Wananchi Kigoma wavunja vibanda vya wakimbizi vilivyojengwa na UNHCR

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
kambi.jpg



Wananchi wa kijiji cha Kagunga wilayani Kigoma,wamevamia na kuvunja vibanda vya muda vilivyojengwa na shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa ajili ya kuwapokea na kuwahifadhi kwa muda wakimbizi toka Burundi waliokuwa wakipokelewa katika kijiji hicho kutokana na vijana kutokuwa na eneo la michezo na shughuli nyingine za kijamii.

Vibanda hivyo vilivunjwa baada ya mkutano wa kijiji kuridhia ili kutoa fursa kwa uwanja huo kuwa wazi kwa shughuli za kijamii ambapo Mwenyekiti wa serikali ya kijiji Hassan Mikidadi aliwaongoza wananchi kufikia maamuzi hayo ambapo wananchi walibomoa vibanda hivyo ambavyo vimekuwepo katika eneo hilo kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kigoma Saveli Maketta amesema hatua iliyochukuliwa na wananchi hao wakiongozwa na Mwenyekiti wao ni kinyume cha sheria na kwamba suala hilo lingeweza kumalizwa kwa kuwataka wenye vibanda kuondoa mali na vibanda hivyo, ameagiza watu waliohusika ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti kukamatwa ili waweze kujibu tuhuma za uharibufu wa mali.

Chanzo: ITV
 
Back
Top Bottom