Wananchi kwa Maelfu wahudhuria mikutano ya CCM, Singida Mjini na Nungwi, Unguja

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195

Msafara wa viongozi, wanachama na wapenzi wa CCM ukielekea kwenye mkutano katika viwanja vya Peoples, Mjini Singida. Anayeonekana kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba na aliyeko kushoto kwake ni Mbunge wa Singida Mjini, Mohamed Dewji.


Katibu Mkuu, Kinana akiwapungia mkono watu waliokuwa wanamshangilia kandoni mwa barabara wakati akielekea kwenye mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Peoples, Singida Mjini.


Umati wa wananchi waliohamasika kwenye Mkutano.Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akiwapungia wananchi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa mikutano, kulia kwake ni Nape Nnauye na kushoto kwake ni Mwigulu Nchemba.

Kinana akiangalia bidhaa mbalimbali za Wajasiriamali zilziokuwa zikioneshwa kwenye mkutano huo

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Peoples, Mjini Singida, wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mohammed Dewji akitaja utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo kwa asilimia kubwa ameifadhili katika jimbo hilo.

Kinana akijadiliana jambo na Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mohammed Dewji (kushoto) pamoja na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye. wakati wa mkutano huo wa hadhara.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Martha Mlata akiwapungia mkono wananchi wakati wa mkutano huo.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba (kushoto) akijadiliana jambo na na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano ya Umma), Steven Wassira wakati wa mkutano huo.

Katibu Mkuu CCM Taifa (katikati) akiwa ameongozana na Naibu katibu Mkuu Mh:Mwigulu Nchemba na Mbunge wa singida Mjini mh:Mo Dewji wakati wakutembelea Ujenzi wa Hospitali Kubwa ya Kisasa Singida Mjini.Hospitali itakayokuwa ni tegemeo kwa Mikoa yote ya kanda ya kati
Moja ya Majengo ya Hospitali Kubwa na Mpya iliyojengwa kwa Nguvu za Mkuu wa Mkoa wa Singida.


Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Singida, alipotembelea kituo cha usambazaji maji Singida Mjini

=================================================================================


WAKATI huo huo, CCM pia kimefanya mkutano mkubwa Nungwi, Unguja. Mkutano uliongozwa na Makamu wa Pili wa Rais Wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi

Alichokiongea na na Mzindakae wakiwa Singida


----------------------------------------------
 
Last edited by a moderator:

Ally Kanah

JF-Expert Member
Jun 7, 2011
1,480
1,500
Kwa maneno haya naona Nape anazidi kuidhalilisha CCM na sio kuijenga kama anavyoona yeye.

Kimbia Ufipa ukachukue chako maana umewashika CCM pabaya sana leo
 
Last edited by a moderator:

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Mheshimiwa Mwenyekiti;
Rasimu ya Katiba ni kitabu kikubwa kilichosheheni mambo mengi. Kina kurasa 106, sura 17 na ibara 271. Wajumbe wa Bunge hili mnatakiwa kusoma na kuelewa vizuri kila kilichoandikwa ili muweze kufanya uamuzi ulio sahihi. Mnawajibika kuchambua kwa kina na umakini mkubwa kila kilichomo, sura kwa sura, ibara kwa ibara, sentensi kwa sentensi na hata neno kwa neno. Hamna budi kujiridhisha kuhusu uandishi wa vifungu vya Rasimu ya Katiba na kufaa kwa dhana mbalimbali zilizoingizwa na kujengeka katika Rasimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti;
Kile ambacho Wajumbe mtaona kinastahili kuboreshwa au kurekebishwa au kufutwa msisite kufanya hivyo ili Watanzania wapate Katiba iliyo bora. Msipofanya hivyo kuna hatari ya kupata Katiba ambayo ni ngumu kuitekeleza. Aidha, tunaweza kuwa na Katiba ambayo itanung'unikiwa na watu wengi na kusababisha madai ya kutaka ifanyiwe marekebisho muda mfupi baada ya kupitishwa. Bunge hili linao wajibu maalum wa kuzuia balaa hilo lisitokee katika nchi yetu. Ngazi mbalimbali zilizowekwa katika mchakato huu ni kama chujio la kuepusha hali hiyo isitokee. Kile ambacho hakikuonekana katika hatua moja kitaonekana katika hatua inayofuata na kurekebishwa. Nawaomba fursa mliyonayo muitumie vizuri-RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE, 21 MACHI, 2014, DODOMA

