Wananchi Geita: Mkuu wa Wilaya anavuta Millioni 42 kwa Mwezi toka Kampuni ya Madini GGM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wananchi Geita: Mkuu wa Wilaya anavuta Millioni 42 kwa Mwezi toka Kampuni ya Madini GGM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DSN, Aug 8, 2011.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Wananchi ambao ni wakazi wa Wilaya ya Geita Wamelalamika juu ya matendo mabaya wanayotendewa na walinzi wa kampuni ya GEITA GOLD MINE [GGM] ya kuwaumisha mbwa wananchi wanaokwenda kuokota mabaki ya mawe ya mchanga wa dhahabu unaotupwa baada ya uchambuzi wa kuchotwa kwa dhahabu.

  Kingine kinachoendeshwa na walinzi hao ni kuwavua nguo wanaume wanaokamatwa na kuwashikisha nyeti zao kama polisi wanavyowafunga watuhumiwa mashati ili kuweka ulinzi haswa wanapokuwa hawana pingu.Kwa kiswahili cha kisasa ni mtungo [kuunganisha] lakini kupitia kila moja kushika nyeti ya mmoja uku mwingine naye akimshika mwingine na kutengeneza mstari.

  Kingine kibaya cha matendo hayo ni kuwabaka wakina dada wanaokamatwa kwenye maeneo hayo.Kwa Matendo hayo ambayo yamesemwa na wananchi hao huku wakionyesha vidonda vya kuumwa na mbwa [taarifa ya habari ITV].Walipofikisha taarifa juu ya matendo hayo ya KINYAMA yanayofanywa na Walinzi hao wa GGM,Viongozi wa Serikali walipofikishia malalamiko hayo hakuna chochote walichopata kama msaada kwa matendo hayo ya kinyama.

  Wananchi walifanya uchunguzi kujua mbona malalamiko yao juu ya matendo ya kampuni hiyo ya GEITA GOLD MINE [GGM] hayana majibu kuna ni?Utafiti [Uchunguzi] wakagundua kuwepo taarifa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita ambae ndiye msimamizi na mwakilishi wa Rais wa jamhuri ya Muungano kwa Wananchi wa Geita anachukua Fedha kutoka kampuni hiyo kiasi cha shilingi Millioni 42 kwa Mwezi.

  Hakika kwa wanaojua watwambie madai ya wananchi hao ambao kwa waliongalia taarifa ya habari ni kweli baadhi ya watu wanamakovu ya vidondo baadhi vikiwa bado vibichi.

  Mtujuze wale wanaojua habari zaa Mgodi wa Geita [GGM] na Mahusiano yake na Mkuu wa Wilaya huyo.
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Aug 8, 2011
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Huyo mzee shelutete ambae amewekwa na mafisadi pale kuhakikisha GGM wako salama anapenda sana rushwa sana sana si ndie anaekula hata pesa za yatima toka mgodini??nashangaa kwa nini hajastaafu muda wake ulishapita!ila hata yeye amuogope Mungu wake amezidi kupenda pesa jamani mzee unaenda kanisani kufanya nini kama hubadiliki kimaadili?
   
 3. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #3
  Aug 8, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  niliona jana ITV .. inasikitisha sana! Hii ni serikali ya mbwa!mbwa kuanzia ikulu mpaka huku chini!
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Aug 8, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hapo ndio utajuwa dini ya haki ni ipi.
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Aug 8, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Na hao wananchi wanafata nini eneo la mgodi? Na wanajua fika kuwa huko kuna walinzi na hawaruhusiwi kusogea?
   
 6. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #6
  Aug 8, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hii nchi ina matatizo mengi yanayohitaji ufumbuzi lakini cha kushangaza ni kuwa hayatatuliwi ipasavyo! Swali langu ni kuwa tufanyeje ili kukomesha haya matatizo?
   
 7. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Maisha yalivyotupindisha ni haki yao kwenda kwa kuwa shamba la bibi yao lilishauzwa watalima wapi?
   
