Wananchi mkoani Tabora wapongeza jitihada za uboreshaji wa reli ya kati

Tanzania Railways Corp

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
250
583
69b4ae84-5fcc-4fb2-b9d2-6d78dbf26ce5.jpg



Wananchi mkoani Tabora wamepongeza jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Shirika la Reli Tanzania - TRC kwa kuboresha miundombinu ya reli mkoani Tabora kupitia mradi wa uboreshaji wa reli ya kati - TIRP, hivi karibuni Juni 2020.

Wananchi hao wameeleza kuwa Serikali imefanya jitihada hizo baada ya kuona umuhimu wa kuiongezea reli ufanisi na kuboresha huduma za usafiri wa reli ili kuwaletea faida wananchi wanaotumia usafiri huo na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.

Hayo yamezungumzwa na wananchi katika nyakati tofauti wakati wa mahojiano kati ya Maafisa Habari wa Shirika na Wananchi mkoani humo ili kufahamu ni kwa namna gani wananchi wanaweza kutambua fursa na faida zinazopatikana katika mradi mara baada ya mradi huo kukamilika mapema mwezi Oktoba 2020.

Bwana Amos Msasu amesema kuwa mradi wa TIRP utakuwa na faida katika kukuza pato la taifa na kupunguza muda wa safari za treni pamoja na mambo mengine amempongeza Rais Magufuli kwani ni mfano wa kuigwa barani Afrika
“Mradi huu binafsi nimeufurahia sana kwani utakapokamilika utaleta faida sana kwa watanzania lakini kwetu sisi wasafiri itatusaidia kusafiri kwa muda mfupi sana, pia shughuli za usafirishaji mizigo utaongezeka kwani treni zitaweza kubeba mzigo mkubwa na kusafiri kwa muda mfupi” alismea Amos.

Shukuru Martin ambaye ni msafiri kutoka Tabora kuelekea Morogoro amesema kuwa uboreshaji utakapokamilika utaweza kupunguza muda wa safari hivyo utaharakisha shughuli za uzalishaji halikadhalika ameishukuru kazi inayofanywa na Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Inaelezwa kwamba kutokana na chanagamoto ya miundombinu ya reli idadi ya abiria na behewa zinazosafirishwa kwa treni zilipungua lakini kutokana na mradi huu utakaoboresha njia ikiwemo kuongeza urefu wa sehemu za kupishana treni, kupungua kwa muda wa safari na ununuzi wa vichwa vya treni na behewa mpya utasaidia katika kuwavutia wasafiri wengi zaidi na kukuza sekta nyingine kama biashara na uzalishaji.

Christina John ni mfanyabiashara wa Chakula katika Stesheni ya Tabora ameeleza kuwa “hapo awali kulikuwa na treni za behewa 24 lakini hivi karibuni kumekuwa na idadi ndogo ya behewa za abiria lakini tunalipongeza Shirika kwa jitihada zinazofanyika, kwani mradi huu utaongeza idadi ya wasafiri na mimi biashara yangu itafanyika na wasafiri wengi watatamani kusafiri na treni” alisema Christina.

Naye Bwana Erasto Charles amesema kuwa “mimi nafurahi kwa kazi anazozifanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Joh Pombe Magufuli, mojawapo ikiwa ni katika sekta ya reli, kwa maboresho haya naona maisha yetu yanavyoboreshwa na tunakwenda kuwa watanzania wa viwango vya juu”

Aidha mradi huu utasaidia katika kuongeza pato la taifa kupitia kodi zinazolipwa na wasafirishaji wa bidhaa ndani na nchi jirani za Congo, Rwanda, Burundi na Uganda, “usafirishaji wa bidhaa nchi jirani utaongeza pato la taifa kwa kupata fedha za kigeni” alisema Kulwa Omary mwanafunzi wa Uhadhiri Tabora.

Ni hakika kwamba watanzania wana matumaini makubwa na jitihada za serikali katika kuboresha huduma za usafiri wa reli nchini, Shirika linaendelea kuwasisitiza wananchi kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano katika kuboresha huduma za usafiri wa reli nchini.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom