Wananachi wa Arumeru Mashariki wanaulizia ahadi ya Mbunge wao kushusha bei ya sukari

Wassira amesema wanajenga viwanda vitano vya sukari waambie wasubiri!!

Mkuu anzisha thread hii thread wananchi wanaulizia ahadi ya sukari Arumeru kama bei imeshuka.
 
Mbona visima vinaendelea kujengwa au hao walio kuulizia ni wale wanao kaa Dar akina Sioi...
bado wanasubiri za mbayuwayu:

====

  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
  7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
  15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
  20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
  21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
  22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
  23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
  24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
  25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
  27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
  28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
  29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
  30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
  31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
  32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
  33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
  34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
  35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
  36. Kulinda haki za walemavu - Makete
  37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
  38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
  39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
  41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
  42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
  43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
  44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
  46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
  47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
  48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
  50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
  51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
  52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
  53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
  54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
  55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
  56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
  57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
  58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
  60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
  61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
  62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
  63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
  64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
  65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
  67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
  68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
  69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha

Kumbe wameuliza hilo moja tu la bei ya sukari. vipi hizo 69 ?
 
Wewe kijana mbona unaruka ruka? Nyie si mnasema sio waongo?! vipi tena kujitetea huko?
Sasa mmeshindwa kuteleza ahadi ndogo tu, je tukiwapa nchi nzima si ndo itakuwa kulalamika na kulinganisha mifano ambayo haihusiki!.

Ndugu yangu naomba ukubaliane na mimi tu kwamba mbunge kadanganya ili apate ubunge sawa?
sema basi ndio
Ama kweli, "Mtu Mpumbavu hata ukimtwanga kwenye kinu pamoja na ngano upumbavu wake haumtoki". Kwahiyo kudanganya kwa Mkwerre ni bora kuliko wa Nassari? Hivi Wanaarumeru Mashariki wakishushiwa bei ya sukari ilhali Watz wengine bei inaendelea kupaa, ndio utakuwa umetatua tatizo la Watz? Kipi bora, kushusha bei ya sukari nchini kote au kushusha Arumeru Mashariki tu? Na kama nchi nzima bei haijashuka, wa kumuuliza ni Nassari au Mkwerre na timu yake ya Magamba? Mbona unakuwa kama sio m.p.u.m.b.a.v.u vile???????????
 
Wanabodi.Habari tulizozipata kutoka kwa Wananchi wa Arumeru Mashariki, wanaomba kuuliza mbunge wao Joshua Nassari kafikia wapi kwenye ahadi yake aliyotoa wakati wa kampeni Arumeru Mashariki.Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari alitoa ahadi kwa wapiga kura wake Wananchi wa Arumeru Mashariki, kuwa wakimchagua kuwa mbunge wao Arumeru Mashariki atashusha bei ya sukari ndani ya miezi miwili.Wananchi wapenda maendeleo Arumeru Mashariki wanahoji lini bei ya sukari itashuka kwenye jimbo lao.
Umbea mwingine si mzuri. Je waweza kutujuza ni wananchi wa kijiji/Kata/Tarafa gani na mkutano wao wa kutoa madai hayo ulifanyikia wapi, na lini?Mimi nipo Arumeru mashariki, madai kama hayo sijayasikia.Nilitegemea ungemuliza Kiwete maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi na si kuulizia sukari.
 
Kumbe wameuliza hilo moja tu la bei ya sukari. vipi hizo 69 ?

Mkuu kwa hiyo Joshua Nassari kapata Excuse? Sasa kwanini mnawadanya wananchi kuwa mtataka kuwakomboa wakati ni uongo.
 
Ama kweli, "Mtu Mpumbavu hata ukimtwanga kwenye kinu pamoja na ngano upumbavu wake haumtoki". Kwahiyo kudanganya kwa Mkwerre ni bora kuliko wa Nassari? Hivi Wanaarumeru Mashariki wakishushiwa bei ya sukari ilhali Watz wengine bei inaendelea kupaa, ndio utakuwa umetatua tatizo la Watz? Kipi bora, kushusha bei ya sukari nchini kote au kushusha Arumeru Mashariki tu? Na kama nchi nzima bei haijashuka, wa kumuuliza ni Nassari au Mkwerre na timu yake ya Magamba? Mbona unakuwa kama sio m.p.u.m.b.a.v.u vile???????????

