Wanamikakati wa CCM Mjifunze kilichotokea Zanzibar, Mtambue mabadiliko hayazuiliki na Bara sio Unguja

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Huo ujumbe uende moja kwa moja kwa wana mikakati wa CCM na washauri wa chama na Serikali.

Mtakosea sana kufanya mbinu zenu za kuzorotesha Upinzani kwa kutumia mbinu za Zanzibnar huku Bara.

Kwa hulka Wazanzibari ni wapole sana lakini ni wamejaaliwa uelewa wa kisiasa. CCM imetumia njia nyingi kutaka kuuwa Upinzani Zanzibar tokea miaka ya 1995 hadi sasa lakini wameshindwa kutokana na uelewa wa siasa kwa Wazanzibari. Vyenginevyo wangekwisha potea lakini ni kinyume chake.

-Mbinu za kuwagombanisha watu kutokana na maeneo hazifai
-Mbinu za kuwabagua watu fulani hazifai
- Mbinu za kuwabambikizia jinai hazifai
- Mbinu za kujeruhi hazifai.
- Mbinu za kuwaweka watu selo na magerezani hazifai.

Mbinu hizo hapo juu zilitumiwa sana Zanzibar ili kuwatisha watu na kunyamazisha. Lakini hazikufanikiwa licha ya Upole wa Wazanzibari. Zilitumika kwa watawala na CCM wakiamini wana uwezo wa KUDHIBITI ikitokea jamii kuripuka kutokana na kwanza Uhaba wa wakaazi, Upole, kuwepo kwa mgawanyiko wa visiwa na advantage ya Zanzibar kuwa visiwa.

Watawala waliamini uwepo wa mipaka ya kibahari haiweezi kuambukiza athari upande wa Bara na kwa zaidi ya miaka 30 sasa CCM imefanya figisu Zanzibar.

Licha ya yote hayo, CCM mtambuwe kuwe Zanzibar hata hivyo ililazimika kuwe na miafaka hewa 3, na vurumai zisizoisha na wakati mwengine amani kutoweka na mshikamano kuharibiuka ili tu CCM itawale. Bara hamkujali hiyo hali na watawala walijiona salama sana. Jumuiya ya Kimataifa inajuwa hali hiyo na nyinyi mnajuwa hali hiyo. Kinachoendelea Zanzibar ni Majaaliwa tu lkn mnajuwa nafasi ya CCM inavyotegemea Dola na si wananchi. Jee mnadhani BARA inaweza ikasurvive ?

Jee BARA inaweza kuservive Dhoruba la Zanzibar?
Jibuni wenyewe

Lakini angalieni Bara kuna Makabila tofauti na Dini tofauti
Angalieni Bara hakuna Upole kuna ujinga wa siasa na uelewa mdogo
Angalieni Bara hakuna mipaka ya visiwa kuna mikoa iliyoshikana na jamii mchanganyiko
Angalieni Uwezo wa uvumilivu na hulka za watu zilivyo tofauti baina ya Bara za Zanzibar
Angalieni wingi wa watu Bara.

CHONDE CHONDE
Kamwe msijisahau mtaingamiza nchi kwa kuamini mbinu za ZANZIBAR ZITAFAA BARA KUIWEKA CCM MADARAKANI.
Hawa watu wana background tofauti, siku wakiamka itakuwa shida.

Tambueni kuazia 2010 - 2015 uelewa wa siasa umepiga hodi rasmi Bara na mwaka 2015 na kuendelea mnaona CCM inavyopata Tabu Bara.

Tafuteni njia nzuri ya kufanya siasa za kistaarabu na mujarabu kwa mujibu wa Mazingira.

Nawaombeni kuzingatia kuwa Bara sio Unguja.

Waelewa wanielewe kabla hayazuka yasioyotabirika.

Tambuweni mabadiliko ni Lazima na mikakati inatofautiana sana kutokana na Mazingira.

CCM bara inahitaji sana maridhiano kama hatua ya Kwanza na wala sio hatua ya nne kama ilivyotokea Zanzibar.

Niko tayari kukosolewa.

Kishada.
 
CUF imetulia baada ya mamluki maalim seif kutimuliwa na wanachama

Vyama vya upinzani bara ni mihemuko ya kisiasa tu hawana ushawishi
 
Usijidanganye Mtanganyika Wazanzibar siasa ipo damuni na si katika vyama tutawapiganao siku zote mbakie kuchukua Nchi kwa Mtutu nao pia una mwisho wake
NIMESEMA
 
Hapo ndipo unapoonekana umuhimu wa walinda usalama wetu kuwa na uhodari wa kupima mambo na kushauri. Upepo unaovuma kwenye hii ishu tu ya Serikali za Mitaa sio nzuri kwa nchi,na hali inaweza ikaambukiza.

