Wananchi Rufiji watakiwa kutunza miradi ya maji

daniel burton

New Member
Jul 19, 2021
1
0
WANANCHI RUFIJI WATAKIWA KUTUNZA MIRADI YA MAJI

Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowelle amewataka Wananchi wa Wilaya ya Rufiji kuhakikisha Wanatunza na kuiendeleza miradi ya Maji Vijijini inayotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).

Ameyasema hayo katika Mkutano na Wananchi wa Kijiji Cha Nyaminywili Kata ya Kipugira ambapo amekagua mradi wa Maji na kusikiliza kero za Wananchi hao.

" Serikali imetoa fedha nyingi ili kutuinua Wanarufiji hasa katika swala zima la kumtua mama ndoo kichwani. Ni wajibu wetu kuitunza na kuilinda miradi hii ili inufaishe kizazi Cha Sasa na baadae." Alisema.

Aidha amezitaka Kamati za maji katika kila mradi kuhakikisha zinasimamia Vizuri miradi hiyo na kushirikiana kwa ukaribu ili kupata fedha zitakazo uwezesha mradi kujiendesha pamoja na kukuza mapato ya Vijiji.

Aidha amemshukuru Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa Mbunge wa Jimbo la Rufiji kwa namna anavyowapigania Wananchi wake hasa katika maswala ya maendeleo ikiwemo uletaji wa wafadhili mbalimbali ambao wamechimba visima na kutatua kero za maji Vijijini na kueleza kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha Wananchi Wote wanaondokana na adha ya ukosefu wa Maji.

Awali akitoa taarifa ya Miradi ya Maji inayotekelezwa, Kaimu Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini( RUWASA) - Rufiji, Mhandisi Tluway Ninga amesema Serikali imetoa takribani shilingi milioni 846 kwaajili ya utekelezaji wa Miradi nane ( 08) ambayo inatekelezwa katika Kata ya Mohoro, Kipugira, Mkongo, pamoja na Mwaseni.

Ameeleza kuwa mpaka Sasa miradi yote ipo katika hatua ya umaliziaji na mitatu Kati ya hiyo imeshaanza kutoa huduma za maji kwa Wananchi.

Aidha Mhandisi Ninga ameeleza kuwa kutokana na utekelezaji wa Miradi mingi ya maji Wilaya ya Rufiji imekuwa ukipata nafasi nzuri katika ngazi ya Mkoa na kuendelea kupokea fedha kutoka mfuko wa lipa kulingana na matoke (PbR) ambapo takribani shilingi milioni 386 zimetolewa kwa Wilaya ya Rufiji na tayari zimeingizwa katika utekelezaji wa Miradi.
 
Back
Top Bottom