Wananchi wa Kibaha Vijijini kubomolewa nyumba zao, Mbunge asema anapeleka mashtaka kwa Waziri Mkuu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
Baadhi ya Wananchi wa Matuga, Kibaha Vijijini Mkoani Pwani wamelalamika uamuzi wa kubomolewa kwa nyumba zao pasipokuwa na taarifa huku wakidai kutokuwa na tamko rasmi la taarifa kutoka kwenye mamlaka.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamedai zoezi hilo limefanyika Februari 5, 2023 na kutarajiwa kuendelea Februari 6, 2023 ambapo wabomoaji wamedai wamefikia hatua hiyo baada ya kutolewa kwa amri ya Mahakama.

5741c586-d59e-4060-bc84-88e5d86a5d0c.jpg

aed71839-bfd1-4c3b-b78e-af6a5c51946b.jpg
Akizungumzia zoezi hilo, Alfred Daniel Malega ambaye ni Diwani wa Kata ya Kawawa amesema hadi zoezi la uvunjaji linafanyika hakuwa na taarifa.

Anasema “Nilipowasiliana na RPC wa Pwani akasema yeye anazo taarifa juu ya kinachoendelea, lakini nikamjulisha Wananchi hawajui mgogoro wa kesi unavyoendelea, pia nikamweleza kilichofanyika si haki kwa kuwa bora Wananchi wangekuwa na taarifa wangejiandaa.”

Nyaraka ambazo zimeonekana za kesi hiyo zimeonesha kulikuwa na kesi kati ya Omari Kadri dhidi ya Mwenyekiti wa Mtaa wa Zegereni pamoja na Bartazar Simeon.

NENO LA SERIKALI ZA MTAA
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Matuga, Geofrey Kazinduki amesema amesikitishwa na ubomoaji uliotokea kwa kuwa hakuwa na taarifa hadi muda wa tukio.

Anaeleza: “Nilipofika eneo la tukio nikaonana na Mkuu wa askari aliyekuwa akisimamia zoezi hilo anaitwa Kadogosa, nikajitambulisha na kumuuliza kwa nini wanabomoa, akasema wao wanafuata amri waliyopewa kuvunja akanitaka niondoke haraka la sivyo watanishughulikia.”

Amesema zaidi ya kaya 92 zimebomolewa nyumba zao.

MABAUNSA WAIBA KUKU
Ameongeza “Niliondolewa mbio na mabaunsa wakiwa na marungu, wakaiba na kuku wangu. Inamaana mimi kama Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa sitambuliki na Serikali? Kibaya zaidi wabomoaji hao wameahidi kuwa watarejea na kuendelea kubomoa.

Amesema Wananchi waliobomolewa nyuma wana hali mbaya kimaisha na wengine hawana pa kukaa tangu uamuzi huo ufanyike, lakini pia wanahofua usalama wao kutokana na kupata vitisho kutoka kwa wahusika waliokuwa wakishiriki kwenye zoezi la ubomoaji.
fd87ffd2-cde0-4874-865a-f84ea94a2254.jpg

MBUNGE ASEMA HAJUI LOLOTE
Mbunge wa Kibaha Vijijini, Michael Constantino Mwakamo ameelezea kwa kusema: “Mimi nilikuwa Mtendaji wa Kata ya Mlandizi ambapo eneo hili wanalobomoa ni moja ya maeneo ya kata husika, sikuwahi kusikia kama kuna mgogoro katika eneo hili.

“Lakini kabla ya hapo pia nilikuwa Afisa Utumishi sikuwahi kusikia kuhusu mgogoro huu.

“Kinachonichanganya ni kuwa eneo hilo wanalosema lina kesi, huyo wanayesema ni mmiliki alikuwa na kesi na watu wawili wenye mamlaka, hivyo ukiangalia asili ya kesi kwa jinsi wananchi wanavyozungumza inaonesha wazi kuwa eneo lililobomolewa hawajawahi kuambiwa kama kuna kesi wala mgogoro wa ardhi.

“Nimewaeleza Wananchi pia watulie kwa kuwa inaonekana waliokuja kutekeleza zoezi la ubomoaji walikuwa wakitoa maneno ya kutengeneza chuki kati ya Wananchi na Rais.

“Nimewaeleza Wananchi kuwa wasihusishe jambo hilo na utendaji wa jumla wa Serikali, tumeelekezana mambo machache ya kufatilia kisheria.”

“Kubwa linalowachanga Wananchi ni kuwa ili upinge lazima ujue unachokipinga, wao hawajui kesi imeendeshwaje hadi kufikia maamuzi kutolewa.

“Hatua gani nachukua? Nimekuwa nikifanya mawasiliano na ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi, wamenithibitishia kuwa wanazo taarifa.

“Nilitegemea viongozi hao wangekuja hapa ili kuwafahamisha Wananchi kinachoendelea, kwa kuwa wanajua ni suala la kesi na hawawezi kulizungumzia, nitakachofanya nitaenda kwa Waziri Mkuu kumfikishia suala hili.”

DC AELEZEA
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nickson John amefafanua kwa kusema “Hiyo ni amri ya Mahakama, unapofanya kesi Mahakama ndio inapitia taratibu zote, hivyo kama wahusika hawakubalini na hukumu wana haki ya kukata rufaa. Mahakama inahojiwa kwa mchakato wa kimahakama.

“Taarifa ilitolewa, mchakato wa kuvunjwa huwa unachukua siku 14, uzuri hivyo ni vitu ambavyo vipo kimaandishi.”
Amri ya kuboa Mahakama Kibaha_page-0001.jpg


BARUA KIBAHA- POLISI_page-0001.jpg

 
Zaidi ya kaya 106 zimeachwa bila makazi kata ya Zegereni wilaya ya Kibaha baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana na kuvunjiwa nyumba zao kwa madai ya kupisha muwekezaji.

Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini kupitia ccm amefoka vikali na kusema hamtambui muwekezaji huyo na kwamba wanachi hao wameishi hapo kwa zaidi ya miaka 30.

 
Aisee, Nakumbuka yule firauni alivyokuwa akivunja nyumba za watu kwa fujo baada tu ya kuingia Ikulu, tena kukiwa na zuio la mahakama, kisa hakupigiwa kura na watu wa Dar

Kaenda Usukumani huko katoa tamko marufuku watu kubomolewa kisa walimpigia kura

Ama kweli Mungu Fundi, 17/03/2021 yapaswa kuwa sikukuu kwa Watanzania
 
Hutosikia wapinzani wakipaza sauti... bado wapo bize na Jiwe sijui Mwendazake
Wapaze sauti waseme kwamba hazijavunjwa au?

Unakumbuka Mnyika pale kimara alokwambia Jiwe angalau awalipe walionomolewa nyumba zao unakumbuka majibu aliyoyatoa?

Kwanini kila tatizo kunapotokea mnawalaumu hao jamaa na wanapoongea mnasema wamedandia hoja au hawana hoja? What do you guys need th m to do?
Mbona mnakuwa saddists kiasi hicho
 
Back
Top Bottom