Hebu tafakarini hao wawekezaji wanaposikia huu mvurugano kweli watapata imani ya kuekeza ? si wataona Tanzania kuna Risk.?

Lakini tazama namna kulivyojengwa tension Tanzania kuelekea 2020? Hivi hao wataalamu wetu wa TISS wako wapi? Hawaoni hatari ya Uchumi wetu kuathirika na kuwapa nafasi majirani na competetors wetu?

Utulivu wa siasa ya ndani ni muhimu kwa maslahi ya kiuchumi na ushawishi.
 
CCM imechokwa na sasa watawala wanalazimisha kupendwa. Wakati wanafanya figisu kwa wapinzani ndio wanaharibu nchi kumbe. Kwa nchi kama Tanzania (Bara) kufanya figisu ya Kuwakata wapinzani kwa maelfu kwenye ngazi za Chini huko ni kukosa weledi wa kisiasa. Unapandikiza chuki kwenye level za chini huko ambako kuna watu wengi. Hili Serikali na watawala hawakuliona wao waliona haja ya kuibeba CCM tu na sio nchi.
 
...........

..........
Ndio hao walioshauri Jafo alambe matapishi yake. wakati its too late
 
CUF imetulia baada ya mamluki maalim seif kutimuliwa na wanachama

Vyama vya upinzani bara ni mihemuko ya kisiasa tu hawana ushawishi
Haya ikiwa ni chama ameachiwa Lipumba uangalie act wazalendo ilivyo sasa.
 
Huo ujumbe uende moja kwa moja kwa wana mikakati wa CCM na washauri wa chama na Serikali.

Mtakosea sana kufanya mbinu zenu za kuzorotesha Upinzani kwa kutumia mbinu za Zanzibnar huku Bara.

Kwa hulka Wazanzibari ni wapole sana lakini ni wamejaaliwa uelewa wa kisiasa. CCM imetumia njia nyingi kutaka kuuwa Upinzani Zanzibar tokea miaka ya 1995 hadi sasa lakini wameshindwa kutokana na uelewa wa siasa kwa Wazanzibari. Vyenginevyo wangekwisha potea lakini ni kinyume chake.

-Mbinu za kuwagombanisha watu kutokana na maeneo hazifai
-Mbinu za kuwabagua watu fulani hazifai
- Mbinu za kuwabambikizia jinai hazifai
- Mbinu za kujeruhi hazifai.
- Mbinu za kuwaweka watu selo na magerezani hazifai.

Mbinu hizo hapo juu zilitumiwa sana Zanzibar ili kuwatisha watu na kunyamazisha. Lakini hazikufanikiwa licha ya Upole wa Wazanzibari. Zilitumika kwa watawala na CCM wakiamini wana uwezo wa KUDHIBITI ikitokea jamii kuripuka kutokana na kwanza Uhaba wa wakaazi, Upole, kuwepo kwa mgawanyiko wa visiwa na advantage ya Zanzibar kuwa visiwa.

Watawala waliamini uwepo wa mipaka ya kibahari haiweezi kuambukiza athari upande wa Bara na kwa zaidi ya miaka 30 sasa CCM imefanya figisu Zanzibar.

Licha ya yote hayo, CCM mtambuwe kuwe Zanzibar hata hivyo ililazimika kuwe na miafaka hewa 3, na vurumai zisizoisha na wakati mwengine amani kutoweka na mshikamano kuharibiuka ili tu CCM itawale. Bara hamkujali hiyo hali na watawala walijiona salama sana. Jumuiya ya Kimataifa inajuwa hali hiyo na nyinyi mnajuwa hali hiyo. Kinachoendelea Zanzibar ni Majaaliwa tu lkn mnajuwa nafasi ya CCM inavyotegemea Dola na si wananchi. Jee mnadhani BARA inaweza ikasurvive ?

Jee BARA inaweza kuservive Dhoruba la Zanzibar?
Jibuni wenyewe

Lakini angalieni Bara kuna Makabila tofauti na Dini tofauti
Angalieni Bara hakuna Upole kuna ujinga wa siasa na uelewa mdogo
Angalieni Bara hakuna mipaka ya visiwa kuna mikoa iliyoshikana na jamii mchanganyiko
Angalieni Uwezo wa uvumilivu na hulka za watu zilivyo tofauti baina ya Bara za Zanzibar
Angalieni wingi wa watu Bara.