Mwl. Nyerere alijenga hoja ambayo Rais Kikwete ameichambua na kuiweka kuwa ni msingi wa hotuba yake katika Bunge la Katiba kwa kuwataka wabunge wa Bunge Maalum kuiboresha au kuirekebish au kufuta kipengele chochote ili wananchi wapate Katiba Bora.

Mwl. Nyerere alisema,
Tanganyika na Zanzibar zilipoamua kuungana na kuwa Nchi Moja, tungeweza kufuata mmojawapo wa mifumo hiyo ya kawaida. Lakini tulishindwa kufanya hivyo kwa sababu ya udogo wa Zanzibar na ukubwa wa Tanganyika. Zanzibar ilikuwa na watu laki tatu (300,000) na Tanganyika watu milioni kumi na mbili (12,000,000). Muungano wa Serikali Moja ungefanya ionekane kama Tanganyika imeimeza Zanzibar. Tulikuwa tunapigania Uhuru na Umoja wa Afrika; hatukutaka tutuhumiwe hata kwa makosa, kwamba tunaanzisha ubeberu mpya!

Kwa hiyo mimi nilipinga mfumo wa Serikali Moja. Shirikisho la Serikali Tatu lingekuwa ni gharama kubwa mno kwa Tanganyika. Zanzibar ingeendesha Serikali yake na kuchangia gharama za kuendesha Serikali ya Shirikisho; na Tanganyika ingefanya vivyo hivyo. Lakini ni dhahiri kwamba mchango wa Tanganyika ndio hasa ungeendesha SerikaIi ya Shirikisho. Kwa hiyo Tanganyika ingeendesha Serikali yake ya watu 12, 000, 000 na pia ndiyo ingetoa sehemu kubwa ya kuendesha Serikali ya Shirikisho la watu 12,300,000.

Ni Watu wanaofikiri kwa ndimi zao wanaodhani kuwa gharama ya Serikali yoyote kati ya hizo ingekuwa ndogo. Gharama ya Serikali ya Tanganyika isingekuwa ndogo, (waulizeni Wazanzibari), na wala ya Serikali ya Shirikisho isingekuwa ndogo. Hata bila ya gharama za mambo yasiyo ya Shirikisho. Na gharama zote hizo kwa kweli zingebebwa na Tanganyika.

Kwa hivyo ilitupasa tujiulize kwa nini tunataka kuibebesha Tanganyika gharama zote hizo; na hasa kwa nini tunataka Serikali ya Tanganyika? Hivi tuna hofu ya kwamba Tanganyika, bila kuwa na SerikaIi yake, itaonekana kuwa imemezwa na Zanzibar? Hofu yetu ni kwamba tukiwa na Serikali Moja Tanganyika itaonekana kuwa imeimeza Zanzibar. Basi na tutafute mfumo ambao utaiondolea Zanzibar hofu hii ya kumezwa, bila kuibebesha Tanganyika mzigo wa kuendesha Serikalli mbili zenye uzito unaolingana.

Hivyo ndivyo tulivyofanya, na hiyo ndiyo asili ya muundo wa Muungano wa serikali mbili. Badala ya kutungua mfumo uliopo kama wapumbavu, tulitazamia hali halisi yetu ilivyokuwa, na tukabuni mfumo uliotufaa zaidi-Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania-Mwl. Nyere
 

Mhabarishaji

JF-Expert Member
Oct 5, 2010
1,005
2,000
Maandamano ya CCM na mapikipiki, ruksa kila mahali. Kwa Wapinzani, Intelijensia huonyesha matatizo, hivyo ni mwiko. Maandamano kukubalika, ni mpaka mapambano makali. Hivi CCM ina hati-miliki ya nchi hii?????? Hivi nchi hii bado ni ya Chama kimoja???? Naendelea kutafakari!!!!!!
 

