Wananchi wa Algeria kupiga kura ya maoni kwa ajili ya kuifanyia mabadiliko Katiba

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Raia wa Algeria watapiga kura ya maoni leo kuhusiana na mapendekezo ya mabadiliko ya kikatiba ambayo upinzani unasema yatasaidia kuupa nguvu udikteta.

Kura hiyo inakuja karibu miezi kumi na tisa baada ya maandamano makubwa yaliyompelekea rais wa muda mrefu wa nchi hiyo Abdelaziz Bouteflika kuachia ngazi.

Rais Abdelmadjid Tebboune ambaye kwa sasa anapokea matibabu nchini Ujerumani aliahidi kuifanyia mabadiliko katiba baada ya kuchaguliwa kwake mwezi Disemba ingawa waandamanaji wamesema kuwa mabadiliko hayo si ya kidemokrasia.

Mabadiliko hayo yanampa rais uwezo wa kuhudumu kwa kipindi cha mihula miwili ya miaka mitano na mamlaka ya kumchagua waziri mkuu kutoka kwa chama cha walio wengi bungeni.

Ingawa wanaounga mkono wanasema mabadiliko haya yanaonyesha Algeria mpya wakosoaji wanaonya mamlaka haya yanakwenda kinyume na ahadi ya Tebboune ya kuondoa udikteta nchini humo.
 
Baada Ya Uchaguzi Nasisitiza tupige kazi kwa Bidii, tujipange kwa 2025.
 
Back
Top Bottom