Wananchi Mpanda (kwa Pinda) wazichapa kugombea ardhi wawili wafa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi Mpanda (kwa Pinda) wazichapa kugombea ardhi wawili wafa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, May 22, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Star tv habari

  JK akiuza ardhi wananchi wazipiga hadi watu wawili kufa
   
 2. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kaka hii nayo ni habari? Mbona kifupi sana na hakieleweki? Yaan thread na contents haziendani hata kidogo!!!! Kama hauna information za uhakika na zinazojitosheleza, siyo lazima kupost, mbona wengine tuna mwezi mzima tunasoma na kuchangia thread za watu tu??? Nimefungua kwa shauku kubwa kweli, kumbe hakuna kitu, au unafikiri wote tuna access na STAR TV?
   
 3. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  WIMBI la wananchi kujichukulia sheria mkononi, limeendelea kutikisa taifa, baada ya kundi la wanakijiji wapatao 3000 wa Kijiji cha Kabage wilayani Mpanda, kuwaua watu wawili kwa kuwashambulia kwa silaha za jadi na kuwajeruhi wengine tisa.

  Mbali ya kufanya mauaji, wananchi walionekana kuwa na hasira na walichoma moto trekta kwa kile kilichoelezwa ni ugomvi wa kugombania shamba la mpunga.

  Tukio hilo la kusikitisha, lilitokea juzi majira ya saa 2 asubuhi kijijini hapo.

  Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Joseph Myuvela, aliwataja marehemu hao kuwa ni Juma Pangani (53) mkazi wa Aitel mtaa wa Nsemulwa na marehemu wawili hawakuweza kutambulika jina.

  Aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni Lufunga maduka (22), Denis Kazimka (23), Joseph Mdachi (28), Maganga Sulu (25), Hamis shababi (29), Noel Kisinza (17), Kabungu Mpanda, Ludovick Sunga (33), Rashid Abdala (28) na wengine wawili ambao majina yao hayakutambuliwa.

  Alisema chanzo cha mauaji hayo, kilitokana na kundi la wanakijiji kupinga maamuzi ya baraza la kata ya Simbwesa, lililotoa maamuzi ya kukipa haki Kikundi cha Nguvu Kazi, kumiliki shamba la mpunga lenye ukubwa wa ekari 650, ambazo zimelimwa mpunga na wanakijiji.

  Alisema baada ya kikundi hicho kupewa mamlaka na baraza la kata juzi, wamiliki wa kikundi hicho, Galus Kasonso na Portazi Ringo walipopeleka vibarua kwenye shamba hilo kwa kutumia trekta yenye namba za usajili T 7006 BQH, walianza kushambuliwa.

  Baada ya vibarua kufika kijijini hapo, wanakijiji walianza kujikusanya na kujadiliana kwanini watu hao wafike kijijini na kuvuna mpunga ambao ulilimwa na wao.

  Ndipo idadi ya watu wapatao 3,000 walipokubaliana na kwenda kuwashambulia.

  Alisema walipofika kwenye kambi ya vibarua hao, walikuta trekta yenye mali ya kikundi cha Nguvu kazi, ikiwa imeegeshwa wakaichoma moto kwa kutumia mafuta ya taa.

  Baada ya kuchoma trekta, walianza kuwashambulia kwa kutumia silaha za jadi, hali iliyopelekea vibarua hao kutimua mbio.

  Alisema baada ya kutimua mbio, wanakijiji waliwakimbiza na kufanikiwa kuwakamata watu wawili, kisha kuanza kuwashambulia kwa mapanga, marungu hadi kufa.

  Jeshi la polisi lilifika katika eneo la kijiji hicho, huku wakiwa na gari lao lenye namba za usajili PT 1529, wakiongozwa na Mkuu wa kituo cha Polisi Mpanda, Magnus Milinga.

  Lakini katika hali ya kushangaza, polisi walikuta nyumba nyingi zikiwa zimebakiwa na mbwa, mbuzi, ngÂ’ombe na kuku kutokana na wengi kukimbia makazi yao.

  Alisema polisi walifanikiwa kuwaokota majeruhi wanne, ambao walikuwa wametupwa vichakani.

  Katibu wa Kijiji cha Kabage, John Malunga alisema viongozi wenzake wanapaswa kulaumiwa kwa kile alichodai kugawa ardhi ya kijiji, bila kuwashirikisha wanakijiji.
   
 4. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umesomeka mkuu,

  Serikali ya CCM chini ya JK inamengi ya kujifunza kutokana na matukio ya ugomvi na migogoro ya ardhi ambayo inaendelea maeneo mengi katika nchi hii. Ila kwa kuwa wana vichwa vya panzi, wanajifanya hawafahamu kinachoendelea. Maendeleo ya nchi hii yanategemea vitu vinne, WATU, ARDHI, SIASA SAFI NA UONGOZI BORA. Kama tunauza ardhi, hatuna siasa safi, uongozi ndio huo wa ccm, unasua sua katika kuchukua maamuzi ya msingi, na viongozi wake wakuu, ndio wakuu wa ufisadi na rushwa, kuwajibika hakuna, hata kuwajibishana hakuna, tumebaki na nini cha kutuletea maendeleo??? Watu tu!! Watu wanayatoa wapi maendeleo kama hakuna ARDHI, SIASA SAFI NA UONGOZI BORA??? That's why we need alternative political party.....CHADEMA FOR LIFE!!!!!

  STK ONE,
  TOGETHER WE CAN BRING THE CHANGES WE NEE....YES WE CAN, GOD BLESS CHADEMA!!!!

   
 5. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Hospitalini kuna majeruhi 15,jana wanakiji wamechoma moto heka 360 za mpunga.Hicho kikundi cha nguvu kazi kinaunda na Afisa Ardhi wa wilaya na wafanyakazi takribani 4 wa serikali ambao walitumia nyadhifa zao kupata heka 360 za ardhi nzuri kabisa kwa mpunga,na kuwabakizia ambayo haifai kwa kilimo ndio chanzo cha ugomvi wote.Jana nilisikia waziri wa ardhi akielezea utaratibu wa kununu ardhi toka kwa kijiji kwamba lazima iamuliwe na mkutano mkuu wa kijiji ambao na afisa ardhi ni mjumbe na lazima watu wote wazima kijijini hapo waweke sahii makubaliano.taratibu izi zote hazikufuatwa.
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Funguka zaidi na source pia utuwekee!
   
Loading...