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Maandamano ya CCM na mapikipiki, ruksa kila mahali. Kwa Wapinzani, Intelijensia huonyesha matatizo, hivyo ni mwiko. Maandamano kukubalika, ni mpaka mapambano makali. Hivi CCM ina hati-miliki ya nchi hii?????? Hivi nchi hii bado ni ya Chama kimoja???? Naendelea kutafakari!!!!!!
Ndugu, nani amekuambia haya ni maandamano.

Msafara na maandamano ni vitu viwili tofauti.

Huu ni msafara wa wananchi na viongozi wao wakielekea kwenye uwanja wa mkutano. Ulitaka wapae angani mpaka kwenye mkutano?.
 

kirikuu10

JF-Expert Member
May 4, 2014
249
0
Ndugu, nani amekuambia haya ni maandamano.

Msafara na maandamano ni vitu viwili tofauti.

Huu ni msafara wa wananchi na viongozi wao wakielekea kwenye uwanja wa mkutano. Ulitaka wapae angani mpaka kwenye mkutano?.

Kweli wewe ni ccm maana hujui hata kujenga hoja msafara na maandamano ninini?
 

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Kweli wewe ni ccm maana hujui hata kujenga hoja msafara na maandamano ninini?
Ndugu, Inawezekana mimi nikawa sifahamu kujenga hoja lakini hiyo haindoi umaana wa maneno Msafara na Maandamano.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts while the stupid ones are full of confidence- Bertrand Russell
 

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Frankly speaking, CCM is the only ACTIVE political party in Tanzania and still the peoples' CHOICE.
The writing is on the wall of CHADEMA.
Mr Mbowe admits that his party is going through difficult times and has critical issues to deal with. "There are a lot of behind-the-scenes efforts to destroy Chadema," he adds. "We are undergoing very critical moments in our political existence. We are not surprised by this because we did not expect CCM to help us grow but to kill us."

But CCM Secretary General Abdulrahman Kinana, who is leading the offensive against Chadema, going from region to region to revitalise his party, dismissed Mr Mbowe's version of the story. Chadema was simply not strategic and relied on sporadic political events to push their case--and that was why the party could not sustain a national agenda, he said.

Mr Kinana added: "It (Chadema) is an event-oriented party. They are always jumping from one agenda to another or reacting to sporadic events to keep their party afloat. They have no national agenda and that picture is becoming clearer to Tanzanians today more than ever before. Today their agenda is the new constitution. Now everything is around Katiba. Their plans are not long-term, objective and sustainable. Whatever they take on is short term and sporadic." Blaming CCM and its government for the party's troubles, the CCM secretary-general said, was escapism and an attempt to hide their weaknesses in managing internal politics.

Chadema changes tack amid CCM onslaught - National - thecitizen.co.tz

 

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,021
2,000
Ndugu, CCM ijiandae kisaikologia kufanya nini?. Fafanua vizuri!.

Mkuu mbona mkutano wa Zanzibar HAUONYESHI hata picha moja ya ugawaji wa PILAU na HARUA?Kwenye mkutano wa Zanzibar kulikuwa na ugawaji wa chakula kwa waliokuwepo!!

Sometimes uwe unatutendea haki hasa kutuletea picha za matukio yote ktk mkutano mmoja sio kuchagua picha zinazokufaa tu!Siasa ni ukweli na uwazi sio bias!
 

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Mkuu mbona mkutano wa Zanzibar HAUONYESHI hata picha moja ya ugawaji wa PILAU na HARUA?Kwenye mkutano wa Zanzibar kulikuwa na ugawaji wa chakula kwa waliokuwepo!!

Sometimes uwe unatutendea haki hasa kutuletea picha za matukio yote ktk mkutano mmoja sio kuchagua picha zinazokufaa tu!Siasa ni ukweli na uwazi sio bias!
Ndugu, wewe unadai kulikuwa na ugawaji wa pilau na harua kwa maana kwamba ulikuwepo kwenye tukio au umeishaona hizo picha. Sasa unataka nikuletee kitu ambacho unadai umeishakiona?.

Mimi nimeleta kitu ambacho kilikuwepo kwenye mkutano, kwa hiyo na wewe unatakiwa ulete kitu ambacho ulikiona.
 

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,727
2,000
Ndugu, wewe unadai kulikuwa na ugawaji wa pilau na harua kwa maana kwamba ulikuwepo kwenye tukio au umeishaona hizo picha. Sasa unataka nikuletee kitu ambacho unadai umeishakiona?.

Mimi nimeleta kitu ambacho kilikuwepo kwenye mkutano, kwa hiyo na wewe unatakiwa ulete kitu ambacho ulikiona. 

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,021
2,000
Ndugu, wewe unadai kulikuwa na ugawaji wa pilau na harua kwa maana kwamba ulikuwepo kwenye tukio au umeishaona hizo picha. Sasa unataka nikuletee kitu ambacho unadai umeishakiona?.

Mimi nimeleta kitu ambacho kilikuwepo kwenye mkutano, kwa hiyo na wewe unatakiwa ulete kitu ambacho ulikiona.

Mkuu unajichanganya sana!Haukuwepo kwenye mkutano wa Zanzibar wewe!!Wewe upo Singida na hizi picha za Zanzibar umeletewa tu!Kwa taarifa yako mkutano wa Zanzibar uliambatana na UGAWAJI wa PILAU ili kuwaleta watu kwenye mkutano!

ALIYEKULETEA PICHA ZA ZANZIBAR MUOMBE PIA AKUONGEZEE PICHA za waliokuja kula ubwabwa!
 

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Akili kama hizi mara nyingi unazipata ndani ya vichwa vya vijana wa BAVICHA. Vijana wa BAVICHA wamepewa kazi ambayo inazidi akili na fikra zao. Hawawezi kupambana na hoja mbadala kwa kujenga hoja. Wanachofanya ni kuleta viroja wakidhani ndiyo hoja mbadala.

Unapoamua kuchafua thread haitofautiani na dikteta anayeziba uhuru wa wananchi kujiamulia mambo yao katika misingi inayokubalika kijamii. CCM iliporidhia mfumo wa uhuru wa habari ilikuwa inafahamu maana na umuhimu wake katika jamii.

Kwa akili zako za kibavicha unadhani kuchafua thread ndiyo kujenga hoja. Dunia itaendelea kukupa darsa.
 

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,535
1,195
Mkuu unajichanganya sana!Haukuwepo kwenye mkutano wa Zanzibar wewe!!Wewe upo Singida na hizi picha za Zanzibar umeletewa tu!Kwa taarifa yako mkutano wa Zanzibar uliambatana na UGAWAJI wa PILAU ili kuwaleta watu kwenye mkutano!

ALIYEKULETEA PICHA ZA ZANZIBAR MUOMBE PIA AKUONGEZEE PICHA za waliokuja kula ubwabwa!
Ndugu, ninakuomba wewe unisaidie hizo picha kwa vile ulikuwepo kwenye mkutano.

Mimi nimeleta kile kilichokuwepo katika mkutano wa CCM, Nungwi, Unguja.
 

nkongu ndasu

JF-Expert Member
Jan 19, 2013
22,524
2,000
Ndugu, nani amekuambia haya ni maandamano.

Msafara na maandamano ni vitu viwili tofauti.

Huu ni msafara wa wananchi na viongozi wao wakielekea kwenye uwanja wa mkutano. Ulitaka wapae angani mpaka kwenye mkutano?.
yaleyale, wakifanya wapinzani ni maandamano na sharti wapigwe mabomu na kukamatwa, wakifanya maccm ni msafara na ruksa! Nchi hii inakoelekea ni kubaya sana! Allah atuepushie balaa hilo..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom