Wananchi ndio Serikali, lakin wananchi hawana nguvu(maamuzi) wala ushawishi kuizidi Serikali

Pain killer

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
14,156
21,295
Habari wakuu

Mimi binafsi kuna vitu nashindwa kuelewa kwenye nchi yetu ya demokrasia, wanasema wananchi ndio serikal

Lakini bila kupindisha maneno, sijajua labda sisi watanzania ndivo tulivo, nchin kwetu hakuna kitu kinachoitwa nguvu ya umma, japo kuwa ni nchi ya demokrasia.

Yaani serikali inanguvu kuzid wananchi, wananchi hawana maamuzi juu ya seriakali.

ile kauli ya mheshimiwa inayosema Tanzania ya wanyonge, aisee hii kauli unaweza kuichukulia poa, ila tunatengeneza taifa la watu wanyonge, tena wanyonge kweli kweli, mayai mayai.

ile Tanzania ya enzi za nyerere yenye kauri za kishujaa haipo tena, watu wananyongonyea na kulegea vibaya mno,wanakufa na matatizo yao vifuani, aisee, hii kitu huwezi amini mpaka upite kwa mtanzania mmoja mmoja.

Hizi kauli za wanyonge, watu masikin, sio nzuri kabisa, maneno yanaumba

Uzi tayari
 
Habari wakuu

Mimi binafsi kuna vitu nashindwa kuelewa kwenye nchi yetu ya demokrasia, wanasema wananchi ndio serikal...
Ulipoenda kupiga kura ulikasimu madaraka ya uongozi wa serikali kwa waliochaguliwa na wengi. Kwa hiyo hao waliopo madarakani ndio Serikali kwa niaba ya wananchi kwa kuwa umewapa mwongozo ambayo ni katiba waiongoze serikali kwa misingi ya katiba na ndio maana wanaapa kuilinda.

Usihofu mkuu huo ndio utaratibu.
 
"Udikteta ni mtu mmoja au kikundi cha watu wachache chenye kutunga sheria kandamizi atakayezivunja kukiona cha moto".

JK Nyerere.

HAKIKA YAMETIMIA MANENO YA MWALIM
 
Habari wakuu

Mimi binafsi kuna vitu nashindwa kuelewa kwenye nchi yetu ya demokrasia, wanasema wananchi ndio serikal...
Tuwakumbushe watawala wa Afrika kuwa kushika hatamu hakukufanyi ugeuke kuwa
1. injinia,
2. daktari bingwa,
3. mhasibu mbobezi,
4. mwanasayansi wa viwango vya NASA
5. au mtaalam zaidi!

Therefore your power doesn’t suddenly increase your knowledge or qualify you to be anything more than you were! Waache u-much-know na upumbavu, wawe humble!
 
Siku hizi nimestaafu kujadili siasa kabisa, hizo nguvu zote natafutia hela napata mademu wakali, bhaaaaasi.
 
Na kwamiaka hii mitano maajabu yataonekana maana hata wale wawakilishi wako itakuwa ni kusifu mwanzo mwisho! Meza ziimarishwe jameni ili wanaposifu zisijevunjika!

Natamani tungekuwa na kanchi mbadala ukichoshwa na maujinga yahuku unaenda pumzika kule
 
Sisi watanzania ndio hatujui wajibu wetu nadhan
 
Hahaaaa
Na kwamiaka hii mitano maajabu yataonekana maana hata wale wawakilishi wako itakuwa ni kusifu mwanzo mwisho! Meza ziimarishwe jameni ili wanaposifu zisijevunjika!
Natamani tungekuwa na kanchi mbadala ukichoshwa na maujinga yahuku unaenda pumzika kule
 
Siasa ndio Maisha mkuu

inakugusa kwa namna moja ama nyingine
Yaani kila inapotaka kugusa maslahi yangu najitahidi kuikwepa kwa namna moja au nyingine. Juzi hapa cement ilivyokwea bei ghafla, wala sikutaka kupambana, nikauza kwa bei niliyonunulia kiwandani+usafiri na ubebaji, mifuko yote ikatoka. Mara wanasiasa hao wanakuja kunikagua, ili wajichukulie umaarufu kupitia jasho langu, wakakuta ghala limejaa chokaa tu.

Wakisha rekebisha mambo nitaleta mali.
 
ile kauli ya mheshimiwa inayosema Tanzania ya wanyonge, aisee hii kauli unaweza kuichukulia poa, ila tunatengeneza taifa la watu wanyonge, tena wanyonge kweli kweli, mayai mayai.
Ni kawaida kwa tawala dhalimu kunyongesha watawaliwa
 
Thus hatuwezi endelea maana wananchi awashirikishwi kwenye upangaji wa vipaumbele vyao.
Watawala upanga vipaumbele vyao ambavyo sio tija kwa wananchi,mfano kununua ndege, kurudia chaguzi, kujenga dodoma, kujenga ikulu mpya, kujenga uwanja wa ndege kijijini,nk.
 
Back
Top Bottom