Wananchi tumekuwa tukiingilia Uhuru wa Mahakama, tubadilike

Jul 11, 2020
64
139
Kumekuwa na tabia kwa wananchi kusema katika mihimili ya serikali, kuna muhimili mmoja huwa unaingilia mamlaka za mihimili nyingine. Mihimili inayotambulika hadi sasa ni Serikali Kuu(Executive), Bunge na Mahakama.

Lakini kwa kiasi kikubwa wananchi wamekuwa wakiingilia uhuru wa mahakama mara kwa mara kwa jina la harakati au kusema fulani ameonewa. Ni muhimu tujue ya kwamba kila raia anaweza kufikishwa mbele ya mahakama, hukumu itakayotoka ndio itaonesha kama mtu ameonewa au la, kwa kuangalia namna kesi imeendeshwa.

Mara kadhaa watanzania tumekuwa tukiona mtu maarufu au mashughuli akiwajibishwa na sheria tunaingia mitandaoni na kusema kuwa ni visa, wanamuonea na maneno mengi kama hayo, badala ya kufuatilia kesi na hukumu itakapotoka ndio tuseme ameonewa.

Kitu kizuri kwa siku hizi ni hili suala la kuandika kesi kwa kiswahili, jambo la kwanza ni kutaka mlolongo wa kesi uwe wazi ili kila raia asome hoja za pande za washtaki na mshtakiwa kisha kuangalia hukumu kabla ya kulalamika mtu kuonewa kabla ya kuruhusu mahakama kufanya kazi yake.

Ni kitu cha kawaida nchi nzhi za nje watu maarufu kukamatwa na kufikishwa mahakami, aidha mara nyingi wanapoandamana kutaka haki ni pale ambapo wanapoona mtu ameonewa na hatua hazichukuliwi, kwa mfano mauji ya George Floyd Marekani watu waliandamana kutaka haki itendeke.

Tabia ya kuona Mahakama inaingiliwa na muhimili fulani huku wananchi wakiwa mstari wa mbele kuingilia uhuru wa mahakama ni jambo ambalo linadhihirisha hatutaki vyombo hivi viwe huru katika maamuzi.

Aidha kama wewe ni raia na unauhakika kuwa fulani hajafanya jambo fulani, mathalani kukwepa kodi au kutakatisha fedha, unaweza kuwasiliana hata na wanasheria ilikuhakikisha unasaidia kuthibitisha kuwa mtu unayemfahamu hana hatia ya makosa yanayosemwa juu yake.

WITO WA MABADILIKO
Ni muhimu sasa tuanze kufuatilia mlolongo wa kesi ili kusema kama shida katika maamuzi, ambapo I baada ya ukumu kutoka. Ambapo itajumuisha kuangalia mianya ya hukumu iliyotangulia ambayo itasaidia katika kukata rufaa.

Kutumia mitandao ya kijamii kuleta fujo kwa kesi zinazoendelea kwa kuwa mtu ni maarufu ni kuingilia uhuru wa mahakama.
 
Hujaeleweka....

Hoja yako haiko specific kwa sababu hata husemi ni nani au raia gani kaingilia mahakama to the extent kwamba ame - influence maamuzi ya kesi fulani specific...

Na kwa ufahamu wangu mimi, serikali kwa maana ya watendaji wa executive branch of the government kama vile Rais mwenyewe, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya nk nk ndiyo wenye tabia mbaya ya kuuingilia na ku - influence maamuzi ya mahakama ktk baadhi ya kesi hususani zile za kisiasa...

Mathalani, kwenye sakata hili linaloendelea sasa hivi la Mwenyekiti wa CHADEMA taifa Mh. Freeman Aikael Mbowe na viongozi wengine kila mwenye akili timamu anaweza bila hata kuwa msomi wa sheria kuelewa moja kwa moja kuwa, linafanyika kwa maelekezo maalumu ya viongozi wenye mamlaka na madaraka makubwa ndani ya serikali...

Kwa maana hiyo, usitegemee mtu wa namna hiyo anapokuwa ametengenezewa makosa makubwa, hatari na mabaya na watawala kisha akapelekwa mahakamani halafu utegemee mahakama itende haki kwa mujibu wa sheria...

Maana yangu ni kuwa, hawa watawala waovu influence yao itaingia mpaka ndani ya mahakama na majaji au hakimu ktk kutoa hukumu wanayoitaka watawala hawa...

Ipo mifano mingi ya kesi za zilizoamuriwa kwa influence ya watawala kwa sababu ya maslahi ya kisiasa ya waliopo madarakani; mfano hukumu ya Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu, Freeman Mbowe na viongozi wenzake wa CHADEMA nk nk...

Sasa ni mtu mpumbavu tu anayeweza kufuata ushauri wako huu wakati mfumo mzima wa kisheria na kiutawala uko compromised....

Kupiga kelele ni muhimu sana ktk mazingira haya ili waonevu hawa ifike mahali waweze hata kuingiwa na hofu kutaka kuonea watu bila sababu...
 
Back
Top Bottom