 8. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #8
  Aug 8, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Twin Crap
   
 9. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  dini ya haki ni ipi ? hebu tujuze! Labda kama haina fisadi hata mmoja nasi tuifuate!
   
 10. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #10
  Aug 8, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Huwa kila nkipita Geita na kufikiria juu ya utajiri ulioko ndani na ardhi na jinsi unavyobebwa na wachanche nikaangalia umasikini uliokithiri pale sina hamu na hali hii!
   
 11. m

  mwananchit Senior Member

  #11
  Aug 8, 2011
  Joined: Oct 13, 2008
  Messages: 145
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Utafiti [Uchunguzi] wakagundua kuwepo taarifa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita ambae ndiye msimamizi na mwakilishi wa Rais wa jamhuri ya Muungano kwa Wananchi wa Geita anachukua Fedha kutoka kampuni hiyo kiasi cha shilingi Millioni 42 kwa Mwezi.

  HILO LINAWEZEKANA MAANA SASA HIVI GGM WANAJICHIMBIA DHAHABU POPOTE WANAPOIONA HATA NJE YA MAENEO RASMI YA MGODI UTADHANI HAMNA UONGOZI PALE WILAYANI!
   
 12. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #12
  Aug 8, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kwani mwekezaji alifuata nini pale kama sio dhahabu yao? serikali ilipaswa kuhakikisha wenyeji waliohamishwa wamelipwa vizuri au kungewekwa utaratibu wa kuwapatia hisa leo usingesikia matatizo hayo
   
 13. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #13
  Aug 8, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nasikia hata chai yenyewe hupata huko ndani ya huo mgodi, jamani huko si kujidhalilisha, jama katika historia, alikaa miezi kadhaa hivi akajenga na nyumba, sasa sijui mshahara wa mkuu wa wilaya unaruhusu kujenga nyumba ndani ya miezi kadhaa. Hii ni aibu sana
   
 14. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #14
  Aug 8, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Jamani Geita pameisha hadhi, kwa sasa ni ukame mbaya sana, kuna vumbi mpaka nasema kweli cha mjinga huliwa bila utaratibu, yaani mkoa ni vumbi, hakun huduma yoyote, maji ndo kitendawili, halafu hii sera ya kuanzisha mikoa mbona imekaa kisiasa sana, hivi unaweza kuanziaha kitu bila kufanya setup ya miundo mbinu, hii hatari sana.
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  Aug 8, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  kila nikija jukwaa la siasa lazima nipate hasira aaAAAAAARRRGHHH
   
 16. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #16
  Aug 8, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Dini ya haki my prolonged squeako farto!!
   
 17. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #17
  Aug 8, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Din ya haki ni moyo wako
   
 18. M

  Mzee Madoshi Senior Member

  #18
  Aug 8, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kutokana na habari hii, wao ndio marais wa maeneo hayo
  [HR][/HR]Henjewele na Tarime, Shelutete na Geita[/h]By Mwandishi Maalum

  Na Mwandishi Maalum - Imechapwa 27 July 2011

  WIKI iliyopita nilifuatana na kundi la viongozi wa dini kutoka ndani na nje ya Tanzania, kutembelea maeneo ya migodi ya dhahabu huko Tarime, mkoani Mara na Geita mkoani Mwanza. Ndani ya kundi hilo walikuwamo wanaharakati wa haki za binadamu, waandishi wa habari na viongozi wa dini.
  Kutoka nje ya nchi, walikuwapo wawakilishi wa nchi za Canada, Afrika Kusini, Zambia, Botswana, Msumbiji na Norway. Niliyoyaona kwa macho yangu na kuyasikia kwa njia ya simulizi mbalimbali za wenyeji, yananifanya niandike makala hii nikiwaangalia wakuu wa wilaya hizo mbili.
  Huko Tarime tulipata nafasi ya kuonana na Mkuu wa Wilaya hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Henjewele. Nitamkumbuka daima ofisa huyu wa serikali kwa mambo mawili makubwa. Kwanza kwa tabia yake ya kukosa hisia na heshima kwa watu wa Tarime, na pili, kwa fikra zake zinazoweza kutafsiriwa kuwa ni mhaini japo yeye hajajifahamu. Nitaeleza.

