Wananchi Mkoa wa Songwe waitikia wito wa Serikali kujisajili Vitambulisho vya Taifa

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Wananchi wa mkoa wa Songwe wameonyesha mwitikio mkubwa katika zoezi la uasjili wa vitambulisho vya taifa ambalo linafanyika nchini kote na kwa mkoa wa Songwe wilaya zote zinafanya usajili katika ofisi za kata na serikali za kijiji/mitaa. Akizungumza afisa msajili NIDA mkoa wa Songwe Bi Colletha Peter amesema katika zoezi hili la usajili wa mkupuo (mass registration) wananchi wa mkoa wa Songwe wamelipokea vizuri zoezi la usajili na utambuzi wa watu jambo ambalo linaonyesha kuwa sasa wananchi wamepata uelewa mkubwa kuhusu umuhimu wa kusajiliwa na kupata Vitambulisho vya Taifa vitakavyowasaidia katika shughuli mbalimbali za maendeleo. Aidha Bi Colletha amesisitiza wananchi wote ambao bado hawajasajiliwa wajitokeze kwa wingi na kuanza mchakato mara moja kwenye ofisi za serikali za mitaa/kijiji.

Ili kusajiliwa ni lazima Mwananchi awe na umri wa miaka 18 na kuendelea pia afike na nakala (copy) ya nyaraka/viambatanisho muhimu vya kuweza kumtambulisha uraia wake, umri na makazi. Mfano wa nyaraka hizo ni; Kadi ya mpiga kura, cheti cha kuzaliwa, leseni ya udereva, ID ya Mzanzibar mkazi, TIN, Pasi ya kusafiria, vyeti vya elimu nk.

1.jpeg

Pichani: Wananchi wa wilaya ya Mbozi kata ya Igamba mtaa wa Igamba wakiwa kwenye zoezi.


2.jpeg

Pichani: Afisa msajili NIDA Eckson Mwakyembe akimchukua alama za vidole Mwananchi wa Kijiji cha Igamba Mbozi​

Wananchi wanaweza kuwasiliana na NIDA kwa kupitia njia zifuatazo;
 
Back
Top Bottom