Wananchi Tunduru watozwa shillingi 50 kwa kila kilo 1 ya korosho kujenga vyoo vya shule

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Katika msimu wa zao la korosho mwaka 2017/2018 wakulima wa Wilaya Tunduru watachangia shilingi 50 kwa kila kilo moja ya korosho na fedha zitakazopatikana zitaelekezwa katika kuboresha miundombinu ya shule ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyoo vya kisasa.

Taarifa iliyotolewa na Afisa Elimu Shule za Msingi Wilaya ya Tunduru, Jafari Abrahaman kupitia Kitengo cha Habari na Mawasiliano inaeleza kuwa Halmashauri hiyo inaendelea na mikakati ya kumaliza tatizo la uhaba wa vyoo katika shule zote ili kuwawezesha wanafunzi kufikia ndoto zao.

“Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 jumla ya milioni 30 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi”, inaeleza ripoti hiyo.

Halmashauri hiyo ina jumla ya shule za msingi 150 zilizopo katika vijiji 157 zikiwa na wanafunzi 62,139 ambapo wavulana ni 31,303 na wasichana ni 30,836.

Kutokana na ongezeko la wanafunzi katika shule limesababisha mahitaji ya vyoo yaongezeke pia. Ili kukabiliana na changamoto hiyo, Halmashauri kupitia makusanyo yake ya ndani katika kipindi cha mwaka 2016/2017 ilitenga fedha katika bajeti ya uboreshaji wa matundu ya vyoo.

Milioni 38.8 zilitumika katika ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi Wilayani Tunduru na miradi hii ya ujenzi wa vyoo ipo katika hatua mbali mbali. Vilevile kupitia fedha za ruzuku ya miradi ya maendeleo, milioni 21 zilielekezwa pia katika ujenzi wa matundu ya vyoo hivyo kupunguza changamoto hii kwa kiasi kikubwa

Zaidi, soma hapa => www.fikrapevu//.Wananchi watozwa sh. 50 kugharimia ujenzi wa vyoo Tunduru
 
Back
Top Bottom