Wananchi kukosa imani na Polisi: CCM yaagiza Jeshi la Polisi lichunguzwe

IGP Sirro ndiye kilaza mkubwa hajui hata PGO inamtaka afanye nini kulisimamia jeshi la polisi!
 
Changa la macho.Huwezi kuukata mkono unaokulisha.Period.CCM na polisi ni kitu kimoja.CCM anapanga,polisi anatekeleza.
 

CCM yaagiza Jeshi la Polisi lichunguzwe, uchunguzi uanzie polisi mkoa wa manyara, babati mkoani.​

Polisi pale ni wapigaji. Kuna kundi linajiita inspectors ni wezi na hakuna wanachokifanya hapa babati bali ni kuwakosenisha raia wema na seriksali
 
Hakuna uwezekano wa jeshi la polisi kubadilika iwapo ccm itaendelea kukaa madarakani kwa shuruti. Wanachoongea ccm hapo ni Hadaa ya mchana kweupe.
 
Polisi hawazi kupendwa na mwananchi hata siku moja tangu enzi za yesu na kabla ya yesu askari hakuwahi kupendwa kwa kilichopo polisi akitenda majikumu yake ipasavyo tayari mwananchi atamuona ni mtu mbaya,jambo la msingi mwananchi afuate sheria na kutii mamlaka zilizopo hakuna kingine hata jeshi libadilishwe vp sijui lakini kama halitakabiliana na wahalifu itakuwa ni kazi bure.
 
Polisi hawazi kupendwa na mwananchi hata siku moja tangu enzi za yesu na kabla ya yesu askari hakuwahi kupendwa kwa kilichopo polisi akitenda majikumu yake ipasavyo tayari mwananchi atamuona ni mtu mbaya,jambo la msingi mwananchi afuate sheria na kutii mamlaka zilizopo hakuna kingine hata jeshi libadilishwe vp sijui lakini kama halitakabiliana na wahalifu itakuwa ni kazi bure.

Ww lazima utakuwa ni polisi, nyie ndio wenye utetezi wa hivi.
 
Kwenye uchaguzi hao CCM huwatuma polisi kuvuruga uchaguzi kwa mtutu wa bunduki na ndiyo maana polisi wanatesa raiya kwasababu wanajua siri ya ushindi wa CCM ni bunduki na kumwaga damu.

Sitegemei mabadiliko yoyote kwa polisi hapa tunahitaji katiba mpya itakayoondoa mamlaka ya rais ya kuteua mkuu wa polisi.
 
Polisi ni kichaka majambazi .wezi .vibaka yaani natapika nikimwona polisi
Yaani katika ubishani wa kurushiana Risasi kati ya Polisi na Majambazi ,Polisi wamefanikiwa kuwauwa Jambazi wawili kati ya wanne na wengine wamekimbia.

Hapa serikali iporuhusu hii kauli ndipo Polisi iliendelea kuharibika kwani ukijakuwauliza Polisi baada zoezi kupambana kuisha je walichokiiba kiko wapi jibu ni kuwa waliokimbia ndo wametokomea na mzigo.

Ndo maana wale Majambazi wakongwe waliamua kuacha hii kazi na kufanya Mambo mengine kwani waliletewa kazi kumbe ni za kwenda kutoana sadaka na wenyekazi waondoke na mzigo.

Hanaga wizi wowote unafanyika wasijue ni wapi na ni nani amelifanya hilo tukio.

Huko uswahili kuna ule wizi wa ukataji wa nyavu za madirisha wenyewe wanajuana kwa aina ya ukataji.

Kwa hiyo hakuna jipya
 
CCM yenyewe wananchi wameichoka, vivyo hivyo kwa hao ndugu zao Polisi!!!

Ushauri:

Wakati CCM na Polisi wakishughulikiana, ni lazima mkakati uwekwe wa kuiondoa CCM madarakani...hii itasaidia kuweza kulifumua na kuunda upya Jeshi la Polisi lenye weledi.

Polisi haiwezi kuwa na weledi CCM ikiwa madarakani,.. NEVER.

CCM iondoshwe KWANZA.

KATIBA MPYA itaweza kutuonyesha njia.
 
Back
Top Bottom