hugochavez
JF-Expert Member
- Mar 1, 2013
- 1,907
- 1,009
Ni habari ya kusikitisha ndugu lakini ndio ukweli mchungu kuumeza. Pamoja na mh Edward Lowasa kuongoza jimbo hilo akiwa mbunge kwa miaka 20 na uwaziri mkuu juu lakini wananchi wa jimbo la monduli wanateseka kuliko kawaida. wanafikia hatua hatua ya kulala njaa kwa kukosa maji. wananchi wanatembea kilometa zaidi ya kumi kufuata maji huku maji yenyewe yakiwa ya kuchangia na mifugo. shame in you Lowasa. Kijiji cha baraka kata ya engaruka na kata ya moito wameapa endapo mzee huyo atafika na hadaa zake watamtemea mate usoni. Kiufupi amechoka na hawataki kumsikia. Unakuta mtu ana chakula cha kutosha lakini hana maji inabidi alale njaa....kauli ya kina mama katika kijiji cha moita wilayani monduli kwa ngoyai..