Wewe Ndugu mbona unaongea kitu usicho kijua? Je kunauongo mkubwa na mdogo?
Ninashukuru kwa kukubali kuwa alindanganya.
 
Usiseme wananchi sema wewe pekee yako. Sisi bado tunamatumaini na CCM sio CHADEMA. Nasikia kunaviongozi wa chadema walishawahi kuchoma Benk kuu. Hivi ni kweli?
No, ukweli ni kwamba pale Benki Kuu kuna kitu kinaitwa EPA ndio kilifichuliwa, wahusika wakuu ni Mkwerre na vidagaa wengine kama Mweka Hazina wa Magamba kule Kigoma! Haikuishia hapo tu, kuna twiga walitoroshwa, MEREMETA, TANGOLD, RICHMOND/DOWANS, Kukodi Ndege aina ya Airbus pale ATCL, Kushonesha sare kule China, Ununuzi tata wa Rada na Ndege ya Rais, Mikataba ya unyonyaji kwenye Madini kama ule wa Buzwagi, jamani wengine endeleeni nimechoka kuandika! Ila yote haya yalifanywa na ANNAEL na wala sio CCM, CHADEMA, CHAUSTA, JAHAZI ASILIA, CUF, UDP, UDPD, APPT MAENDELEO, NCCR-MAGEUZI, CCK, DP, n.k! Pambaf zako!
 
Bei ya sukari kule Arumeru ni tsh ngapi? Na kule Mosì je? Vp Dar? Au Morogoro? Znatofautiana?
 
Wewe Ndugu mbona unaongea kitu usicho kijua? Je kunauongo mkubwa na mdogo?
Ninashukuru kwa kukubali kuwa alindanganya.
Kwanza hicho kwenye italic ndio nini? Pili, umenisikia nikiongea? Mimi naandika ndugu, mbona umeanza kuchanganyikiwa? Tatu, wewe ndio unaandila usichokijua, kuhoji ahadi 1 ambayo mtekelezaji hana hata miezi 3 ofisini na kuacha ahadi zaidi ya 300 za Mkwerre aliyeko madarakani kwa miaka 7 sasa ni utimamu wa akili kweli? Au nyie ndio mahawara wa Mkwerre mnaotoka mapovu kumtetea mtu mwenye akili butu kuliko za maiti?
 
Nina maanisha kuwa Umekubali kuwa mbunge alindanganya.
Kumbuka alisema baada ya "miezi miwili ahadi itatimia" sasa miezi mitatu. Je hajasema uongo?
 
Mkuu kwa hiyo Joshua Nassari kapata Excuse? Sasa kwanini mnawadanya wananchi kuwa mtataka kuwakomboa wakati ni uongo.

Nyani haoni kundule, Nani mwongo wa kupiga hadi afe kama si ccm!
Magamba imemkomboa nani?

mbona inaelekea imekuuma sana Nassari kuchukua hilo jimbo! uliahidiwa nn na hao magamba shwain?
 
No, ukweli ni kwamba pale Benki Kuu kuna kitu kinaitwa EPA ndio kilifichuliwa, wahusika wakuu ni Mkwerre na vidagaa wengine kama Mweka Hazina wa Magamba kule Kigoma! Haikuishia hapo tu, kuna twiga walitoroshwa, MEREMETA, TANGOLD, RICHMOND/DOWANS, Kukodi Ndege aina ya Airbus pale ATCL, Kushonesha sare kule China, Ununuzi tata wa Rada na Ndege ya Rais, Mikataba ya unyonyaji kwenye Madini kama ule wa Buzwagi, jamani wengine endeleeni nimechoka kuandika! Ila yote haya yalifanywa na ANNAEL na wala sio CCM, CHADEMA, CHAUSTA, JAHAZI ASILIA, CUF, UDP, UDPD, APPT MAENDELEO, NCCR-MAGEUZI, CCK, DP, n.k! Pambaf zako!

