Wananchi jimbo la Kalenga mkoani Iringa wadai wametelekezwa na Mbunge wao

Jan 29, 2014
36
125
WALIA KUTELEKEZWA NA MBUNGE WAO
________________________________________
Wanachi wa jimbo la Kalenga Mkoani Iringa wamelalamikia kitendo cha mbunge wao Mh Mgimwa(CCM) kutoonekana jimboni wala kutojihusisha na kusikiliza wala kutatua kero zao, huku wakidai kuwa hata Bungeni hawamsikii akichangia

Wakimfikishia kero hizo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wamesema "Toka achaguliwe hajawahi kututembelea wala kusikiliza kero zetu, hata simu hapokei na wala Katibu wake haonekani, hata tulipo mchagua hakuja kutushukuru, pengine tulikosea kumchagua mtu aliyekua anaishi nje ya nchi."

Naye mmoja wa madiwani wa CCM amesema "Ni kweli Mbunge haoneshi ushirikiano hata ktk ujenzi wa miradi mbalimbali huwa tunafanya wenyewe pamoja na Wananchi na wakati mwingine Mimi Kama diwani nalazimika kwenda TAMISEMI kuomba msaada kwa sababu Mbunge hata simu hapokei na hata pesa za mfuko wa jimbo huwa tunagawana wenyewe madiwani bila ya yeye kuwepo wala katibu wake"

FB_IMG_1550173638721.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom