Wananchi hawa nao lugha yao iwe ya pili ya taifa

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
19,273
23,086
Wananchi hawa tunaishi nao ila tumewabagua kwa kuwaita "viziwi, bubu"! Kwenye maisha yetu ya kila siku huwa hatuwashirikishi kwenye maongezi, tunawabagua japo tumezaliwa nao tumbo moja!

Umefika wakati sasa tuwaite mezani tuongee nao kwa kutumia lugha moja bila kuwepo mtu wa kati, ili kufanikisha hili serikali ianzishe somo la lugha ya alama shuleni ambapo nalo litapewa uzito kama kiswahili na kiingereza. Wananchi wote tukijua lugha ya alama tutakuwa tumewapa furaha ambayo wameikosa tangu wazaliwe kwa kuwa tunawabagua bila kosa.
 
Wazo lako zuri, lakini itabidi Wizara ya Elimu iweke iyo option kuanzia shule ya msingi kama somo, na pia kuna uwezekano tukaanza na kusoma "nukta" kwa ajili ya walemavu wa kuona.
 
Kwenye hoja yangu nimesema serikali iweke somo la lugha hiyo kama ilivyo kwenye kiswahili na kiingereza.
 
Upo sahii mkuu,Mimi mara nyingi huwa nataka kujifunza Lugha ya alama ila sijui nianzie wapi,siku hizi watu wenye changamoto hizi wengi sana, serikali ifanye jambo kwa ndugu zetu Hawa,Kila shule iwe na mwalimu ambae anajua Lugha hiyo,mwanafunzi atakae penda ajifunze..

Kuna Binti(double entendre) ni kiziwi,huwa nawasiliana nae kwa meseji tu,..Rafiki yangu Mzuri
 
Bahati mbaya Mods hawajapenda wameihamishia kwenye burudani hivyo umekosa mvuto na ushiriki.
 
Msg wanajua kuandika?

Back
Top Bottom