Wananchi wa Bujonde Kyela wamkataa Mwenyekiti waliochaguliwa na CCM

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,684
8,832
Habari kamili, Bujonde:

Wananchi wa kitongoji cha itope kata ya Bujonde wamemkataa vikali mwenyekiti wao mpya kupitia Chama cha Mapinduzi kuwa hawamtambui na kusema hawataki atoe matangazo yoyote kuhusiana na kitongoji hicho.

Hayo yametokea leo katika msiba wa ndugu David Kimetelo alifariki jana kutokana na ajali ya gari hapa Kyela Mjini maeneo ya Orofea.

Sintofahamu hii imetokea pale MC wa msiba huo alipotoa nafasi kwa serikali ya kitongoji hicho kutoa matangazo kama ilivyo kawaida ya misiba yote, lakini wananchi hao wamekataa katakata Mwenyekiti huyo kutoa matangazo, hali iliyomlazimisha Mwenyekiti huyo kushindwa kusogea hata eneo la meza kuu ili atoe matangazo yake.

Aidha ikapendekezwa kuwa mtendaji wa kijiji atoe matangazo badala ya mwenyekiti lakni nayeye wamemkata na kusema kuwa hao viongozi sio chaguo lao.

Vuta nikuvute hii ikaendelea hadi pale Katibu wa kanisa la Last Church a.k.a Ngemela alipolazimika kutoa matangazo kwa niaba ya serikali suala ambalo si kawaida na nikinyume na utaratibu.

Mpaka watu wanatawanyika katika msiba huo, si Mwenyekiti wala si Mtendaji aliyethubutu kutoa matangazo msibani hapo.

Nikiripoti kutoka eneo la tukio katika kitongoji cha Itope, kijiji cha Itope kata ya Bujonde mimi ni Daniel Brighton wa Ijimbwi.
 
na hapo ndio tatizo litakuja, tofauti na viongozi wengine, hao viongozi wa mitaa wanaishi pamoja na wananchi, kama wananchi wataamua kuwatenga kwenye kilakitu basi maisha yao yatakua magumu sana.

lakini hatari kubwa zaidi ni mpasuko katika jamii, itafika kipindi watu wa CCM wakipata matatizo basi wa vyama vingine hawahangaiki kuwasaidia vilevile wa vyama vingine hawatakubali msaada wa watu wa CCM.

Asante Magufuli kwa kuendelea kuigawa nchi yetu huku 'wazalendo uchwara' wakikukenulia meno tu. siku wakijakujua kuwa maslahi ya nchi ni muhimu kuliko 'ego' ya rais itakua too late.
 
Ni imani yangu wapo wana ccm wengi hata wateule ambao hawafurahishwi na figusu za kubebwa zinazo haribu umoja wa taifa letu. Ushauri wengu tupeane elimu wajitambue wajiudhuru nyathifa zao kupisha ushaguzi halali.
 
Back
Top Bottom