WanaMzumbe wanajua kuwa wanaibiwa nauli za daladala?


Mchumia Rungu

Mchumia Rungu

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2013
Messages
1,231
Likes
415
Points
180
Mchumia Rungu

Mchumia Rungu

JF-Expert Member
Joined Apr 26, 2013
1,231 415 180
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Bw. A.S.K. Kilima, alitangaza kuwa nauli mpya za daladala kuanzia 12/4/2013 itakuwa kama ifuatavyo:
sh. 400/= kwa umbali wa Km 0-10,
sh. 450/= kwa umbali wa Km 11-15,
sh. 500/= kwa umbali wa Km 16-20,
sh. 600/= kwa umbali wa Km 21-25 na
sh. 750/= kwa umbali wa Km 26-30.

Wakati nauli hizo mpya zikitangazwa, tayari Mzumbe - Mjini nauli ilikuwa ni sh. 900/=! ambayo inadaiwa kuwa imekuwa ikitozwa tangu 2011. Na umbali wa Mzumbe mjini ni Km 19.6. Nimejaribu kucheck katika milango ya daladala hizo nimekuta wengine wameandika nauli ni sh. 1000/=, wengine sh. 900/= na wengine wamepata kigumizi wameandika sh. 00/=! Na nauli inayotozwa katika daladala hizi ni sh. 1000/=

Hali hii imenifanya nijiulize maswali mengi bila majibu. Hivi hali hiyo ni wenye daladala au madereva na makondakta ndio wameamua? Uamzi huo ni kuwa wamiliki wa usafiri huo wa umma wako juu ya sheria? Morogoro kuna SUMATRA au hakuna! Watu kama wanaoibiwa nauli ama kwa kujua au kwa kutojua, wasaidiweje? Ni sheria gani inawashitaki ama wenye magari kwa kuwaibia watu nauli na kuvunja kanuni na taratibu za SUMATRA au SUMATRA kwa kushindwa kuwatetea abiria wanaoibiwa nauli ama kwa kujua au kwa kutokujua?

Wadau naomba tupeane mawazo.
 

Forum statistics

Threads 1,275,055
Members 490,894
Posts 30,531,653