Uchaguzi 2020 Wananchi wa Lamadi wana neno lao kwa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM ndugu Magufuli

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
SALAAM KUTOKA LAMADI KWENDA CHATO ALIKOPUMZIKA MGOMBEA WA CCM NDG. MAGUFULI.

Ndg, mgombea na Mh. Rais salaam sana. Hivi majuzi umekuwa kwenye ziara ya mikutano yako ya kampeni kwa mikoa ya kanda ya ziwa. Watu wamekusanyika kwa hiyari yao na wengine kwa kushawishiwa ili wakusikilize.

Mh. Mgombea umenukuliwa ulipokuwa Bunda na hata ulipofika masanza Busega ukisema wanainchi wasifanye ushabiki katika kuchagua, wasije wakawa kama Bunda, ambayo ilichagua upinzani na matokeo yake inazidiwa mpaka na Lamadi kamji kadogo ila kana taa za barabarani.

Ndg. Mgombea na Mh. Rais, kauli hii sisi wana Lamadi tumeipokea kwa masikitiko makubwa sana, . kwanza tumeiona ni kauli ya kichonganishi kati ya bunda na Lamadi, lkn vile vile ni kauli ya kibaguzi. Lakini tunashangaa kwamba wasaidizi wako hawakukuambia vizuri kwamba hizi taa za Lamadi zimefungwa wakati Lamadi ikiwa chini ya upinzani kbla ya diwani kuunga mkono juhudi.

Lakini pia watu wa Lamadi tunajihoji, kama hoja ya maendeleo ni CCM kuwa watawala, kwa nn hizo taa hazikufungwa
Gamboshi ambako tangu Mungu aumbe dunia mtawala ni CCM?

Lakini kitu cha pekee na cha kushangaza katika mikutano yako, unahubiri ubaguzi wazi wazi, kwamba mkichagua wa vyama vingine sitaleta maendeleo na wakati huo huo unahubiri maendeleo hayana chama!

Ndugu Mgombea na Mh. Rais, tunakuomba sana, ktk hotuba zako punguza kauli za ubaguzi, eleza Sera na usiwalazimishe watu kuchagua kiongozi unayemtaka wewe.

Asalam allaikum.
 
Sky Eclat

W/Msalaam

Kumbe Mayoo Unaishi Lamadi eee?!!!😁😁

Looh Nyinyinyinyi Jamani aiseee Mtatuua Na Maneno Yenu Jama

Nina Imani wapiga Kura wetu Milioni 17 Watatuvusha....aaamin
 
Labda amehakikishiwa na Tume ya uchaguzi + vyombo vya dola kuwa ataongoza kwa kipindi cha pili sasa anashindwa kuficha hiyo hali kwakutamka maneno ambayo anajua kipindi cha kampeni si mazuri. "Jeshini mtu kama huyu anauwawa kwasabau ni msaliti" baada ya kauli hiyo.

Zipo kauli nyingi ambazo ni za kukera, kujaa kiburi, ubabe ambazo si sahihi kwa mgombea nafasi ile nzito kuzitoa lakini tunazisikia..
Wananchi ndio waamuzi hata kama matokeo yatatangazwa vingine. Mungu ibariki Tanzania yetu.
 
Back
Top Bottom