Wananchi wa Iran waandamana baada ya Serikali kukiri kuitungua ndege ya Ukraine

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,482
9,242
5dba28fe9d52b5492b37afd1af00e29d

Tehran. Muda mfupi baada ya Serikali ya Iran kukiri kuitungua ndege kwa bahati mbaya, kundi la waandamanaji nchini humo limejitokeza kutaka kiongozi wa juu, Ayatollah Khamenei pamoja na viongozi wengine waandamizi kujiuzulu nyadhifa zao.

Ndege aina ya Boeing 737-800, mali ya Shirika la Ndege la Kimataifa la Ukraine (UIA) ilitunguliwa Jumatano iliyopita wakati Iran ikishambulia kambi za kijeshi za Marekani zilizopo Iraq kwa lengo la kulipa kisasi baada ya kuuawa kwa kamanda wake, Qasem Soleimani.

Nchi za Marekani na Canada zilieleza kwamba ndege hiyo iliyokuwa na watu 176 ilitunguliwa na makombora ya Iran wakati wakilenga kuzishambulia kambi za jeshi la Marekani. Baadaye, serikali ya Iran ilikiri kuitungua ndege hiyo kwa bhati mbaya.

Baada ya serikali ya Iran kukiri kutenda kosa hilo, wananchi wake walianza kuandamana sehemu mbalimbali wakiikosoa serikali yao na kuwataka viongozi wake wa juu kujiuzulu nyadhifa zao mara moja.

“Amiri Jeshi Mkuu (Khamenei) jiuzulu, jiuzulu,” video iliyopostiwa kwenye mtandao wa Twitter ilionyesha mamia ya waandamanaji wakiimba mbele ya Chuo Kikuu cha Amir Kabir kilichopo mjini Tehran.

Waandamanaji hao waliwaita viongozi wa Iran “waongo” na kushinikiza wajiuzulu huku wale waliohusika kuitungua ndege hiyo waadhibiwe kwa kosa hilo na kuficha taarifa za kitendo hicho kilichogharimu maisha ya watu kutoka mataifa mbalimbali.

Shirika la habari la Fars liliripoti kwamba jeshi la polisi liliwatawanya wanafunzi ambao walikuwa wakiimba nyimbo za kuwakashifu viongozi wa taifa hilo kutokana na kitendo cha kuangushwa kwa ndege hiyo.

Uingereza ilithibitisha kukamatwa kwa balozi wake nchini Iran, Rob Macaire kwa madai kwamba alikuwa anachochea maandamano ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Amir Kabir. Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Dominic Raab alisema kukamatwa kwa balozi huyo ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa.

Rais wa Marekani ameandika katika ukurasa wake wa Twitter akisema Marekani inafuatilia kwa karibu maandamano ya Iran na kwamba wamevutiwa na ujasiri wa watu wa Iran ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipata shida.

“Serikali ya Iran lazima iruhusu vikundi vya haki za binadamu kufuatilia na kuripoti ukweli halisi juu ya maandamano yanayoendelea ya watu wa Iran. Hakuwezi kuwa na mauaji mengine ya waandamanaji wa amani, wala kuzimwa kwa mtandao. Ulimwengu unaangalia,” ameandika Trump katika ukurasa wake wa Twitter.
 
Wamefanya Rookie mistake kwa kulishwa matango pori ya intel kama ambavyo Egypt alivyotulizwa naona na Iran ya kimagharibi ikirudi
 
'Uingereza ilithibitisha kukamatwa kwa balozi wake nchini Iran, Rob Macaire kwa madai kwamba alikuwa anachochea maandamano ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Amir Kabir.'

Hapo Iran hua nawakubali hamna cha kufuata mikataba ya kimataifa wala nini,balozi akizingua anadakwa chap chap tu.

dodge
 
Maandamano yapo au hayapo?
 
  • Thanks
Reactions: PNC

Anasingizia eti hakushiriki na alikuwa kwa kinyozi alipokamatwa
Hakuna cha diplomatic immunity wala nini ukizingua wanakubeba
Heshima na woga wa mtu mweupe kwisha

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Mm nasisitiza jeshi halina kosa, wenye kosa ni walio iruhusu ndege kupaa wakati jeshi lilisha onya kitu chochote kisipae angani mpaka litakapo toa hakikisho kwamba anga ni salama.
 
'Uingereza ilithibitisha kukamatwa kwa balozi wake nchini Iran, Rob Macaire kwa madai kwamba alikuwa anachochea maandamano ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Amir Kabir.'

Hapo Iran hua nawakubali hamna cha kufuata mikataba ya kimataifa wala nini,balozi akizingua anadakwa chap chap tu.

dodge
Wapenzi wa Iran nawaona mnavyotapatapa. Mkuu sahau kuhusu iran,tayari imepatikana,imeshaingia kwenye target. Soon itakuwa kama Libya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: PNC
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom