Wananchi wa Canada wapendekeza nchi yao iwakilishwe na Rais atakayechaguliwa badala ya Malkia wa Uingereza

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,655
2,000

Canada yataka nchi iwakilishwe na Rais badala ya Malkia


Katika nchi ya Canada ambayo ni mwanachama wa Jumuiya ya Madola ya Mataifa ya Uingereza, takriban nusu ya watu wameitaka nchi yao iwakilishwe na rais atakayechaguliwa badala ya Malkia wa Uingereza.

Asilimia 45 ya wananchi wa Canada walioshiriki mchakato ulioandaliwa na wakala wa utafiti wa kura ya maoni, walibainishwa kwamba wanapendelea kuwa na rais wa nchi aliyechaguliwa kuliko Malkia.

Ilielezwa kuwa pendekezo hili lilikuwa "katika kiwango cha kihistoria" ambapo limeongezeka kwa alama 13 zaidi ikilinganishwa na utafiti kama huo uliofanywa na wakala hao mnamo Februari 2020.

Wakati asilimia 24 ya wahojiwa walionekana kupendelea Canada ibaki ya kifalme, asilimia 18 walisema "hawakujali hata kidogo juu ya suala hili" na asilimia 13 walikosa maamuzi.

Maoni ya kupambana na ufalme, ambayo yaliongezeka hadi asilimia 51 kati ya wanaume wenye umri wa miaka 35-54, yalifikia asilimia 57 kati ya wakaazi wa mkoa wa Quebec, wanaojulikana kwa maoni yao ya kujitenga.

Asilimia 31 ya wahojiwa walisema nchi hiyo itakuwa na rais aliyechaguliwa katika miaka 20 ijayo.
Watu walioshiriki utafiti huo pia walisema kwamba chaguo la kwanza la mrithi wa Malkia Elizabeth II atakapofariki, ni Prince William.

Wakati asilimia 35 ya watu wakionekana kutaka kumwona Prince William kwenye kiti cha enzi kama Mfalme wa Uingereza, asilimia 22 yao walitoa maoni ya kumpendelea Prince Charles.
 

Fursa Pesa

JF-Expert Member
May 30, 2012
3,834
2,000
Mitikisiko iliyokumba tawala nyingi Duniani inaweza kuikumba UK miaka ijayo.

Cha msingi kufanyia kazi mapema hisia na mitazamo ya walio wengi ili UK iendane na Dunia ya leo kiutawala.
 

Emmanuel J. Buyamba

Verified Member
May 24, 2013
1,073
2,000
Kwamba Malkia Elizabeth akifa mrithi awe Prince William? Wamejuaje kama Malkia Elizabeth atatangulia kabla ya huyo Prince?

Halafu Canada wameshakua huu upuuzi wa kuendelea kutawaliwa na Mwingereza waachane nao.
 

Mkongwee

JF-Expert Member
Jul 29, 2018
288
1,000
daaaaaaah yaani kumbe kile kibibi cha Uingeleza bado kina nafasi kubwa kwenye Taifa lingine tena kubwa kabisa la Canada
aiseeee duniani kuna mamboooo
 

Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
7,533
2,000
Lakini serikali inakuwa chini ya Waziri Mkuu, huu utawala wa malkia ni symbolic tu.
 

bwii

JF-Expert Member
May 24, 2014
1,220
2,000
daaaaaaah yaani kumbe kile kibibi cha Uingeleza bado kina nafasi kubwa kwenye Taifa lingine tena kubwa kabisa la Canada
aiseeee duniani kuna mamboooo
sio Canada tu bali hata Australia
 

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
4,442
2,000
Mitikisiko iliyokumba tawala nyingi Duniani inaweza kuikumba UK miaka ijayo.

Cha msingi kufanyia kazi mapema hisia na mitazamo ya walio wengi ili UK iendane na Dunia ya leo kiutawala.
Mitazamo ya Waingereza [walio wengi] kwa sasa ni kuendelea na utawala wa Kifalme.
 

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
May 27, 2016
4,442
2,000
Kwamba Malkia Elizabeth akifa mrithi awe Prince William? Wamejuaje kama Malkia Elizabeth atatangulia kabla ya huyo Prince?

Halafu Canada wameshakua huu upuuzi wa kuendelea kutawaliwa na Mwingereza waachane nao.
Si rahisi kwa Canada kuachana na utawala wa Kifalme (Monarchy). Pia, hakuna sababu ya lazima ya kufanya hivyo.

Ili iachane na utawala huo, italazimu kufanyika kwa mabadiliko ya katiba ambayo yataridhiwa na bunge (mabaraza yote) pamoja na majimbo yote ya Canada kwa mujibu wa Katiba ya Canada. Hii ni process ndefu ambayo inaweza kushindikana endapo jimbo moja tu litakataa.
 

Fursa Pesa

JF-Expert Member
May 30, 2012
3,834
2,000
Mitazamo ya Waingereza [walio wengi] kwa sasa ni kuendelea na utawala wa Kifalme.
Ni kweli, lakini vipi mitazamo ya wasio waingereza/waingereza walio nje ya Uingereza?
Cha kufanya labda ni kuweka bases mpya za Malkia /Mfalme kila nchi iliyo chini ya UK ili nao waone uwepo wa Ukuu wa Utawala.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom