Wananchi kumuondoa Rais Al Bashir wa Sudani kwa aibu Nkamia na wapambe wenzake wamejifunza?

Kasegela

Senior Member
Mar 24, 2019
127
261
Ndugu wanabodi,ni wazi kuwa Sudani chini ya Rais Al Bashir ilikuwa na intelligence kubwa kubaini wasaliti.

Sudani ilikuwa na jeshi imara huku kitengo cha Usalama kikiwa kazini kwa muda wote kulinda maslahi ya Al Bashiri na washirika wake.

Hata hivyo wananchi walipoamua kupinga mauaji yaliyofanywa na vyombo vya dola,kupinga kuongezeka kwa gharama za maisha,kupinga uonevu na uminywaji wa demokrasia si polisi wala jeshi walioweza kuwarudisha nyuma.

Hatimae utawala wa miaka 30 umekomeshwa na nguvu ya umma.

Waliokula na kusaza na kuwakejeli wananchi leo wanajificha kwenye vichaka,karavati na wengine kukutwa wamepanda juu ya miti.

Yaanu Mawaziri waandamizi leo wanaogopa kwenda jela na kuishia kujificha kwenye mutaro ya maji machafu.

Walikuwa ni mashujaa wakitembea na Ving'ora,leo wanatamani maisha ya chinga anaeshinda njaa,nyumba zao wamezikimbia,mipaka imefungwa,Viwanja vya ndege wakionekana wanakamatwa na jeshi hilohilo walilokuwa wanalitumia

Kila jambo lina mwanzo na mwisho.

Ni funzo gani tunalipata sisi Watanzania kutoka Sudan ya Al Bashiri ?

Nkamia na wachafuzi wa amani wengine bado msimamo wenu ni kufanya mikakati ya kuvuruga katiba na kuongeza muda wa Rais kusalia madarakani?

Tunajua lengo lenu halina tofauti na waliomponza Rais Al Bashir,lkn mtambue kuwa mwisho wa kuchezea hisia za wananchi ni mbaya.

Dr.Bashiru aliliona mapema na kutambua madhara yake.

Aliukwepa mtego wa Nkamia ambae nae alitumwa kupima upepo.

Nampongeza Rais Magufuli kwa kukwepa mtego wa wapambe wanaotengeneza mazingira ya kuendelea kujinufaisha kupitia yeye kung'ang'ania madaraka.

Rais mchana kweupe aliamua kuufunga mjadala na kusema atafuata njia ya watangulizi wake,na atakuwa amejijengea heshma kama wanavyoheshimika sasa Wastaafu wetu(Mwinyi,Mkapa na Kikwete)

Bora ustaafu uishi kwa heshima mpaka kifo chako kuliko kung'ang'ania ukatolewa kwa aibu na kuishia Jela kama Al Bashir na wapambe wake.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM ni chama kinachojali demokrasia kuanzia ndani mpaka nje! Haitatokea ndani ya CCM mtu akaongoza zaidi ya miaka kumi.....

Sent using Jamii Forums mobile app
Na tuseme ukweli tu...hakuna chama kibaya na kandamizi kama ccm.
Hiki chama ni kiovu na fidhuli kuliko hata wakoloni wa kiingereza na kijerumani.
Wananchi tukikatae na tukipinge kwa nguvu zote kama walivyofanya wenzetu huko Sudani kwa Albashir
 
Back
Top Bottom