Wananchi wa Bujonde Kyela wamkataa Mwenyekiti waliochaguliwa na CCM

Wananchi wa kijiji cha Ruvu Jiungeni, Same wamemkataa mwenyekiti wa kijiji kwa tiketi ya CCM katika mkutano wa kijiji wakidai hawakumchagua baada ya Mkuu wa wilaya kufanya ziara katika kijiji hapo!

Jamiiforums kwa sasa ni haina chujio la habari zinazoletwa hapa jukwaani!
Kuna tofauti sana kati ya hii yako na ile iliyoletwa huko juu. Utakuwa una matatizo kama huoni tofauti hizo.
 
Kyela si kama kwenu Chamwino , Mwenyekiti wenu amekataliwa na asipojiuzulu yatamkuta makubwa zaidi
Erythro, rafiki yangu, hapa kuna jambo zuri sana.

Hali hii waTanzania wakijua jinsi ya kuitumia vyema itatuondolea hofu na uwezekano wa kumwaga damu za waTanzania, jambo ambalo ndio wanalolitegemea sana wenye madaraka.

Unauona uwezekano huu kama ninavyouona mimi? Mmeujadili kwa kina na mapana yake ndani ya chama ili utekelezaji wake uandaliwe vyema?

Huwa unalalamika sana hapa tunapojaribu kuwapa mbinu mbalimbali za kuwapunguzia maumivu viongozi wenu. Je, hili nalo mtaliachia lipotee bure?
 
Huyu jiwe aneamua kuingwa taifa kabisa kwa hizi hujuma na huu ukatili wake, sasa taifa imegawayika, na niseme hizi kuirudisha taifa pamoja itakuwa kazi nzito sana, sasa chuki imeongezeka sana hapa kwetu, mungu tulikukosea wapi, siumupumuzishe huyu jambazi gaidi la ajabu
 
Binafsi nimekuwa nikijitahidi kusaidia mambo mbalimbali katika kata yetu. Kwa mwaka nimekuwa nikisaidia kati ya TZS 20 - 30m. Lakini kwa uhuni huu uliofanyika ndiyo mwisho. Karibuni nimeletewa ombi, nikalitupilia mbali.

Lakini pia nimekuwa nikiishawishi kampuni ambayo mimi ni mmoja wa wakurugenzi, kusaidia mambo ya kijamii kwenye vijiji. Nilipoona ule upuuzi uliofanyika kwenye uchaguzi, nikasema ndiyo mwisho. Utatoaje msaada usimamiwe na mtu ambaye una uhakika hakuchaguliwa? Uwezekano mkubwa hata hao unaowasaidia, hawatampa ushirikiano kiongozi aliyepachikwa.
Unajua mkuu Bams, kuna njia nzuri na salama sana za kuzima na kuondoa ukandamizaji huu tunaoushuhudia sasa hivi bila ya kuwepo na vurugu na hata kumwaga damu za waTanzania.

Huu mfano ulioutoa hapa ni njia mojawapo, laiti kama watu kama nyinyi katika umoja wenu huko kwenye biashara mngeshawishiana kuchukua hatua za pamoja, mambo yangeanza kubadilika haraka sana. Makundi mengine mbalimbali nayo kwa umoja wao wangechukua hatua , ingesaidia sana kuleta mabadiliko kwa njia ya amani.

Wananchi vitongojini wangekataa kutoa ushirikiano, kama ilivyoelezwa katika mada hii, hao wanaotuvuruga wangefanya nini?
Wanaweza kuwaweka wanaogomea viongozi hao wa kuteuliwa vizuizini?

Watapeleka polisi wakawasombe watu kwenye makazi yao na kuwapiga virungu kama wanavyofanya wakati wa maandamano?

Tatizo ni kukosa uongozi na usimamizi wa mambo haya ili yafanyike kwa ufanisi.
 
Huyu jiwe aneamua kuingwa taifa kabisa kwa hizi hujuma na huu ukatili wake, sasa taifa imegawayika, na niseme hizi kuirudisha taifa pamoja itakuwa kazi nzito sana, sasa chuki imeongezeka sana hapa kwetu, mungu tulikukosea wapi, siumupumuzishe huyu jambazi gaidi la ajabu
Mimi nina imani, taratibu watu wameanza kutambua tatizo lillpo. Mwisho wa siku, wananchi wenyewe wataliondoa na tutaendelea sote kwa umoja wetu. Nchi hii ilijengwa katika msingi imara sana, sio rahisi kwa kiongozi mmoja kuja kuvuruga taifa ambalo limekuwa mfano wa kuigwa, sio Afrika tu, bali duniani kote.

Asilani hatofanikiwa kutuvuruga.
 
Binafsi nimekuwa nikijitahidi kusaidia mambo mbalimbali katika kata yetu. Kwa mwaka nimekuwa nikisaidia kati ya TZS 20 - 30m. Lakini kwa uhuni huu uliofanyika ndiyo mwisho. Karibuni nimeletewa ombi, nikalitupilia mbali.

Lakini pia nimekuwa nikiishawishi kampuni ambayo mimi ni mmoja wa wakurugenzi, kusaidia mambo ya kijamii kwenye vijiji. Nilipoona ule upuuzi uliofanyika kwenye uchaguzi, nikasema ndiyo mwisho. Utatoaje msaada usimamiwe na mtu ambaye una uhakika hakuchaguliwa? Uwezekano mkubwa hata hao unaowasaidia, hawatampa ushirikiano kiongozi aliyepachikwa.

Nahisi ww ni mwanaume umekataa kistaarabu!huo m-barua wao ningeletewa mm ndo mkurugenzi🤣🤣! Ningewaambia mnikome na tusizoeane!huandiki kingine!safi sana !tuoneshe kwa vitendo!
 
Kuna tofauti sana kati ya hii yako na ile iliyoletwa huko juu. Utakuwa una matatizo kama huoni tofauti hizo.

Usiwaze kumhusu huyo!mara nyingi wanaume wakiwa hawana hela wanakuwa stressd sana..achana naye hajui hata chai atakunywa kwa nani leo!😇au hajapewa b7!
 
Mimi nina imani, taratibu watu wameanza kutambua tatizo lillpo. Mwisho wa siku, wananchi wenyewe wataliondoa na tutaendelea sote kwa umoja wetu. Nchi hii ilijengwa katika msingi imara sana, sio rahisi kwa kiongozi mmoja kuja kuvuruga taifa ambalo limekuwa mfano wa kuigwa, sio Afrika tu, bali duniani kote.

Asilani hatofanikiwa kutuvuruga.
AMINA
 
Back
Top Bottom