Wananchi wa Bujonde Kyela wamkataa Mwenyekiti waliochaguliwa na CCM

Nazjaz

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Messages
6,554
Points
2,000

Nazjaz

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2011
6,554 2,000
Habari kamili, Bujonde:

Wananchi wa kitongoji cha itope kata ya Bujonde wamemkataa vikali mwenyekiti wao mpya kupitia Chama cha Mapinduzi kuwa hawamtambui na kusema hawataki atoe matangazo yoyote kuhusiana na kitongoji hicho.

Hayo yametokea leo katika msiba wa ndugu David Kimetelo alifariki jana kutokana na ajali ya gari hapa Kyela Mjini maeneo ya Orofea.

Sintofahamu hii imetokea pale MC wa msiba huo alipotoa nafasi kwa serikali ya kitongoji hicho kutoa matangazo kama ilivyo kawaida ya misiba yote, lakini wananchi hao wamekataa katakata Mwenyekiti huyo kutoa matangazo, hali iliyomlazimisha Mwenyekiti huyo kushindwa kusogea hata eneo la meza kuu ili atoe matangazo yake.

Aidha ikapendekezwa kuwa mtendaji wa kijiji atoe matangazo badala ya mwenyekiti lakni nayeye wamemkata na kusema kuwa hao viongozi sio chaguo lao.

Vuta nikuvute hii ikaendelea hadi pale Katibu wa kanisa la Last Church a.k.a Ngemela alipolazimika kutoa matangazo kwa niaba ya serikali suala ambalo si kawaida na nikinyume na utaratibu.

Mpaka watu wanatawanyika katika msiba huo, si Mwenyekiti wala si Mtendaji aliyethubutu kutoa matangazo msibani hapo.

Nikiripoti kutoka eneo la tukio katika kitongoji cha Itope, kijiji cha Itope kata ya Bujonde mimi ni Daniel Brighton wa Ijimbwi.
 

ELI-91

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2014
Messages
3,606
Points
2,000

ELI-91

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2014
3,606 2,000
na hapo ndio tatizo litakuja, tofauti na viongozi wengine, hao viongozi wa mitaa wanaishi pamoja na wananchi, kama wananchi wataamua kuwatenga kwenye kilakitu basi maisha yao yatakua magumu sana.

lakini hatari kubwa zaidi ni mpasuko katika jamii, itafika kipindi watu wa CCM wakipata matatizo basi wa vyama vingine hawahangaiki kuwasaidia vilevile wa vyama vingine hawatakubali msaada wa watu wa CCM.

Asante Magufuli kwa kuendelea kuigawa nchi yetu huku 'wazalendo uchwara' wakikukenulia meno tu. siku wakijakujua kuwa maslahi ya nchi ni muhimu kuliko 'ego' ya rais itakua too late.
 

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Messages
11,739
Points
2,000

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2012
11,739 2,000
Wananchi wa kijiji cha Ruvu Jiungeni, Same wamemkataa mwenyekiti wa kijiji kwa tiketi ya CCM katika mkutano wa kijiji wakidai hawakumchagua baada ya Mkuu wa wilaya kufanya ziara katika kijiji hapo!

Jamiiforums kwa sasa ni haina chujio la habari zinazoletwa hapa jukwaani!
 

Forum statistics

Threads 1,389,064
Members 527,848
Posts 34,016,403
Top