Mimi ninaongealea kabla hawajang'atuka (GAVANA fulani) aliichoma benki ili kupoteza kumbukumbu na wakasepa na pesa na inasemekana wakaanzisha chama fulani. Sijui ni kweli?
 
Mkuu kwa hiyo Joshua Nassari kapata Excuse? Sasa kwanini mnawadanya wananchi kuwa mtataka kuwakomboa wakati ni uongo.
Hata Mkwerre alipata "excuse" palipotokea Mtikisiko wa Uchumi Duniani, Ukame na cha ajabu hata Tsunami na Milipuko ya Nuclear kule Japan ****** ali-capitalize na kupata "excuse" ingawa ukimtaiti sawasawa hajui hata hayo yote ni nini! Pia, Nassari hawezi kuonekana muongo kwani hana dola wala mamlaka ya kuwalazimisha Magamba wachape kazi, yeye kazi yake ni kuwasemea na kuwatetea Wanaarumeru. Sasa inapotokea anakowasemea hasikilizwi tatizo linakuwa la msemaji au msikilizaji? Mbona Mkwerre aliahidi "Maisha Bora kwa Kila Mtanzania", au alimaanisha kwako wewe Ridhiwan na dada yako aliyefeli Mwanaasha? Kwamantiki hii, Baba yenu huyo si muongo? Mbona unaona kibanzi kwenye jicho la mwenzio wakati boriti iliyoko kwenye jicho lako mwenyewe huiangalii? Wanamagamba, msaidieni huyu ritz, kama kaishiwa na akili basi mkopesheni ikifika 2015 atawarudishia!
 
wanabodi.

Habari tulizozipata kutoka kwa wananchi wa arumeru mashariki, wanaomba kuuliza mbunge wao joshua nassari kafikia wapi kwenye ahadi yake aliyotoa wakati wa kampeni arumeru mashariki.

Mbunge wa arumeru mashariki, joshua nassari alitoa ahadi kwa wapiga kura wake wananchi wa arumeru mashariki, kuwa wakimchagua kuwa mbunge wao arumeru mashariki atashusha bei ya sukari ndani ya miezi miwili.

Wananchi wapenda maendeleo arumeru mashariki wanahoji lini bei ya sukari itashuka kwenye jimbo lao.
wewe arumeru mashariki na wewe wapi na wapi?acha majungu,kama kunatatizo si watauliza wenyewe.ingekuwa kuna kodi ya mdomo,serikali ingepata pesa sana.kunawatu wanwashwa umbea.
 
Watu wengi hawewezi kunyamaza bila kutunga uongo, umesikia wapi hizo habari?au unatufanya hatujui nchi inaendaje, mimi na kaa leganga,pia huyo anayesema kisima ni kimoja ni muongo, jamani tusiweke propaganda sehemu ambayo huijui wala hujawahi fika, chungeni kauli
 
Mimi ninaongealea kabla hawajang'atuka (GAVANA fulani) aliichoma benki ili kupoteza kumbukumbu na wakasepa na pesa na inasemekana wakaanzisha chama fulani. Sijui ni kweli?
Ni kama unamuongelea Mkono vile? Na wakati wanachoma na hatimaye kusepa, Chama cha Magamba kilikuwa wapi? Rais aliyekuwa na mamlaka ya kuwashughulikia alikuwa wa Chama gani? Na baadaye Marais waliofuata walikuwa wa Chama kipi? Sasa kama hayo yote unayoyasema yana ushahidi wa kutosha, mbona Chama cha Majambazi hakijawachukulia hatua watu hao? Au hao watu wameshafariki dunia? Kama wapo, kwanini nyie Magamba msimshinikize Mkwerre ambaye ndiye Rais wenu wa mweisho awashughulikie? Kama yote hayo yameshindikana, huoni kuwa habari yako hii ni uzushi mtupu na uzandiki uliokomaa?
 
Kimsingi,ni uongo wa mchana mbunge kuahidi atashusha bei ya sukari;maana uwezo huo hana yeye binafsi bali kazi yake ni kupiga kelele bungeni ili kodi ishushwe ya sukari na ndipo bei yake ishuke!
Hapa mheshimiwa Nassari aliwaingiza mjini wapiga kura wa arumeru mash.
 
Back
Top Bottom