na kutulia majumbani mara baada ya kupiga kura.

Itakumbukwa kuwa, ni miaka kumi sasa tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vimalizike nchini Sierra Leone na uchaguzi huu ni wa tatu tangu kumalizika kwa vita hivyo.

Tuwatakie wananchi wa Sierra Leone uchaguzi mwema, huru na wa haki.
Nimekupata, Sahara Voice,
 
Forum statistics

Threads 1,294,754
Members 498,027
Posts 31,187,127
Top