Wananchi wa bahi wala pumba za mahindi;kikwete unajua hili?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi wa bahi wala pumba za mahindi;kikwete unajua hili??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Oct 29, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,613
  Likes Received: 5,782
  Trophy Points: 280
  Bahi wala pumba za mahindi na Danson Kaijage, Bahi PAMOJA na juhudi za kutoa msaada wa chakula katika maeneo mbalimbali mkoani hapa, Wilaya ya Bahi bado inakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na kusababisha wakazi wake kula pumba za mahindi ambazo nazo hupatikana kwa shida. Haya yalibainishwa na wakazi wa wilaya hiyo walipozungumza na Tanzania Daima baada ya kutembelea Kijiji cha Makanda kilichopo wilayani Bahi, Dodoma. Mmoja wa wakazi hao, Julia Kuselya (76) alisema wanakabiliwa na njaa iliyosababishwa na ukosefu wa mvua na kwamba sasa wanaishi maisha ya dhiki kubwa kutokana na kukosa chakula. Alisema pamoja na kukosa chakula, pia maji nayo ni tabu, kwani hulazimika kutembea umbali mrefu kufuata maji. Kuselya alisema ili kujinusuru na njaa wamefikia hatua ya kununua debe la pumba za mahindi na kuzisaga upya na kuzitumia kama chakula na pumba hizo hupatikana kwa shida, kwani debe huuzwa sh 2,500. Aidha, alisema kutokana na hali hiyo, baadhi ya wazazi wanalazimika kuwazuia watoto wasiende shule, ili waweze kuwasaidia kufanya biashara ndogo ndogo kama kuuza kuni sehemu za mijini ili waweze kupata pesa za kununulia chakula. Pamoja na hayo, wakazi wa kijiji hicho walisema wengi wao walishindwa kwenda kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa kutokana na wengi wao kwenda kutafuta chakula cha familia. Viongozi wa kijiji hicho wamekiri kuwepo kwa njaa, lakini walikataa kuzungumzia kwa undani suala hilo, kwa madai bado ni wageni katika uongozi, kwani wamechaguliwa hivi karibuni. juu Habari Mpya | Matangazo | Bei zetu | Wasiliana nasi | Tuma habari | Webmaster Copyright 2009 © FreeMedia Ltd. Wasomaji national finance news national finance news © free media limited 2009
   
Loading...