Wakazi wa Kitongoji cha Kigoto, wameuomba Mbunge was jimbo la Sengerema Mh. William Ngeleja kuingilia kati mgogoro kati yao na
mwenyekiti wa serikali ya kijiji baada ya
kuzuiwa kulisha mifugo yao kwenye eneo la
mbuga na kuligeuza mali yake.
Pia, walimuomba Mkuu wa wilaya hiyo,
Zainab Telack kuingilia kati kwa kufuatilia
mmiliki wa eneo lilipo karibu na Mlima
Lwepisi, ambao mwenyekiti huyo anadaiwa
kutumia kwa shughuli za uzalishaji.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakazi
hao walisema eneo hilo walikuwa walikitumia
kulisha mifugo yao, lakini baada ya
mwenyekiti kuapishwa alianza kuwawekea
vikwazo.
Mwenyekiti huyo, Tiba Magambo alikanusha
kuzuia mbuga hiyo kwa lengo la kuifanya
eneo la hifadhi la kijiji na kuliepusha
kuvamiwa na wajanja.
Kuhusu suala la eneo la mlima, Magambo
alisema kwa mujibu wa sheria na taratibu za
nchi, siyo miliki ya mtu, hivyo alizuia ili
uendelee kuwa hifadhi ya kijiji.
Naye Tiba Nsiyonka anayedai mmiliki halali
wa mlima huo, alisema mgogoro uliibuka
baada ya mwenyekiti kumwandikia muhtasari
wa umiliki na kuanza ujenzi wa vibanda vya
ufugaji nyuki.
Mwenyekiti wa Kitogoji cha Kigoto, Mbikisa
Galingulwa alisema aliandika muhtasari wa
kummilikisha mlima baada ya baraza la
wazee kuridhia kuwa mlima huo ulikuwa
kwenye miliki yake halali.
“Niliandika muhtasari wa kumpatia mlima
huo, kutokana na wazee kujiridhisha kuwa ni
eneo lake,” alisema Galingulwa.
Mkuu wa Wilaya Telack aliwataka wakazi hao
kufika ofisini kwake Februari mosi, ili
awasikilize madai yao, yakishindikana
kutatuliwa watapatiwa msaada wa kisheria
badala ya kuendeleza malumbano kwenye
vyombo vya habari.