Wananchi Bukombe waomba Rais Magufuli aongezewe muda wa kukaa madarakani

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Screenshot from 2017-06-20 08-28-10.png

Wananchi wa vijiji vya Bulangwa na Katente mkoani Geita,wameliomba Bunge la Tanzania kufanya marekebisho ya muda wa ukomo wa urais kutoka miaka kumi ya sasa hadi miaka ishirini ili kumuwezesha Rais Dk.John Pombe Magufuli kuendelea kubakia madarakani.

Wananchi hao wametoa ushauri huo katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na mbunge wa jimbo la bukombe mh. Dotto biteko kwa ajili ya kumpongeza Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa namna alisimamia sekta ya madini,mkutano ambao umehudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Mh.Costantine Kanyasu.

Akiwahutubia wananchi,Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Mwenyekiti wa kamati ya Nishati na Madini Mh. Dotto Biteko,amesema kazi ya kupigania rasilimali za taifa inayofanywa na Rais Dk. John Pombe Magufuli si ya lelemama,huku Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Mh. Kanyasu akisema serikali ya awamu ya tano haiwachukii wawekezaji, bali inawachukia waporaji wa raslimali za nchi.

Ripoti ya kamati ya pili ya mchanga wa madini wa Makinikia,iliyowasilishwa Juni 12 mwaka huu kwa Rais Magufuli na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Prof.Nehemiah Ossoro ilibaini taifa kupoteza shilingi Trilioni 252 kupitia usafirishaji wa mchanga wa madini ya makinikia nje ya nchi kuanzia mwaka 1998 hadi kufikia mwaka huu,huku ikiwahusisha baadhi ya mawaziri wa zamani wa nishati na madini waliohusika kuingia mikataba mibovu iliyoisababishia serikali hasara.
 
Wananchi wa kijiji. Teh teh teh
elimu yao sidhani km inafika darasa la 7.
Hawajui km kubadilisha katiba ni kosa? Watembelee Burundi wakaone. Wananchi km hawa ni mzigo kwa taifa. Ngozi nyeusi ni majanga sana. Mbona wenzetu huu ujinga haupo? Afrika tunasafari ndefu sana.
 
Hao wanaoomba mh.aongezewe muda yawezekana ndiyo wale tulioambiwa na watafiti wa TWAWEZA,matokeo ya utafiti yalibainisha kuwa ccm inakubalika zaidi na watu duni,wasio na akili na waishio vijijini.Hao ndiyo wanaoweza kushangilia mazingaombwe na push-ups.

Ushauri:
Waanzishe jamuhuri ya Geita na kumfanya huyo wanayetamani aongezewe muda awe rais wao wa milele,Ahsante TWAWEZA kwa kutuletea matokeo sahihi ya utafiti juu ya watu wanaoichagua ccm.
 
Kuna ndege iliwahi kuruka Zanzibar ikamwaga vipeperushi kwamba Salmini Amour aongezewe muda, yeye akasema hahusiki. Na JPM hahusiki.
 
Tunajua hizo ndio chokochoko za madictator at a wakina kagame walianza ivi ivo na kusingizia wananchi nawaambieni watazania kuwa jpm ameanza kuandaa mpango yakubafili katiba aje kuongoza mpaka kifo
 
Bongo bahati mbaya kweli Young D ameona mbali kuimba meseji nzito kiasi kile.haya ndio madhara ya kuzaliwa bongo young d salute mdogo wang
 
Wananchi wa kijiji. Teh teh teh
elimu yao sidhani km inafika darasa la 7.
Hawajui km kubadilisha katiba ni kosa? Watembelee Burundi wakaone. Wananchi km hawa ni mzigo kwa taifa. Ngozi nyeusi ni majanga sana. Mbona wenzetu huu ujinga haupo? Afrika tunasafari ndefu sana.
kubadilisha katiba haijawahi kuwa kosa!, kosa ni kujiongezea muda wa kukaa madarakani!...niishie hapo kwanza [HASHTAG]#jikubali[/HASHTAG]
 
Kwa vyovyote hao watakuwa ni magamba ambao hawajawahi kujitambua,wanasema katiba ibadilishwe Ili Magufuli atawale kwa muda mrefu zaidi,watangulizi wake waliomtangulia wangefanya upuuzi wa kubadilisha katiba Ili watawale muda mrefu huyu Magufuli angepataje urais?.
 
Wananza pole pole,siku sio nyingi watasema na katiba itupwe kwasababu inamzuia Rais kutekeleza majukumu yake.
 
UFISADI KATIKA SEKTA YA NISHATI UMEFANYA BEI YA UMEME KUWA GHALI SANA..UMEME UMEKUWA ANASA..UHARIBIFU WA MAZINGIRA UNAZIDI KILA LEO MOJA YA SABABU NI KUNI NA MKAA HATA KWA WALIOUNGANISHIWA UMEME...

TULIHITAJI MABADIRIKO KATIKA NCHI HII,TULIHITAJI KIONGOZI MKUU MWENYE MAAMUZI MAGUMU NA IKIBIDI DIKTETA..KWA UTHUBUTU UNAOENDELEA TUTAKUWA WACHAWI TUSIPOPONGEZA.


PONGEZI ZA DHATI KWA SERIKALI YA CCM,PONGEZI KWA SERIKALI YA AWAMU YA TANO..

PONGEZI ZA DHATI KWA UTHUBUTU WA VITENDO KATIKA KUPAMBANA NA UHARAMIA,UBINAFSI,WIZI NA UFISADI.

HONGERA JEMEDALI MKUU MH.RAIS,BARAZA LA MAWAZIRI,TAASISI ZA UCHUNGUZI NA USALAMA..

MMETHUBUTU,MTAWEZA,MTASHINDA...MSIKATE TAMAA,MTAPINGWA NA KUDHIAKIWA LAKINI MKISIMAMA KTK KULIPIGANIA TAIFA..THAWABU YENU NI KUBWA KWA VIZAZI VILIVYOPO,VIJAVYO NA MBINGUNI.
 
Back
Top Bottom