MwanaDiwani
JF-Expert Member
- Mar 22, 2013
- 5,536
- 2,264
Msafara wa viongozi, wanachama na wapenzi wa CCM ukielekea kwenye mkutano katika viwanja vya Peoples, Mjini Singida. Anayeonekana kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba na aliyeko kushoto kwake ni Mbunge wa Singida Mjini, Mohamed Dewji.
Katibu Mkuu, Kinana akiwapungia mkono watu waliokuwa wanamshangilia kandoni mwa barabara wakati akielekea kwenye mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Peoples, Singida Mjini.
Umati wa wananchi waliohamasika kwenye Mkutano.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akiwapungia wananchi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa mikutano, kulia kwake ni Nape Nnauye na kushoto kwake ni Mwigulu Nchemba.
Kinana akiangalia bidhaa mbalimbali za Wajasiriamali zilziokuwa zikioneshwa kwenye mkutano huo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Peoples, Mjini Singida, wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mohammed Dewji akitaja utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo kwa asilimia kubwa ameifadhili katika jimbo hilo.
Kinana akijadiliana jambo na Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mohammed Dewji (kushoto) pamoja na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye. wakati wa mkutano huo wa hadhara.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Martha Mlata akiwapungia mkono wananchi wakati wa mkutano huo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba (kushoto) akijadiliana jambo na na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano ya Umma), Steven Wassira wakati wa mkutano huo.
Katibu Mkuu CCM Taifa (katikati) akiwa ameongozana na Naibu katibu Mkuu Mh:Mwigulu Nchemba na Mbunge wa singida Mjini mh:Mo Dewji wakati wakutembelea Ujenzi wa Hospitali Kubwa ya Kisasa Singida Mjini.Hospitali itakayokuwa ni tegemeo kwa Mikoa yote ya kanda ya kati
Moja ya Majengo ya Hospitali Kubwa na Mpya iliyojengwa kwa Nguvu za Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Singida, alipotembelea kituo cha usambazaji maji Singida Mjini
=================================================================================
WAKATI huo huo, CCM pia kimefanya mkutano mkubwa Nungwi, Unguja. Mkutano uliongozwa na Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi
Alichokiongea na na Mzindakae wakiwa Singida
----------------------------------------------
Last edited by a moderator: