Wananchi ruksa kupinga maamuzi ya bunge!

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
15,394
12,978
Wananchi ruksa kupinga maamuzi ya bunge

2008-05-06 10:31:53
Na Gaudensia Mngumi


Iwapo wananchi hawakuridhika na uamuzi uliofanywa na Bunge au wamebaini kuwepo kwa kasoro kwenye baadhi ya vipengele vya sheria, wanaweza kuwasilisha hati ya kupinga maamuzi au ya kutaka kurekebishwa kwa sheria wanazoona hazina maslahi kwa umma.

Kanuni za Kudumu za Bunge, toleo la 2007 linawapa Watanzania wa makundi mbalimbali idhini ya kuandaa hati ya kukataa jambo kwa kuliwasilisha ombi bungeni ili kufanyiwa marekebisho au kuondolewa.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 34, wana jamii wanaweza kuandaa pingamizi kwa jambo wasiloridhia na kuweka saini zao kisha kulikabidhi kwa mbunge yeyote ili awakilishe bungeni.

Hayo ni miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa mwishoni mwa wiki kwenye warsha ya vyombo vya habari na Bunge iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 34(1) mbunge yeyote anaweza kuwasilisha bungeni maombi kuhusu jambo lolote kwa niaba ya watu wanaotoa lalamiko au pendekezo.

Hata hivyo, inasisitiza kuwa halitawasilishwa bungeni mpaka kwanza taarifa za kufikishwa kwake zimetolewa kwa maandishi na kupokelewa na Katibu wa Bunge kwa kipindi kisichopungua siku mbili za kazi kabla ya mkutano wa Bunge ambao ombi hilo linakusukudiwa kufikishwa.

Katika mjadala huo ulioshirikisha maofisa wa Ofisi ya Bunge na waandishi wa waandamizi na wanaoandika habari za Bunge ilielezwa kuwa ombi lolote linaweza kuwasilishwa bungeni na Mbunge likiwa na jina la mbunge huyo anayelipeleka.

`Mbunge anayewasilisha ombi atatoa maelezo mafupi ya kutambulisha watu wanaotoa ombi hilo, idadi yao, saini zilizoambatanishwa kwenye ombi hilo, madai ya msingi yaliyomo na madhumuni ya ombi hilo,` kinasema kifungu cha 34(3).

Kwa upande mwingine washiriki walielezwa kuwa wananchi wasikae kimya na kulalamika bali waeleze masuala ya msingi wasioridhirika nayo kwa kuwasilisha maombi bungeni kwani kanuni na sheria za nchi zinawaruhusu.

SOURCE: Nipashe
 
Back
Top Bottom