  Mkuu wa Wilaya anadai watu wa Tarime hawatawaliki. Anasema mbele ya wageni, wakiwamo maaskofu kuwa watu wa Tarime si wastaarabu hata kidogo, na ndiyo maana wanatawaliwa kipolisi polisi.
  Akautisha ujumbe wetu kuwa tusiende Nyamongo na kama tutakaidi maelekezo yake, yeye hayuko tayari kuwajibika kwa ajili ya ukaidi wetu maana anawajua vizuri watu wa huko walivyo na vurugu.

  Akaendelea kutoa maelezo kuwa, umefanyika utafiti juu ya watu wa Tarime na kubaini kuwa watu wa Tarime si Watanzania, wala si Wakenya, bali ni “Watarime”. Ndipo zikaingia fikra za kihaini pale alipodai kuwa Tarime ni taifa pekee na huru nje ya himaya ya Tanzania, na yeye ndiye rais wa taifa hilo.
  Kwa mteule wa rais wa nchi, aliyetumwa kuongoza eneo kisha akalitangaza kuwa ni taifa maalumu na watu wake ni watu maalumu, ni fikra za hatari sana. Yawezekana aliyasema haya kwa kejeli na utani uliozidi mipaka, lakini maneno haya kusemwa mbele ya wageni wa kutoka nje ya nchi, tafsiri yake ilikuwa mbaya sana.
  Sisi watanzania tuliokuwa ndani ya msafara huo tulipata taabu sana kujibu maswali ya wageni kuhusu matamshi ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mheshimiwa Henjewele.

  Baada ya maelekezo yake hayo na zuio lake la kututaka tusiende maeneo ya mgodi, tuliamua kwenda kwa ridhaa yetu wenyewe. Tulipofika kule, tulipokelewa vizuri na wananchi wa huko, na bila kuwauliza lolote juu ya mkuu wa wilaya, walianza kutueleza jinsi mkuu huyo wa wilaya anavyotumikia wawekezaji wa mgodi.

  Walikwenda mbali na kusema watoto wa mkuu wa wilaya wanalipiwa karo na wawekezaji, na kuwa posho anayopata kutoka mgodini ni kubwa mara kumi kuliko mshahara wa serikali. Yawezekana sana huu ni uwongo lakini ambao umechochewa sana na tabia ya mkuu wa wilaya ya kuwatelekeza wananchi wake na kuwatumikia wawekezaji.

  Wananchi walitupokea kwa amani na walitulia wakati wote wakieleza kero zao mbalimbali na madhara ya kiafya, kiuchumi na kijamii wanayoyapata
  kutokana na uchimbaji wa dhahabu. Wageni wetu walishangaa kukuta wananchi wale ni wakweli, wanaoongea kwa vielelezo na ustaarabu mkubwa. Baadhi yao waliongea kwa jazba zinazotokana na ukandamizaji wa muda mrefu kutoka kwa wawekezaji na watendaji wa serikali.
  Huko Geita nako tulikumbana na kigingi cha kwanza baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo aitwaye Shelutete alipokataa kukutana na ujumbe wetu kwa madai kuwa mkuu wa mkoa alikuwa anafika wilayani humo.
  Mwenye hekima angedhani mkuu wa wilaya angetumia fursa hiyo kukutana na ugeni huu mkubwa akiwa na mkuu wake wa mkoa, lakini haikutokea hivyo.

  Umbali usiozidi kilomita moja kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya, kuna kambi ya wakimbizi wa ndani ambayo imekuwa hapo kwa takribani miaka mitatu sasa. Watu hao ambao sasa wamebakia familia ishirini, wanaishi kwenye mahema yaliyotolewa na makanisa na misikiti ili kuwasitiri baada ya kudhulumiwa ardhi yao na wawekezaji katika migodi.

