Wananchi Kilwa watakiwa kutozomea watalii na kuwaita Corona

yu KIMARO

New Member
Apr 30, 2019
4
5
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi Christopher Ngubiagai amekemea vikali na kuahidi kuwachulia hatua kali, baadhi ya wananchi wa wilaya hiyo kwa kuwazomea watalii wa kizungu na kuwaita majina ya corona baada ya watalii hao kutembelea wilaya hiyo.

Ngubiagai ameyasema hayo alipokuwa akitoa maelekezo juu ya ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona ofisini kwake huku akiagiza taasisi zote binafsi na za umma wilayani humo kutengeneza sehemu ya kunawia mikono watu mbalimbali pindi waingiapo ofisi zao.

Ngubiagai ameongeza kwa kusema licha ya ustarabu wa wananchi wa Kilwa kusalimiana kwa kupeana mikono nivvyema kipindi hiki waepuke kusalimiana kwa kupeana mikono.

Mpaka sasa mataifa mataifa 180 yameathirika kutokana na virusi hivyo huku watu 246,594 wakiathirika na virus hivyo huku watu 10,050 wakipoteza maisha na 88,486 wakipona virusi hiyo.

Ngubiagai.jpg

Mkuu wa wilaya Kilwa, Christopher Ngubiagai

Chanzo: Mashujaa FM
 
Ndio shida ya kuwa na nchi yenye watu wajinga wajinga!

Kwahiyo wamezomea ili iweje kwa mfano?

Wakajipanga mstari kabisa ili waanze zomea zomea au ilikuwa kuwaje?
 
Ndio shida ya kuwa na nchi yenye watu wajinga wajinga!

Kwahiyo wamezomea ili iweje kwa mfano?

Wakajipanga mstari kabisa ili waanze zomea zomea au ilikuwa kuwaje?
Hiyi hali hata jana nimeikuta mbagala rangi tatu!! Kuna wazungu wawili walikuwa wanapita, wa machinga ndio wakaanza kuwazomea, na kuwatukana kuwa ndio wametuletea corona, "NYIE KENGE SANA NDIO MNATAKA KUTUUA, KWA KUTULETEA CORONA, SASA HAPA HAFI MTU" UKIMWI MMETUSHINDWA MMEKUJA KI VINGINE"
 
Hawa wazungu wakiwa kule ulaya wakimuona mtu mwenye ngozi nyeusi wanaenda kumshika ile rangi kwa kumkejeli kwamba labda inafutika pia wakati mwengine huwaita watu weusi monkey, lakini haitoahi huwa wana msemo wanasema kwamba “black people are uncivilized” yan watu weusi ni watu wasiostaarabika.

Saa nyengine utamkuta mzungu anaimba “sun shine... sun shine... ujue hapo kuna muafrika ama watu wa ngoz nyeusi karibu,
 
Msiwachukukie hatua kali sana jamani mtawaumiza ndugu zenu hao ni wa tz tu

Hata kama wamekosea kuwazomea hao wageni, lakini wapewe elimu kwanza. Wao wameambiwa ulaya ugonjwa umeenea sana, sasa labda wamepata hasira. Waelimishwe na kukemewa lakini msiwachukulie hatua kali sana wabongo hao maskini.


amekemea vikali na kuahidi kuwachulia hatua kali,
 
Hiyi hali hata jana nimeikuta mbagala rangi tatu!! Kuna wazungu wawili walikuwa wanapita, wa machinga ndio wakaanza kuwazomea, na kuwatukana kuwa ndio wametuletea corona, "NYIE KENGE SANA NDIO MNATAKA KUTUUA, KWA KUTULETEA CORONA, SASA HAPA HAFI MTU" UKIMWI MMETUSHINDWA MMEKUJA KI VINGINE"
Tuna watu wajinga sana!
 
Back
Top Bottom