Uchaguzi 2020 Wanamuziki watakiwa kuhamasisha amani wakati wa kupiga kura

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,874
WANAMUZIKI nchini wametakiwa kuhamasisha amani katika uchaguzi mkuu na kwenda kupiga kura ifikapo Oktoba 28 ili kuwachagua viongozi wanao wataka.

Ombi hilo linetolewa na Rais mpya wa Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO) Erick Kisanga wakati akizungunza na waandishi wa habari jijini Arusha.

“Nina wahimiza wanamuziki wote hapa nchini wajitokeze kupiga kura kwa Rais, wabunge pamoja na madiwani katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwezi huu” alisema.

Kisanga amewaomba watanzania kuombea uchaguzi huo ili Mungu atujalie kuwapata viongozi watakaoliongoza vema Taifa letu la Tanzania na kuwaomba wanamuziki kuendelea kutunga na kuimba nyimbo za kuhamasisha amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

“Wanamuziki ni watu muhimu kupeleka ujumbe haraka kwa wananchi kupitia nyimbo zao hivyo niwaombe katika hizi siku chache zilizosalia wahamasishe kujitokeza kupiga kura na kulinda amani ya nchi.

Kisanga alisema kila mwanamuziki mwenye sifa ya kupiga kura ajitokeze na kadi yake ya kupigia kura katika kituo alichojiandikisha ili kutimiza haki yake ya msingi na ya kikatiba.

Aidha Kisanga alilisitiza umuhimi wa kila mtanzania kuzingatia misingi ya amani na utulivu wakati mchakato huo ukiendelea, ikiwemo kufika mapema kituoni kupiga kura na kuondoka kuelekea kwenye majukumu mengine kwa mujibu wa sheria za uchaguzi ili kuepusha madhara au viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyoweza kujitokeza.
 
Kwa nini wasihamasishe haki ambayo ndio huleta amani ? Chokochoko zote zinatokana na viashirio vya ukosefu wa haki kwenye uchaguzi huu
 
Huyo anatumika kama Co ndo M inayotumiwa kunyima maisha watoto halafu badae inaenda kutupwa jalalani
 
Chadema imekataliwa na kila mwanamuziki, hii gundu ya lissu sijawahi kuiona duniani
 
Erick Kissanga, wahimize wanamuziki wahamasishe HAKI ambayo ndio mama wa AMANI. Hizi unazofanya ni propoganda za CCM. Wao wanafikiri amani hudondoka kama mvua, yaani kwa kudura ya Mungu!! Amani hujengwa, na msingi wa amani ni haki.
 
Back
Top Bottom