  Tulipofika katika kambi hiyo inayosikitisha, tuliwaona watoto wadogo waliozaliwa ndani ya kambi hiyo, akina mama wajawazito, wazee na wagonjwa. Mateso wanayoyapata watu hawa yaliwafanya baadhi ya wageni kutoa machozi na kuuliza ikiwa kuna serikali katika eneo hilo.
  Mkuu wa wilaya ya Geita anadaiwa kukaa sana wilayani humo. Hata baadhi ya wakuu wa mikoa waliowahi kukaa mkoa wa Mwanza wanashangaa kwa nini mtu huyu ameachwa na kuota mizizi katika wilaya hii.
  Fikra kwamba anatumiwa na wakubwa zinaibuka haraka, na sasa hata fikra za kutumiwa na wawekezaji zimezagaa mji mzima wa Geita. Utendaji wa serikali hauendeshwi na fikra za barabarani, lakini mtendaji wa serikali asiyeshtushwa na hali ya mateso ya watu wake, anasababisha yeye mwenyewe kufikiriwa na watu wa barabarani kuwa anawatumikia wawekezaji.

  Wakimbizi hao walisimulia kwa kirefu historia ya kuwa kwao pale, na kuwa hata mkuu wa wilaya hataki hata kuwasikiliza kwa sababu ni yeye aliyegoma kutekeleza amri ya mahakama ya rufaa iliyowapa haki ya kukaa katika ardhi yao mpaka hapo kesi ya msingi itakapomalizika kusikilizwa.
  Taarifa hiyo iliwashtua sana wageni na viongozi wa dini waliotaka kujua ikiwa wakuu wa wilaya wana mamlaka kuliko mahakama ya rufaa! Jibu lilipatikana kuwa wawekezaji ndio wana nguvu kuliko mahakama, na mkuu wa wilaya ni mtumishi wa wawekezaji wenye nguvu nyingi.
  Hali hii pia ilidhihirishwa na mkimbizi mmoja mwanaume aliyesimama mbele ya wageni na kuomba kuwa mkimbizi katika nchi zao ili iwe rahisi kupata matibabu kwa sababu amekuwa anaumwa muda mrefu na akienda hospitali hapati huduma yoyote.

  Inakatisha tamaa sana kuona raia wa nchi wanakuwa wakimbizi katika nchi yao na viongozi wa serikali wanageuka watumishi wa wageni. Hali iliyo huko Geita na Tarime inakatisha tamaa sana na kuzua fikra za ikiwa kweli tunahitaji uwekezaji huu. Muda si mrefu, maofisa wa serikali na hata wa vyombo vya dola, wataanza hata kutoa siri za nchi kwa wawekezaji, na hatimaye kuhujumu usalama wa nchi yetu. Hatukujua kama tunawekeza hata usalama na roho za wananchi wetu.

  Source URL:
  Henjewele na Tarime, Shelutete na Geita | Gazeti la MwanaHalisi


  [​IMG]
   
 19. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #19
  Aug 8, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Poleni sana lakini siwashawishi kusogelea eneo la mgodi, ni hatari sana
   
 20. M

  MINAKI Member

  #20
  Aug 8, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 41
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Sisi watanzania tunatakiwa kuwalaumu viongozi wa serikali waliokubali kusaini mikataba ambayo inawaumiza watanzania! Nchi hii inaongozwa na sheria na kama wawekezaji walitiliana saini na wakuu wa nchi kwa makubaliano flaniflani katika hii mikataba,tusiwalaumu wawekezaji! Tunatakiwa kuomba hiyo mikataba kutoka serikalini ili tuisome na kujua kilichoandikwa humo ndo tuanze kujiuliza nini cha kufanya! Watanzania wenzangu,kama mkipata hii mikataba na kuisoma mtagundua ni kwa jinsi sisi wenyewe ni wa kulaumiwa na si wawekezaji kama wengi wetu tunavyoamini! Naomba kuwakilisha!
   
Loading...