Wananchi wa gonja milimani wakosa huduma ya usafiriAmri iliyotolewa ya magari ya abiria wilayani sam

Mavella

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
459
75
Amri iliyotolewa ya magari ya abiria wilayani same
kuondoka mda wa saa 12 asubuhi umeleta adha
kubwa kwa wananchi wa maeneo ya milimani hasa
maeneo ya gonja baada ya mabasi yaliyokuwa
yanafanya usafiri wa dar na arusha kuacha kwenda
huko, kabla ya amri hiyo magari yalikuwa
yanaondoka katika vituo wanakolala kabla ya saa
12 asubuhi
Sababu kubwa ni kuwa mda huo kutokana na
ubovu wa barabara uliosababiswa na mvua zinazo
endelea kunyesha pamoja na mzunguko wa
barabara za milimani itakuwa ngumu kwao kupata
abiria wa maeneo ya mabondeni sababu kama
utatoka saa 12 utafika saa 2 mda ambao watakuta
abiria wote wamechukua wenzao.
Kwakweli kutokana na ubovu wa barabara pamoja
na mzunguko wa barabara za milimani
unaosabashwa na jiografia ya maeneo hayo ni kweli
kuwa wanatumia mda mrefu sana kufika maeneo ya
tambarare, kwa mfano kutoka lilipokuwa linalala
basi mpaka tambarare eneo la gonja maore ni
kama km 30 za barabara mbovu yenye mashimo
na milima.
Kwahiyo wananchi wa maeneo hayo wamekosa
huduma hiyo ya usafiri kabisa wanaomba uongozi
wa wilaya ya same wawaangalie kwa jicho la
huruma ili wenye mabasi hayo waweze kurudisha
huduma hiyo.
 
Back
Top Bottom