CHONDE CHONDE
Kamwe msijisahau mtaingamiza nchi kwa kuamini mbinu za ZANZIBAR ZITAFAA BARA KUIWEKA CCM MADARAKANI.
Hawa watu wana background tofauti, siku wakiamka itakuwa shida.

Tambueni kuazia 2010 - 2015 uelewa wa siasa umepiga hodi rasmi Bara na mwaka 2015 na kuendelea mnaona CCM inavyopata Tabu Bara.

Tafuteni njia nzuri ya kufanya siasa za kistaarabu na mujarabu kwa mujibu wa Mazingira.

Nawaombeni kuzingatia kuwa Bara sio Unguja.

Waelewa wanielewe kabla hayazuka yasioyotabirika.

Tambuweni mabadiliko ni Lazima na mikakati inatofautiana sana kutokana na Mazingira.

CCM bara inahitaji sana maridhiano kama hatua ya Kwanza na wala sio hatua ya nne kama ilivyotokea Zanzibar.

Niko tayari kukosolewa.

Kishada.
Mkuu leo umeandika. Mungu akubariki. Naomba wengine wasome vizuri. tutakukumbuka.
 
Hapo ndipo unapoonekana umuhimu wa walinda usalama wetu kuwa na uhodari wa kupima mambo na kushauri. Upepo unaovuma kwenye hii ishu tu ya Serikali za Mitaa sio nzuri kwa nchi,na hali inaweza ikaambukiza.

Hebu tafakarini hao wawekezaji wanaposikia huu mvurugano kweli watapata imani ya kuekeza ? si wataona Tanzania kuna Risk.?

Lakini tazama namna kulivyojengwa tension Tanzania kuelekea 2020? Hivi hao wataalamu wetu wa TISS wako wapi? Hawaoni hatari ya Uchumi wetu kuathirika na kuwapa nafasi majirani na competetors wetu?

Utulivu wa siasa ya ndani ni muhimu kwa maslahi ya kiuchumi na ushawishi.
Mkuu ,Umeuchoma san moyo wangu .
 
CCM imechokwa na sasa watawala wanalazimisha kupendwa. Wakati wanafanya figisu kwa wapinzani ndio wanaharibu nchi kumbe. Kwa nchi kama Tanzania (Bara) kufanya figisu ya Kuwakata wapinzani kwa maelfu kwenye ngazi za Chini huko ni kukosa weledi wa kisiasa. Unapandikiza chuki kwenye level za chini huko ambako kuna watu wengi. Hili Serikali na watawala hawakuliona wao waliona haja ya kuibeba CCM tu na sio nchi.
Akili yako ni kubwa san ndugu kwa haya unayoyanena hapa.
 
CUF imetulia baada ya mamluki maalim seif kutimuliwa na wanachama

Vyama vya upinzani bara ni mihemuko ya kisiasa tu hawana ushawishi

Wanatumia nguvu kubwa kuuza wagombea wao kwa Wapiga kura kuwa ni waadilifu ndio hao hao wanarudi kuwaambia ‘... kanunuliwa na Ccm ..’
 
Asante ndugu mtoa mada. Ama kweli viongozi wa CCM wamefanya na wataaendelea kufanya watakavo wakijua hadi kuwa wananchi hawawezi kufanya lolote. Lakini hiyo ni ndoto tu. Binadamu huchoka na akichoka huwezi tena kuongea lugha akakufahamu. Tuangalie Mobutu alifika wapi na aliifikisha wapi nchi yake. Tumwangalie Robert Mugabe, alianza vizuri nakumbuka kuenda Harare, ilikuwa mji safi kabisa. Alipoanza kuwanyanganya wawekezaji mali zao, nchi ilifilisika. Zimbabwe imekuwa katika nchi duni duniani kwa siasa za mtu mmoja. South Afrika wameanza kufuata njia ya zimbabwe na kama hawakushituka, tutiona itakavo anguka. Damu za wawekezaji walio uawa afrika kusini lazima zitarudi kujitetea. Sasa Tanzania na CCM yake ndio wanadhani ni wababe, tusubiri dhoruba linalo kuja.CCM na Magu watajitafuta.
 
Back
Top Bottom